Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani
Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.
Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.
Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.
Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.
Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?
Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.
Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.
Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Nawasilisha.
Mwanajukwaa acha uongo wa kichawa
Ukweli ni kwamba Christopher Bageni alitiwa hatiani kwa sababu ndio alikuwa ni kiongozi wa kikosi kilichotumwa na Abdallaha Zombe kuwakabili wafanyabiashara wa madini watatu kutoka huko Ifakara au Ulanga hivyo alikuwa na wajibu wa kujua kilichotokea au kuzuia mauaji hayo.
Askari aliyefyatua risasi hakukamatwa na kushtakiwa mpaka leo.
Kumbukumbu hii hapa:
Uchambuzi wa hoja (Facts Analysis)
Scenario 1
Walioshitakiwa walikuwa 13, SP Christopher Bageni, ACP Abdallah Zombe, ASP Ahmed Makele, PC Noel Leornard, WP 4593 Jane Andrew, CPL Nyangerela Moris, PC Michael Shonza, CPL Abeneth Saro, DC Rashid Mahmoud Lema, CPL Emmanuel Mabura, CPL Felix Sandys Cedrick, CPL Rajab Hamis Bakari na CPL Festus Philipo Gwabisabi.
Kwanini wameshitakiwa watu wote hawa halafu mtu mmoja ndiye aliyepatikana na hatia na akahukumiwa kunyongwa?
Kwa kumbukumbu, kesi hii ilianzia Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Salum A. Massati Jaji Kiongozi. Wakati upande wa mashitaka ukifunga kesi yao mahakama ikawaondoa watuhumiwa watatu PC Noel Leornard, CPL Nyangerela Moris na CPL Felix Sandys Cedrick kwa kuwaona hawana kesi ya kujibu, hivyo ikaona hakuna haja ya kuwataka kujitetea na kuendelea kuwa katika kesi.
Kwa hiyo wakabaki 10 ambao sasa walikutwa na kesi ya kujibu, hivyo kesi ikaendelea na hao 10 akiwamo Bageni. Wakati wameanza kujitetea, mmoja wao hao 10,
DC Rashid Mahmoud Lema alifariki dunia, hivyo kesi yake ikaishia hapo na sasa idadi ikabaki tisa.
Mwisho wa kesi hapo Mahakama Kuu, Jaji Massati aliwaachilia huru watuhumiwa wote tisa waliokuwa wamebaki kwa kuwaona hawana hatia. Moja ya hoja kubwa ya kuachiliwa kwao huru ilikuwa kwamba kati ya wote hao tisa waliobaki katika kesi hiyo hakuna hata mmoja
kati yao aliyefyatua risasi na kuua.
Ikumbukwe
aliyefyatua risasi na kuua ni CPL Saad ambaye hakuwahi kukamatwa na kufikishwa mahakamani baada ya kutoroka mapema ‘liliposanuka’. Kwa hiyo Mahakama Kuu iliona kutokuwepo kwa CPL Saad ili atiwe hatiani kwa kuua au amtaje mtu mwingine aliyempa amri ya kuua ili wote wahukumiwe kwa kosa moja, iliona ni udhaifu ambao unatosha kuwaachilia watuhumiwa wote tisa, na iliwaachilia wote huru. Kwa ufupi iliona hakuna kinachowaunganisha na mauaji zaidi ya tu kuwa walikuwa kwenye tukio.
Kumbuka Mahakama Kuu ilimuachilia Bageni kwa sababu kuu mbili. Kwanza, siye aliyefyatua risasi; pili, yule aliyefyatua risasi CPL Saad hakufika mahakamani kumtaja Bageni kuwa ndiye aliyemuamrisha kupiga risasi ili wote wawe na hatia sawa.
Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Kifungu cha 22 cha Kanuni za Adhabu aliyetenda kosa kama vile CPL Saad alivyopiga risasi (
kutenda-Actus reus/guilty act & Mens rea/guilty mind-the act of physically committing a crime), na aliyeamrisha (
kusaidia-aid to commit offence) kutendwa kosa, wote hatia yao ni moja. Kama ni kunyongwa ni wote na kama ni kifungo ni wote.
Kwa msingi huu, Mahakama Kuu haikumuona Bageni akifyatua risasi kwa sababu si yeye aliyefyatua risasi, hivyo upande huo akaondolewa, lakini pia haikumuona akiamrisha risasi kufyatuliwa, kwa sababu aliyefyatua hakuwapo mahakamani kumtaja kuwa ndiye aliyemwamrisha kufyatua, hivyo upande huo pia nako akaondolewa. Mwisho akaonekana haingii popote kwenye kosa, basi akaachiliwa huru.
Types of mens rea/guilty mind
1.
Purposely - the person wants the outcome and acts in such a way to try and create the desired outcome
2.
Knowingly - the person is aware that what they do will likely cause the desired outcome, or that the outcome is not allowed
3.
Recklessly - the person is aware that their behavior is such of "a substantial and unjustifiable risk" that the outcome is not allowed
4.
Negligently - a "reasonable person" would have been or should have been aware that their behavior would have led to an outcome that was not allowed
Aina za akili yenye hatia/uovu
1.
Kwa makusudi - mtu anataka matokeo na vitendo kwa njia ya kujaribu na kuunda matokeo yaliyohitajika
2.
Kwa kujua - mtu anajua kwamba kile wanachofanya kitasababisha matokeo yaliyotakiwa, au kwamba matokeo hayaruhusiwi
3.
Bila kujali - mtu anajua kuwa tabia yake ni kama "hatari kubwa na isiyo ya haki" kwamba matokeo hayaruhusiwi
4.
Kwa uzembe - "mtu mwenye busara" angekuwa au angepaswa kujua kwamba tabia zao zingesababisha matokeo ambayo hayakuruhusiwa
Scenario 2

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ilala Christopher Bageni amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kutengua hukumu iliyomwachia huru na kumtia hatiani kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja.
Kadhalika mahakama hiyo imewaachia huru Mkuu wa Upelelezi wa zamani (wakati huo Mkoa wa Dar es Salaam) (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi mstaafu Abdallah Zombe na wenzake wawili baada ya ushahidi wa rufaa hiyo kushindwa kuwatia hatiani.
Mara baada ya hukumu kusomwa, ghafla Bageni aliduwaa wakati wenzake wakimkumbatia huku wakibubujikwa na machozi wakiwa kizimbani.

Wanaodaiwa kuwa wanafamilia wa washtakiwa hao waliangua vilio huku washtakiwa wenzake walisikika wakieleza masikitiko yao. Wengine walisikika wakisema angejua asingekuja mahakamani kusikiliza hukumu hiyo.
“Namshukuru Mungu...Lakini nasikitika kwa Bageni kukutwa na hatia sina raha kabisa....” alisema ASP Makele wakati akitoka katika ukumbi namba moja wa mahakama hiyo.

Hukumu hiyo imesomwa leo na Msajili wa mahakama hiyo Mhe. John Kahyoza baada ya rufani iliyokatwa na upande wa Jamhuri kusikilizwa na jopo la majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Jaji Bernard Luanda, Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage.
Msajili alisema awali Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Jaji Salum Massati (wakati huo kabla ya kupanda kuwa jaji wa rufani), ilimuona Zombe na wenzake hawana hatia na kwamba haiwezi kuwahukumu kwa kosa la kusaidia kufanyika mauaji hayo.
SSP-Christopher Bageni
Alisema Mahakama ya Rufani inakubaliana na Jaji Massati kwamba mtuhumiwa hawezi kutiwa hatiani bila kuthibitisha mtu aliyetenda kosa hajashtakiwa na kutiwa hatiani...."