UPDATE
Matokeo ya mtihani wa kujiunga Marrian Girls ya Bagamoyo yalitoka kesho yake Jumapili jioni kwa wazazi wa watoto wao walioshinda kujulishwa kwa simu na kesho yake Jumatatu asubuhi yalibandikwa kwenye ubao wa Matangazo wa shule na kwenye ile ofisi yao iliyopo Msimbazi Center.
Jumla ya wanafunzi 120 ndio waliochaguliwa cut off point ni wastani wa marks 35 chini ya 50.
Nimeishuhudia marking scheme yao, mtihani wao sio tuu ulikuwa mgumu bali pia ulikuwa a bit tricky ili wanafunzi wale tuu wenye IQ above average ndio waliofaulu.
Nimethibitisha beyond reasonable doubt kuwa mchakato wa kuipata Marrian Girls ya Bagamoyo ni mchakato wa haki wenye maximum transparency na waliochaguliwa wote walistahili, hakuna upendeleo wa aina yoyote na hakuna deals.
Ila pia niliposoma majina ya ubini ya wengi walioshinda idadi kubwa ni majina ya watu kutoka makabila fulani fulani ambayo yanatambulika kirahisi. Lazima tukubali, tukatae, huu ni ukweli isiopingika kuwa japo Watanzania ni wamoja na hatuna ukabila, ila pia yapo makabila ambayo yamebarikiwa kwa wengi wao kuwa na akili kuliko makabila mengine.
Pia mtihani wa kujiunga na shule hii haukubagua dini, yaani watu wa dini zote wamefanya interview ila kwenye matokeo very very unfortunately majina mengi ni ya dini fulani na sikubahatika kuyaona majina ya dini nyingine!.
Mwalimu alipofanya affimative action ili watu wa makabila yote wapate fursa sawa za elimu, pia alitakiwa afanye vivyo hivyo kwa affimative actions ili watu wa dini wapate fursa sawa kupata elimu bora!
Naomba Kuwakilisha.
Pasco.
Mimi nadhani hayo makabila yanachanamkia fursa. Yanawaandaa watoto wao kuweza kukabiliana na demand ya Marian Sec School. Ndiyo maelezo ninayoweza kuyapata. Na sidhani wazazi wengi wana mwamko huo!