Siku nzuri wakuu!
Watasha wanasema "learning is the continuous process from cradle to grave" kujifunza ni kitendo cha kuanzia unazaliwa hadi unakufa..hakikomi..Leo tujifunze hiki kinachowasibu jamaa Tanzania one hawa a.k.a "John kisomo" au "somasoma jinsi wanavovurugwa na maisha kuliko sisi akina Ngumbaru.
Kila kitu kina haja ya kufanyika kwa wastani kikizidi ni tatizo..too much of anything is harmful. Hata Akili zikizidi sana huwa inakuwa tatizo kwa sababu mhusika anavuka kwenye akili ya kawaida na kuingia kwenye wehu na ukichaa kutokana kwamba anakuwa sio normal tena bali ni abnormal.. Ingia hapa nilifafanua zaidi juu yao kwa kina
Hii ndio sababu Magenius hawawezi kuwa matapeli
Kwa ishu ya hawa magenius na wale highly intelligent people wao wanakuwaga na matatizo haya hapa; wako hivi;
Mwanzoni kabisa Walipokua wanasoma huko Mzumbe, Mazengo, na kutandika mamisonge non stop huku sisi tukitandika mafafa aka fatuma waliamini kwamba wao ni special and noble people e.t.c walijua watafanikiwa kwa ubwete after school, waliamini kabisa watapata kazi nzuri, Mkwanja mrefu, Mama chanja chuma sana, e.t.c unfortunately baada ya masomo sasa wakiingia mtaani wanakutana na maisha magumu kama ugoko wa anko halfan Ngasa yasiyo tambua kabisa +AAA. Then wakiona matarajio yao hayajakamilika hapo ndipo wanapojikana, kujihukumu na kujishambulia wenyewe... Na wana jaribu kutafuta option hapa ndipo unaposikia engineer aliekuwa Tanzania one O-level hadi chuo kikuuu anabet kwa Mhindi na masela ambao wasio na vision wala mission wenye ngeu za kutosha usoni, wakiwa vifua wazi vitovu vikubwa kama lile lisehemu la kutafutia stesheni kwenye redio Mbao za zamani hakudhani kama atakutana na watu kama hawa maishani hapa unazidi kuvurugwa na kuwa psycho na violent person bila sababu yeyote ile yaani ukimsemesha tu anakuattack kama Mcambodia wa Vietnam....Ahahaha!
Wako violent na depressed sana sababu wanaona wale mamgumbaru waliopata fatuma saba O-level ndio wanapata nafasi nyeti serikalini za uongozi ilhali wao wakijitahidi sana wanakuwa ma engineer wa kurepair vyoo vya serikali na halmashauri maana ma engineer wa madaraja na majengo nyeti ni macho madogo ndugu zake na Jackie Chan.
Huwa hawawezi kutengeneza marafiki kihurahisi sababu ubongo wao unafikiri kitu kimoja pekee, masomo yao tu... Na kitaalamu ni wagonjwa wa autism na bipolar disorder inayowalazimu wawe alone and sad with deep concentration... Lakini hapo hapo akitokea mtu mwenye maneno au Maandishi matamu ya kitapeli wanawahi sana kuelekea kibra maana ubongo wao umechoka kusikia na kujadili vitu vigumu muda mwingi hivyo wanahitaji kusikia na kusoma vitamu ili Ku easy mind zao. Sasa kuna genius mmoja wa Enginnering TO nguli huyu alisikia ishu za Forex zikiwa ziko sugarcoated na maneno matamu ya kibazazi akaingia mzima hawakumchelewesha wakampa na special desk la kutredia pale pale ofisini ili wazae nae vizuri. Kilichotokea hadi Leo hana hamu. Nikajitosa kumuokoa maana nilisanuka mapema nikampa maneno machungu yasiyo ya kitapeli very raw and undigested jinsi anavyochakatwa.. Kama ilivyo kawaida neno lenye ukweli huwa halina utamu na neno lenye fiksi huwa tamu sana kama alivyosema Fid Q. Kuanzia siku hiyo ananiita mnafiki...(LINAFIKI). Ahahaha!
Maisha ndivyo yalivyo wenye akili wamelaaniwa na akili zao wenyewe na zimegeuka kuwa ghost kwao badala ya msaada maana wamejifunza elimu ya darasani na kuacha elimu ya mtaani ndio maana wanapanga foleni Wasafi record wakiomba nafasi ya kuwa wakala wa kuuza karanga kwa mtu ambae haijui A+ ya darasani ikoje.
Lakini ndivyo inavyokuwaga maana magenius na intelligent wengi hata kuoa hawakuoa na wengi waliishia kujiua ili kukwepa ile solid depression and killer anxiety ya intensity ya kuyasaka maisha mazuri bila mafanikio. rejea ishu ya Vincent Van Gogh, Michelangelo, Da Vinci, Newton, e.t.c...sijui wewe unawasaidiaje? Kwa upande wangu nawapa suicide help line ya USA hii +1 37478494366361 kwa msaada zaidi yakiwafika na kutaka kujitoa uhai, USA wanasaidia saana nikiwapa ya bongo haitawasaidia maana sio professional. Ahahaha! Na ninasisitiza siwaonei donge kwa ufaulu wao mkubwa bali kutokana na huu msemo wa kiingereza unaosisitiza kwamba "ignorance is bliss" kuna raha flani hivi sometimes kwenye kuwa na akili ya kawaida tunapata muda wa kutosha wa kufikiri kwa amani na Uhuru bila kujichosa na yale MaQuantum physics.
Niko kwenye traffic jam nimeona nikavurumushe haka kasomo maana nimevurumushiwa na Mimi kabomu huko. No fight tonight tunaelimishana tu kwa facts in issue.
Bring it on!. [emoji112][emoji108]