Sababu za kwanini bei za vyakula Tanzania zipande mara dufu

Sababu za kwanini bei za vyakula Tanzania zipande mara dufu

feisar wa moro

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2020
Posts
365
Reaction score
858
Wakuu sina mengi hizi ni sababu zangu kutokana na hali halisi iliyopo huku mashambani kunakofanyika kilimo..( nipo kilombero morogoro)

ZAO MPUNGA

Bei ya kukodi shamba Ni laki 2 kutoka laki 1 msimu uliopita

Bei ya kuvuruga ni laki moja na 40 kutoka 80elf msimu uliopita

Bei ya kupanda ni laki na 20 kutoka 80elf season iliyopita

Ng'olezi laki 1

Dawa za kuua magugu elf 20 kwa dumu la lita 1 kutoka elf 10 msimu uliopita

Mfuko wa mbolea ya kukuzia 50kg unauzwa laki moja na 80 kutoka 80elf msimu uliopita

Mbolea ya kuzalishia laki na 30 from 60elf

Gharama za uvunaji,usafirishaji zimepanda hadi mara tatu ya msimu uliopita

Kifupi gharama zimekuwa juu mara mbili ya msimu uliopita na inawekana hizo pembejeo zikawa juu zaidi pindi msimu mpya ukianza
 
Hali ya hewa mbaya kuna mother wangu mkubwa kwa kilimo chake cha kuunga unga anapatagaga gunia kuanzia 30 kwa heka 5 huko Kahama .Msimu uliopita kapiga kisado.
 
Back
Top Bottom