Sababu za kwanini MaT.O (Tanzania one) hawafanikiwi kimaisha!?

Sema kweli jamani kwahiyo ni tajiri wa nyuma ya keyboard
Ndio ukifuatilia nyuzi zake na michango yake humu utagundua uhalisia wa maisha yake
Kitu pekee anachojivunia ni A alizopata miaka kadhaa nyuma
 
Inategemeana na wewe kwako definition ya mafanikio unaiweka vipi. Kwanza hujatoa mifano hai ya hao maTO unaosema hawajafanikiwa kimaisha,

Pili mtu yoyote mwenye kumiliki nyumba,uhakika wa kula, kuisadia familia yake pale anapoitajika, kusomesha watoto wake i.e kuwa na uhakika na kupata mahitaji yake anytime tayari maisha kayapatia. Labda ungetoa mfano nani kati yao ni ombaomba

Tatu kubeti hakuna uhusiano wowote na utajiri ama umaskini wa mtu, ndo maana mpka leo hii Floyd myweather, Michael Owen nk wanabet..

Mwisho lazima utambue elimu ni njia tu ya kupata mafanikio maishani kwa kumuwezesha mtu kutatua changamoto mbalimbali katika jamii yake ila si lazima iwe hivyo kwani kuna factors nyingi zinaingilia kati baada ya elimu husika. Kama ambavyo kuna wafanyabiashara, wavuvi ama wakulima wengi wanafeli katika kazi zao.

Ukiwa na mawazo mgando kama yako hata watoto wako hutawapeleka shule na cha moto mtaani watakiona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…