Wanabodi,
Leo ndio siku ya Interview ya kujiunga na Shule ya Sekondary ya Marrian Girls iliyopo Bagamoyo.
Interview hiyo inahusisha mtihani wa masomo matatu ya Hisabati, Kiingereza na Maarifa ambayo wataifanya kwa masaa 4 mfulilizo. Imeelezwa mtihani huo ni mgumu mara 10 kumi zaidi ya mtihani wa taifa wa darasa la 7 uliofanyika wiki mbili zilizopita ili watakaofaulu ndio watakao chaguliwa kujiunga na shule hiyo.
Jumla ya waombaji ni 3000 wakigombea nafasi 150 tuu!. Kila muombaji amelipia fomu ya kujiunga kwa Sh. 15,000/= hivyo kwa zoezi hilo la interview pekee, shule hiyo imeshajiingizia Shilingi Miilioni 45 ya chap chap!.
Kufuatia interview hiyo, asubuhi ya leo imeanza kwa mashindano ya magari kuelekea Bagamoyo na mjini Bagamoyo penyewe ndio hapafai kabisa kwa makundi ya watu. Ziko familia zenye uwezo wamekuja na magari mawili kuanzia baba, mama, bibi, babu, mjomba, shangazi, na watoto wa familia wakimsindikiza mtoto kufanya interview as if wakiwa wengi basi mtoto wao ataongezewa maksi!.
Magari zaidi ya 1000 kuizunguka Marian Girls ni kizungumkuti, hivyo Traffic police wametanda kuyaongoza magari kwa kuyazuia kukaribia eneo la shule hivyo wanafunzi kulazimika kutembea nusu maili kuifikia shule. Hao traffic wakiona gari za kipesa pesa ziliruhusiwa kupita ndani kwa kihisiwa ni waheshimiwa!.
Na tukirudi mitaani Bagamoyo leo, kila hoteli, kila mgahawa, kila kioski, kila chini ya mti kwenye kivuli ni parking za magari!. Waliokuja ki-pikiniki wamekuja,waliokuja ki beach beach wamekuja na mahotelini hakuna chochote watu wameshakomba kila kitu!.
Kwa wale watoto wa familia za kula kuku sio mpaka siku ya sikukuu au soda sio mpaka wakija wageni au mayai mpaka wakiogua na matunda mpaka waambiwe na dakitari, ile kutembezwa tuu nusu maili kabla ya kuingia chumba cha mtihani ndio elimination test ya kwanza kwa wabafunzi wenye uwezo wa wastan kufanya mtihani wakiwa tayari exhausted hivyo kufanya vibaya.
Kwa idadi hiyo ya wanafunzi 3000 kugombea nafasi 150 inamaanisha watakaofaulu ndio top most cream hivyo wanakuwa ni wepesi kufundishika ukijumlisha na spoon feeding ya kutafuniwa kila kitu na wao kupewa kumeza, then no wonder ni kwa nini St. Marrian Girls wanatoa Div 1 za darasa zima na kuongoza kwenye ufaulu kitaifa.
Swali kwa nyie wanafunzi wa kisasa ambao mtakutana na hivi vichwa vya Marrian Girls jee ni vichwa kiukweli mpaka huko mavyuoni?.
Nakumbuka tukiwa UD shule zilizokuwa zikiongoza wakati huo zilileta nusu ya darasa kupiga Law. Tangu registration pale chini ya Mdigrii hadi faculty walikuwa wakipiga ung'eng'e tuu as if Kiswahili hawajui yaani hadi kucheka walikuwa wakicheka kizingu!. Hata ukimuuliza kitu kwa Kiswahili kwanza atakuuliza " what?" ili swali lako uliulize kwa Kiingereza na ukisisitiza kwa Kiswahili ndipo atajilazimisha kwa "you mean" nyingi na ma "what na what not" kibao ili mradi ni kiswanglish kwa kwenda mbele!. Sie wengine tukawaona kusema ukweli wenzetu wanaakili!. Kufika matokea ya mwisho ya mwaka wa kwanza, wanafunzi kumi naa wakapigwa Disco, wachache waliobakia nao wakalabwa disco mwaka wa pili, na sikumbuki hata ni wangapi walifanikiwa kumaliza ila tukikutana nao mitaani kwa sasa ni Kiswahili safi kwa kwenda mbele!.
Naomba Kuwakiliza.