Goodrich
JF-Expert Member
- Jan 29, 2012
- 2,091
- 1,178
Haijaweka mfumo wa kutenganisha mamlaka (separation of powers) na hivyo inatoa fursa kwa matumizi mabaya ya madaraka (abuse of powers)
Imeweka mazingira kwa viongozi wa umma kuwa na fedha nje ya nchi ibara 29(2)(b).
Maslahi ya taifa la leo na kesho hayakuwekwa mbele na BMK kwa lengo la kuwalinda wabunge wasio na elimu ya kutosha. Mfano: Katiba pendekezwa ilitaka mbunge awe na kiwango cha elimu ya angalau kidato cha nne, lakini pendekezo hilo likaondolewa.
Katiba hii pia bado inapingana katika maeneo mengi na Katiba ya Zanzibar ya mwaka (1984) toleo la 2010.
Tume huru ya uchaguzi ni jina tu, lakini sio huru - viongozi wake wote wanateuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa ccm - Ibara 217(2) na 222(1).
Lakini pia kuna mambo ya msingi yameachwa kama vile
1. Kutenganisha mihimili ya dola
2. Muundo wa serikali ikiwamo baraza la mawaziri ulipaswa kuwekwa kwenye katiba
3. Kuweka malengo, dira na sera ya kitaifa inayopaswa kutekelezwa na dola. Kazi hii kwa sasa vimeachiwa vyama vya siasa na ndio sababu kila baada ya miaka 5 au 10 tunaanza upya. Vyama vya siasa kazi yao ingekuwa ni kuelezea wanavyoweza kutekeleza sera zilizopo kwenye katiba.
Nadhani ilikuwa vema kwa Bunge Maalumu kuzingatia maoni ya Tume ya Jaji Warioba.
N.B
Separation of powers is a political system in which Legislative, Executive, and Judicial are kept distinct in order to prevent abuse of power and promote a system of checks and balances.

Tuikatae katiba hiyo kwa kuwa :
1. Inaruhusu watumishi wa umma kuwa na fedha nje ya nchi - ibara 29(2)(b)
2. Imempa Rais madaraka makubwa sana na haina separation of powers, mfano;
- Rais ni sehemu ya Bunge 129(1)
- Rais anateua Katibu wa Bunge 151(1)
- Rais anateua wabunge 15 ibara 129(2)(b)(c)
- Rais anateua Jaji mkuu 175(1)
- Rais anateua majaji 176,177
- Rais anateua mkuu wa mahakama 202 (1)
- Rais anateua tume ya utumishi 210 (1)
- Rais anateua Mwenyekiti na viongozi wa Tume ya Uchaguzi 217(2)
- Rais anateua wajumbe wa kamati ya uteuzi 218(1)
- Rais anateua Mkurugenzi wa Uchaguzi 222(1)
- Na taasisi nyingine zote ambazo ni nyeti zipo chini ya Mwenyekiti huyu wa ccm ie 225,226,243,270,273,276 nk
3. Katiba hii ina jumla ya marais 6 ibara 80,99,164
4. Pia ibara nyingi hasa zinazohusu muundo wa nchi zinakinzana ie 1(1), 75, 76, 77, 163.
C. Tukishindwa kuamua sasa au mwaka huu kuwa na msimamo mmoja bila kujali vyama vyetu basi tutaendelea kuwa na nchi isiyoeleweka na isiyo na utaifa.