Sababu za Marrian Girls ya Bagamoyo Kung'aa!.

Sababu za Marrian Girls ya Bagamoyo Kung'aa!.

UPDATE
Matokeo ya mtihani wa kujiunga Marrian Girls ya Bagamoyo yalitoka kesho yake Jumapili jioni kwa wazazi wa watoto wao walioshinda kujulishwa kwa simu na kesho yake Jumatatu asubuhi yalibandikwa kwenye ubao wa Matangazo wa shule na kwenye ile ofisi yao iliyopo Msimbazi Center.

Jumla ya wanafunzi 120 ndio waliochaguliwa cut off point ni wastani wa marks 35 chini ya 50.

Nimeishuhudia marking scheme yao, mtihani wao sio tuu ulikuwa mgumu bali pia ulikuwa a bit tricky ili wanafunzi wale tuu wenye IQ above average ndio waliofaulu.

Nimethibitisha beyond reasonable doubt kuwa mchakato wa kuipata Marrian Girls ya Bagamoyo ni mchakato wa haki wenye maximum transparency na waliochaguliwa wote walistahili, hakuna upendeleo wa aina yoyote na hakuna deals.

Ila pia niliposoma majina ya ubini ya wengi walioshinda idadi kubwa ni majina ya watu kutoka makabila fulani fulani ambayo yanatambulika kirahisi. Lazima tukubali, tukatae, huu ni ukweli isiopingika kuwa japo Watanzania ni wamoja na hatuna ukabila, ila pia yapo makabila ambayo yamebarikiwa kwa wengi wao kuwa na akili kuliko makabila mengine.

Pia mtihani wa kujiunga na shule hii haukubagua dini, yaani watu wa dini zote wamefanya interview ila kwenye matokeo very very unfortunately majina mengi ni ya dini fulani na sikubahatika kuyaona majina ya dini nyingine!.

Mwalimu alipofanya affimative action ili watu wa makabila yote wapate fursa sawa za elimu, pia alitakiwa afanye vivyo hivyo kwa affimative actions ili watu wa dini wapate fursa sawa kupata elimu bora!

Naomba Kuwakilisha.

Pasco.

Mimi nadhani hayo makabila yanachanamkia fursa. Yanawaandaa watoto wao kuweza kukabiliana na demand ya Marian Sec School. Ndiyo maelezo ninayoweza kuyapata. Na sidhani wazazi wengi wana mwamko huo!
 
Nilibahatika mwaka jana kwenda kumpeleka mtoto kwenye interview ya kidato cha tano. Nilipokuwa pale tulikuta wazazi fulani ambao watoto wao wamemeliza kidato cha nne mwaka juzi wakiomba uongozi wa shule watoto wao wafanye usaili ili wapata kusoma kidato cha tano hapo Mirian. Nilipofuatilia sababu ya wazazi kuomba, niliambiwa kuwa watoto wao walitaka kuanzisha mgomo walipokuwa kidato cha tatu, pamoja na adhabu nyingine, uongozi uliamua kuwa hawataruhusiwa kuendelea kidato cha tano katika shule hiyo. Hii ni dalili moja ya kuwa shule hii ina taratibu wanazozifuata, na hili ni jambo la msingi sana kwenye maendeleo ya mtoto shule. Na sijui hii dhana ya kuwa waalimu wa shule hizo hawana sifa inatoka wapi, tukumbuke kuwa sifa ni jambo moja lakini hata kama una sifa za mwalimu wa kemia, unawezaje kufundisha wakati huna maabara , vitabu vya kiada wala ziada.

Kumekuwa na matatizo mengi sana kwenye mfumo wetu wa elimu, wanasiasa wameanza kutuaminisha kuwa shule ni majengo na si taasisi. Matokeo yake, tunaendelea kuwa na majengo na wanafunzi bila kuwa na uwiano wa wanafunzi wa mwalimu. Wakati darasa la Mirian lina wanafunzi 35 maximum, kuna shule (Kawe ukwamani) mkondo mmoja una wanafunzi 150 na darasa wanafunzi 600 wakisoma kwa session ya asubuhi na mchana, Kuna mwalimu hata mwenye bidii kiasi gani anaweza kufuatilia maendeleo ya mtoto mmoja mmoja? Lakini lazima uwepo mfumo wa kuwaangalia walimu ( wakaguzi wa elimu), siku hizi sijui hata kama wakaguzi wapo, na kama wapo wanafanya kazi yao sawasawa. Sasa haya ni matatizo yanayozipata sehemu kubwa ya shule zetu za serikali, kinyume chake shule kama Marian, ina waalimu ( ambao uongozi unahakikisha wanafanya kazi yao sawasawa), kuna vitabu, maabara na wanafunzi wana shughuli moja tu, kusoma. Wana test za mara kwa mara kupima wanafunzi, kwanini wasifaulu vizuri wakipewa mitihani.

Mimi siamini kuwa Marian ina magenius, bali mazingira mazuri ya kusoma kitaasisi (walimu, vitabu, maabara, uongozi, chakula na malazi) unachangia sana wao kufanya vizuri katika masomo yao.

Kuhusu suala la makabila na dini za wanafunzi wanaochanguliwa kuingia shule hiyo, naona inachangiwa zaidi na background za hao watoto. Kuna ukweli kuwa makabila fulani wao elimu ilianza kutiliwa maanani zamani kidogo, na kwa mtazamo wangu ilikuwa kosa kuwapa upendeleo wanafunzi kutoka mikoa iliyokuwa nyumba kieimul kuingia sekondari hata kwa maksi za chini, kama uamuzi ule ulikuwa urudiwe ingekuwa kutengenza shule nzuri huko huko na kuwaandaa wanafunzi wataopata viwango vya ufaulu vinayvotakiwa kuliko kuwabeba.

Umesema kweli. Mimi nilisoma Maua 1982-1988 - tulikuwa tunachukua masomo 12 na kila somo kila mwanafunzi alikuwa na vitabu vyake muhimu na maabala ilikuwa well equipped. Ratiba yetu ilikuwa mwisho wa masomo usiku saa 9, kisha manual work, michezo na mwisho wa kujisomosea saa 4 usiku na asubuhi kama mtu anataka kuamka ni kuanzia saa 12. Pamoja na hayo, tulihimizwa sana kufanya kazi (manual work), michezo na social events kama English debate na shule zingine mkoani Kilimanjaro + kila mwaka wanafunzi wa Kidato wa IV walikuwa na study tours kutembelea mashamba ya ngano, mifugo kule West Kilimanjaro maana shule yetu ilkuwa inachukua mchepuo wa Kilimo (Kilimo + mifugo).

Tuliweza pia kutembelea kila mwaka bandari ya Mombasa kujifunza jinsi meli zinavyotua, kupakia mizigo nk na Kiwanda cha Korosho Bamburi na pia kujifunza kuhusu 'land reclamation'. Hapo Bamburi zamani ilikuwa nusu jangwa lakini mwekezaji mmoja aliweza kubadilisha na kuifanya fertile land kwa kuweka majongoo aliyoyakuwa akiyakusanya kutoka visiwa vya Bahari ya Hindi na yalipooza yalitengeneza udongo na kuanza kuotesha mimea na kufuga wanyama mbalimbali. Mambo mengine tuliyoyafanya nje ya masomo ni kujifunza music [kusoma notes, kucheza flute, kinanda, gitar, piano, kodiani (sijui nimepatia spellling), kupiga ngoma, kuigiza], kutengeneza matofali, ku'service machine' mfano trekta etc, kufuga nyuki, kufanya survey (kama wanavyofanya wapima barabara), grafting, sauna bath, kuogelea etc.

Hivyo, mtu akimaliza Maua alikuwa na elimu karibu ya kila kitu na kila kitu mwanafunzi anajifunza kwa kuona mfano kwa somo la geografia kuhusu erosion inayosababishwa na mto tulikuwa tunaenda kwenye mto kuona inafanyika namna gani. Pia tulikuwa tunatembelea bwawa la Nyumba ya Mungu, Crater Lake (Ziwa Jipe) na kupanda mlima Kilimanjaro maana Maua ilikuwa inatoa huduma kwa wale wanaopanda mlima Kilimanjaro kama huduma ya nguo za baridi, groves na viatu vyake. Ila ukitoka kwenye mazingira kama haya uende sehemu ambayo inabidi uibie mitihani, umhonge mwalimu, kupata maksi mpaka ujikombe kwa mwalimu wa somo nk, of course, utafeli tena sana!

Msingi huu umefanya elimu ya kilimo, utunzaji wa mazingira, ujenzi, carpentry, ufugaji nk ibaki kwenye damu yangu hadi leo.
 
mie nilisoma nao nairobi primary kufika secondary maisha yakaisha nkarud shule za uswahilin wenyewe wakienda hayo mashule mara fedha boys, marian na nyingine nimemaliza chuo kila niliesoma Nae primary akaenda hizo shule hajamaliza. Ni wachache sana waliomaliza. Mie nawashaur wazaz waskurupuke na hiz shule kule n luxury 2 na kuvuka form 6, lakin maisha hawawez unakuta et mtu kazaliwa dar mpaka anafika chuo hajawah fika hamjui hata jiran yake, ndo wakienda chuo wanachanyikiwa na maisha. Wanakutana na watu ambao wamesomea st. Kayumba kwao kutoroka n jad na kufaulu lazima, club ndo home, pombe ful mzuka, kenyewe unakuta hata kunywaa hakajawah Ila kwa sabab wanajifanyaga wenyewe wanajua wanaangukia pua, break ya kwanza apata boyfriend au girlfriend tapeli, Ile ndo yamekolea final hiyo, wanadharau kusoma SI wameingia chuo na 1. Wanajiona vichwa, na watoto wa uswaz kwa kupiga vibut wakat wa final ni balaa wataacha kudisco hapo.(kumbuka mtoto wa hizi shule mfano wa st. Francis hawajui kuweka mpenz wa ziada wakati wa maana)

Hawa watoto wa kishua wanaosoma katika shule hizi, mwisho wao wa kuwakilisha unaishiaga katika Vyuo Vikuu. Tulianza nao pale Muhimbili, wengi waliliwa vichwa katika Semister ya kwanza tu, na wengine wengi walikimbilia mzumbe! tukabaki sisi watoto wa uswazi tuliotokea Kibaha, Mzumbe, Ilboru na Pugu boyz. Ni mbwembwe tu! whatzup nyingi!
 
Sio wote kuna wengine ni vipanga kwelikweli hadi chuo...sitamsahau dada mmoja alisoma A-level Marian PCM alitukimbiza balaa hadi tunamaliza chuo..na ndie aliyeongoza mwaka huo kwa G.P.A kubwa pale udsm...my point is kuna wengine kweli ni dhaifu sana ila wengi wao wanajitahidi sana...sio wao tu mbona hata wale vipanga wa Mzumbe,Ilboru,Tabora boys n.k wakifika chuo wanapotea vibaya..ni akili ya mtu na juhudi binafsi..Chuo ni tifauti sana na secondary..

hv ratio zpo sawa???? wanaoingia chuo na kufeli kutoka vipaji na saint.....
 
Back
Top Bottom