Kuna sababu nyingi za kuipigia kura ya hapana katiba inayopendekezwa.
Kati ya sababu hizo ni ubatili wa mchakato wenyewe ambao ulihodhiwa na ccm, kutokuwa na sifa za msingi za katiba, kutokuwa na muafaka wa kitaifa zaidi ya kulinda maslahi ya ccm na baadhi ya wabunge hasa wasio na elimu na uwezo, kuacha mambo yote ya msingi yaliyopendekezwa na wananchi nk.
Lakini pia katika kuipitia katiba yenyewe inayopendekezwa nimeona mapungufu mengi, hasa katika muundo wa serikali ambao una mikanganyiko mingi ibara za 1(1), 75, 76, 77 na 163.
Katiba hii pia bado inapingana katika maeneo mengi na Katiba ya Zanzibar ya mwaka (1984) toleo la 2010.
Tume huru ya uchaguzi ni jina tu, lakini sio huru - viongozi wake wote wanateuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa ccm - Ibara 217(2) na 222(1).
Nadhani ilikuwa vema kwa Bunge Maalumu kuzingatia maoni ya Tume ya Jaji Warioba.