Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

.... Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?
Unasema mahakama ilitumia busara, halafu unasema kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Basi kama mtumaji hana kosa kisheria, hiyo sio busara, ni sheria kamili kwamba hana hatia. Vinginevyo utakuwa unajichanganya
 
Kwa mifano hiyo hiyo iliyotolewa, yule Padri aliyefadhili mauaji ya mtoto mwenye ualbino kule Kagera naye aachiwe. Kwa mujibu wa maelezo yako mleta mada, Padre naye hana kesi ya kujibu na kwakuwa amedhalilishwa, Jamhuri inapaswa kumwomba radhi.
Tuvute subira mahakama ifanye uamuzi wake mkuu. Inawezekana padre alihusika kuua.
 
Hili ndo nilikuwa nasema watu wanataka watu wapandishwe kizimbani kwa mihemko tu hawajui mahakamani ni ushahidi usio shaka ndo unasimama, kwa hiii kesi kumkuta na hatia huyu mama ni kazi sana maana inabidi ueleze kinaga ubaga chain yake na hao watu na uthibitishe kuwa yeye aliwatuma jambo ambalo si rahisi. Hii dunia ya mitando ni ngumu sana kwenda nayo maana kila mtu ni mtaalam na hisia ni bora zaidi kuliko ukweli
kuna kitu kinaitwa kuunda genge la kihalifu hicho kingemuunganisha na kosa ni kula njama.Unaonaje?
 
Nimeona kwenye mtandao wa x kuna wakili kafungua shitaka kumuhusu huyo Askari
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani

Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.

Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.

Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.

Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.

Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?

Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.

Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.

Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha.
Kwa ufafanuzi huu, wewe siyo layman wa sheria kama kina sisi, wewe ni mwanasheria.

Kumbu kumbu za kesi za mfano ulizoambatanisha zina majibu ya mustakabali kamili wa kesi hii.

Hivyo ulivyotunasihi raia tuache ama tupunguze munkari wa kushadadia 'mtumaji' afikishwe kwa Pontio Pilato ni ushauri wenye busara na wa kisomi.

Lakini kupunguza maumivu ya mwathiriwa, inafaa sana 'mtumaji' aburutwe tu mahakamani akashindie huko na si kumwacha tu huru akizurula huku kesi ikiunguruma.

Kanuni kwa mfanyakazi wa umma anapotuhumiwa na kashifa na kesi nzito ama yenye public interest husimamishwa kazi hadi hapo atakapojisafisha.

Ninazijua athari za kusimamishwa kazi na kuburutwa mahakamani zinavyong'onyeza mtuhumiwa.

Kwanza ataanza kupokea nusu mshahara, Kama alikuwa si wa kwenda kanisani, sasa atakwenda, kama alikuwa si wa kwenda kwa waganga wa kienyeji, sasa atakwenda, nafasi ya kiofisi aliyokuwa nayo sasa itachukuliwa na mtu mwingine.

Itoshe kusema kuwa, kumburuta mahakamani mtumishi wa umma bila hata hukumu ni adhabu tosha sana kwake na humfanya ajute hata kama atashinda.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani

Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.

Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.

Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.

Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.

Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?

Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.

Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.

Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha.
Mwanajukwaa acha uongo wa kichawa

Ukweli ni kwamba Christopher Bageni alitiwa hatiani kwa sababu ndio alikuwa ni kiongozi wa kikosi kilichotumwa na Abdallaha Zombe kuwakabili wafanyabiashara wa madini watatu kutoka huko Ifakara au Ulanga hivyo alikuwa na wajibu wa kujua kilichotokea au kuzuia mauaji hayo.

Askari aliyefyatua risasi hakukamatwa na kushtakiwa mpaka leo.
Kumbukumbu hii hapa:
Uchambuzi wa hoja (Facts Analysis)
Scenario 1

Walioshitakiwa walikuwa 13, SP Christopher Bageni, ACP Abdallah Zombe, ASP Ahmed Makele, PC Noel Leornard, WP 4593 Jane Andrew, CPL Nyangerela Moris, PC Michael Shonza, CPL Abeneth Saro, DC Rashid Mahmoud Lema, CPL Emmanuel Mabura, CPL Felix Sandys Cedrick, CPL Rajab Hamis Bakari na CPL Festus Philipo Gwabisabi.

Kwanini wameshitakiwa watu wote hawa halafu mtu mmoja ndiye aliyepatikana na hatia na akahukumiwa kunyongwa?

Kwa kumbukumbu, kesi hii ilianzia Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Salum A. Massati Jaji Kiongozi. Wakati upande wa mashitaka ukifunga kesi yao mahakama ikawaondoa watuhumiwa watatu PC Noel Leornard, CPL Nyangerela Moris na CPL Felix Sandys Cedrick kwa kuwaona hawana kesi ya kujibu, hivyo ikaona hakuna haja ya kuwataka kujitetea na kuendelea kuwa katika kesi.

Kwa hiyo wakabaki 10 ambao sasa walikutwa na kesi ya kujibu, hivyo kesi ikaendelea na hao 10 akiwamo Bageni. Wakati wameanza kujitetea, mmoja wao hao 10, DC Rashid Mahmoud Lema alifariki dunia, hivyo kesi yake ikaishia hapo na sasa idadi ikabaki tisa.

Mwisho wa kesi hapo Mahakama Kuu, Jaji Massati aliwaachilia huru watuhumiwa wote tisa waliokuwa wamebaki kwa kuwaona hawana hatia. Moja ya hoja kubwa ya kuachiliwa kwao huru ilikuwa kwamba kati ya wote hao tisa waliobaki katika kesi hiyo hakuna hata mmoja kati yao aliyefyatua risasi na kuua.

Ikumbukwe aliyefyatua risasi na kuua ni CPL Saad ambaye hakuwahi kukamatwa na kufikishwa mahakamani baada ya kutoroka mapema ‘liliposanuka’. Kwa hiyo Mahakama Kuu iliona kutokuwepo kwa CPL Saad ili atiwe hatiani kwa kuua au amtaje mtu mwingine aliyempa amri ya kuua ili wote wahukumiwe kwa kosa moja, iliona ni udhaifu ambao unatosha kuwaachilia watuhumiwa wote tisa, na iliwaachilia wote huru. Kwa ufupi iliona hakuna kinachowaunganisha na mauaji zaidi ya tu kuwa walikuwa kwenye tukio.
Kumbuka Mahakama Kuu ilimuachilia Bageni kwa sababu kuu mbili. Kwanza, siye aliyefyatua risasi; pili, yule aliyefyatua risasi CPL Saad hakufika mahakamani kumtaja Bageni kuwa ndiye aliyemuamrisha kupiga risasi ili wote wawe na hatia sawa.

Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Kifungu cha 22 cha Kanuni za Adhabu aliyetenda kosa kama vile CPL Saad alivyopiga risasi (kutenda-Actus reus/guilty act & Mens rea/guilty mind-the act of physically committing a crime), na aliyeamrisha (kusaidia-aid to commit offence) kutendwa kosa, wote hatia yao ni moja. Kama ni kunyongwa ni wote na kama ni kifungo ni wote.

Kwa msingi huu, Mahakama Kuu haikumuona Bageni akifyatua risasi kwa sababu si yeye aliyefyatua risasi, hivyo upande huo akaondolewa, lakini pia haikumuona akiamrisha risasi kufyatuliwa, kwa sababu aliyefyatua hakuwapo mahakamani kumtaja kuwa ndiye aliyemwamrisha kufyatua, hivyo upande huo pia nako akaondolewa. Mwisho akaonekana haingii popote kwenye kosa, basi akaachiliwa huru.

Types of mens rea/guilty mind​

1. Purposely - the person wants the outcome and acts in such a way to try and create the desired outcome
2. Knowingly - the person is aware that what they do will likely cause the desired outcome, or that the outcome is not allowed
3. Recklessly - the person is aware that their behavior is such of "a substantial and unjustifiable risk" that the outcome is not allowed
4. Negligently - a "reasonable person" would have been or should have been aware that their behavior would have led to an outcome that was not allowed

Aina za akili yenye hatia/uovu

1. Kwa makusudi - mtu anataka matokeo na vitendo kwa njia ya kujaribu na kuunda matokeo yaliyohitajika
2. Kwa kujua - mtu anajua kwamba kile wanachofanya kitasababisha matokeo yaliyotakiwa, au kwamba matokeo hayaruhusiwi
3. Bila kujali - mtu anajua kuwa tabia yake ni kama "hatari kubwa na isiyo ya haki" kwamba matokeo hayaruhusiwi
4. Kwa uzembe - "mtu mwenye busara" angekuwa au angepaswa kujua kwamba tabia zao zingesababisha matokeo ambayo hayakuruhusiwa

Scenario 2

"..Kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja: Christopher Bageni ahukumiwa kunyongwa hadi kufa, zombe na wenzie wawili waachiwa huru

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ilala Christopher Bageni amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kutengua hukumu iliyomwachia huru na kumtia hatiani kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja.

Kadhalika mahakama hiyo imewaachia huru Mkuu wa Upelelezi wa zamani (wakati huo Mkoa wa Dar es Salaam) (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi mstaafu Abdallah Zombe na wenzake wawili baada ya ushahidi wa rufaa hiyo kushindwa kuwatia hatiani.
Mara baada ya hukumu kusomwa, ghafla Bageni aliduwaa wakati wenzake wakimkumbatia huku wakibubujikwa na machozi wakiwa kizimbani.

Wanaodaiwa kuwa wanafamilia wa washtakiwa hao waliangua vilio huku washtakiwa wenzake walisikika wakieleza masikitiko yao. Wengine walisikika wakisema angejua asingekuja mahakamani kusikiliza hukumu hiyo.
“Namshukuru Mungu...Lakini nasikitika kwa Bageni kukutwa na hatia sina raha kabisa....” alisema ASP Makele wakati akitoka katika ukumbi namba moja wa mahakama hiyo.

Hukumu hiyo imesomwa leo na Msajili wa mahakama hiyo Mhe. John Kahyoza baada ya rufani iliyokatwa na upande wa Jamhuri kusikilizwa na jopo la majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Jaji Bernard Luanda, Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage.

Msajili alisema awali Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Jaji Salum Massati (wakati huo kabla ya kupanda kuwa jaji wa rufani), ilimuona Zombe na wenzake hawana hatia na kwamba haiwezi kuwahukumu kwa kosa la kusaidia kufanyika mauaji hayo.
1724162919515.png

SSP-Christopher Bageni
Alisema Mahakama ya Rufani inakubaliana na Jaji Massati kwamba mtuhumiwa hawezi kutiwa hatiani bila kuthibitisha mtu aliyetenda kosa hajashtakiwa na kutiwa hatiani...."
 
Lakini sheria zetu zinawalinda watu wanaowatuma watu kwenda kutenda uhalifu ila zinamkaanga aliyetenda uhalifu personally. Unadhani nini kifanyike kuweka hili uambo sawa?
KOSA LA KUFANYA NJAMA
Kwa Mujibu wa Sheria ya Adhabu namba 384
✅Hili ni kosa la jinai ambalo hufanyika na watu wawili au zaidi wakiwa na nia ovu kushirikiana kupanga, na kutenda uhalifu pamoja.
✅Mtu yeyote ambaye anakula njama na mtu mwingine katika kutenda kosa lolote, ambalo linaadhibiwa kwa kifungo cha kipindi cha miaka mitatu au zaidi, au kutenda kitendo chochote katika sehemu yoyote ya dunia ambalo kama limetendeka Tanzania lingekuwa ni kosa ambalo linaadhibiwa, na ambalo ni kosa chini ya sheria zinazotumika katika sehemu ambayo limefanyika, atakuwa anatenda kosa, na atawajibika, kama hakuna adhabu nyingine iliyotolewa, kwa adhabu ya kifungo cha miaka saba au,
✅iwapo adhabu kubwa kabisa ambapo mtu huyo amehukumiwa kwa kosa husika ni ndogo kuliko kifungo cha miaka saba, basi kwa adhabu hiyo ndogo kuliko. Kama ilivyo elezwa na Kanuni ya Adhabu 384
✅Hata hivyo Mtu yeyote ambaye anakula njama na mtu mwingine katika kutenda kosa ambalo linaadhibiwa kwa kifungo cha kipindi kisichopungua miaka mitatu, au kufanya kitendo chochote katika sehemu yoyote ya dunia ambalo kama limetendeka Tanzania lingekuwa ni kosa ambalo linaadhibiwa, na ambalo ni kosa chini ya Sheria zinazotumika katika sehemu ambayo imependekezwa kufanyika, atakuwa anatenda kosa. Kanuni ya Adhabu 385
JE MKE NA MUME WANAWEZA KUFANYA NJAMA
✅Jibu ni ndio mtu yeyote ambaye anakula njama na mtu mwingine ili kutimiza lolote katika madhumuni haya yafuatayo, ndio kusema wanaweza kuzuia au kupinga utimilizaji au utumikaji wa Sheria yoyote;
1.kusababisha dhara lolote kwa mtu au sifa ya mtu yeyote au
2.kushusha thamani ya mali yoyote ya mtu yoyote;
kuzuia au kukinga uuzaji huru na wa halali wa mali yoyote ya mmiliki ili kupata thamani inayostahili kwa mali hiyo;
3.kumdhuru mtu yeyote katika biashara au taaluma yake; au kuzuia au kukinga, kwa njia yeyote tendo lolote au matendo yeyote ambayo kama yatafanywa na mtu yatasababisha kosa kwa upande wake,uendeshaji huru na wa halali wa mtu katika biashara, taaluma au nafasi yake ya kazi; kutimiza madhumuni yoyote yasiyokuwa halali; ni kosa la jinai.
 
Usisahau kwenye hii kesi binti yumo ndani yake, vip km akaonyesha ushirikiano kwa kumtaja huyo mme wa mtu ambaye mkewe ndiye aliyepelekea yeye kutekwa kufanyiwa unyama ili aachane nae bado huoni kama mpangaji wa hilitukio anakesi ya kujibu NB: sijui sheria nimejaribu kuwaza tu
 
Mkuu naomba ieleweke kwamba sio mm ninayetetea hili jambo bali lipo kwa mujibu wa sheria za nchi. Labda cha msingi ungemuomba mbunge wako apeleke muswada wa mabadiliko bungeni ili kipengele hiki cha sheria kirekebishwe.
Sheria ipi?

Kama ni sheria na ni kinyume cha Katiba haina maana

Sheria ni kitu kimoja na ku enforce sheria ni kitu kingine

Tunga sheria sana,ila kufanya wananchi waifate ni another issue...Kama wananchi hawataki,no matter what sheria u write!Keep them for yourself na CCM yako
 
Hili ndo nilikuwa nasema watu wanataka watu wapandishwe kizimbani kwa mihemko tu hawajui mahakamani ni ushahidi usio shaka ndo unasimama, kwa hiii kesi kumkuta na hatia huyu mama ni kazi sana maana inabidi ueleze kinaga ubaga chain yake na hao watu na uthibitishe kuwa yeye aliwatuma jambo ambalo si rahisi. Hii dunia ya mitando ni ngumu sana kwenda nayo maana kila mtu ni mtaalam na hisia ni bora zaidi kuliko ukweli
•PLOTTING AND SCHEMING TO
•CONSPIRACY TO

Ingekuwa ni karne ya 20 kushuka chini, basi ni kweli "kumkuta na hatia" kama usemavyo ingekuwa "kazi sana" haswa kwa technology ya nchi yetu. Ila hii ni karne ya 21 mkuu, labda kama mawasiliano hayakufanyika kwa simu wala kifaa chochote cha aina hiyo. Japo pia uwepo wa mashahidi watano sio kitu kinaweza kupuuziwa kwa urahisi mahakamani.
 
Upo sahihi kwa marejeo yako ya kesi.
Lakini polisi wafanye sehemu yake (kuwakamata wahusika).
Then mahakama nayo itafanya ya kimahakama!
Huyo afande kazi yake ni kuhakisha uharamia hautokei.
Sasa yeye kama kahusika na kutoa amri kufanyika uharamia, hata kama ata toka lakini hafai kuwa polisi tena ni kufukuzwa kazi.

Kwa hivyo afikishwe mahakamani.
 
Mimi siizungumzii hii kesi ila nazungumzia hoja yako ya kesi ya kwanza, aidha unadanganya au huijui hiyo kesi vizuri na sababu za kuachiwa wake askari wengine na kuhukumiwa Bageni .

Ukweli ni huu kwanza uelewe katika majeshi yote duniani ukipewa order na mkubwa wako lazima uitekeleze hata kama amri hiyo haina busara, ukigoma kutekeleza ni usaliti na adhabu yake ni kuuliwa. Hii ni tofauti na uraiani ambako unaweza kukataa anri ya mkubwa wako na ukawa sakama kikazi.

Zombe kilichomsaidia akachomoka wakati ndiye aliyetia amri ni kuwa kwanza alikataa kuwa hakutoa order wale wafanyabiashara wauawe pili hakuwepo eneo la tukio. yule askari akiyefyatua risasi kuwaua wale wafanyabiashara wa madini alisaidiwa akatoroka hivyo shahidi muhimu hakuwepo mahakamani. Pili yule askari akiyechukua miili ya wale marehemu na kuipeleka hospitali mochwari alikufa kifo cha kuugua mahtuti akalazwa hospitali na kufia huko hivyo naye kama shahidi muhimu akawa hayupo. Askari wengine wadogo wakiachiwa kwa sababu hawakutajwa kufyatua risasi licha ya order kutolewa ya kuwaua wale wafanyabiashara japo hata kama wangetajwa wasingetiwa hatiani. Bageni kilichomtia hatiani ni kuwa yeye ndiye alikuwa kiongozi wa operesheni wadhifa wake alikuwa afisa upelekezi wa wilaya na ndiye aliyepokea amri kutoka kwa Zombe na yeye ilithibitika ndiye aliyetoa order kwa askari wa chini kuua wale marehemu. Kumbuka Zombe aliruka kutoa order wafanyabiashara wauawe hivyo msala ukamuangukia mkuu wa operesheni site ( Bageni), kama ingethibitika Zombe ndiye aliyetoa order Bageni asingetiwa hatiani hata kama ingethibitika ndiye aliyewaagiza askari wa chini kuua kwa sababu kijeshi aliyetoa order ndiye mwenye hatia sio mtekekezaji.

Ni vizuri jambo usilolijua usilisemee
Mku7 naona bado unarudi palepale. Kwani sheria za nchi zinabagua kati ya askari na raia?
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani

Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.

Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.

Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.

Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.

Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?

Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.

Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.

Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha.
Tayari ameshakamatwa acha porojo
Ni ASP.
Yupo ananywea kikombe huko
 
Mimi ningependa huyo afande naye aunganishwe kwenye kesi hii kama kuchomoka akachomokee Mahakamani, sababu yangu kubwa ni kutaka umma umfahamamu kuwa ni yeye aliyefadhili uharamia uliofanyika ili iwe pia ni fundisho kwake.
Kama hakuwatuma je? Waliamua kumfurahisha baada ya kupata fununu kuwa binti anatembea na mme wake? Mimi siyo mwana sheria ila hapo inaonekana ngumu kumtia hatiani
Hakuna ushahidi wa kutosha hapo mfano ...maongezi yao yalikuwa wapi , nani shahidi? Transactions je?
In short hao wamejimaliza wao wenyewe
 
Huyo aliyewatuma akishawakataa hawa vibaka, mbona yeye anang'oka ktk hiyo case! Hakuna ushahidi wa wazi kuhusu yeye kuhusika.

Muhimu hawa vibaka wakanyee ndoo huko lupango basi.
Afu naomba kujuzwa ni kweli hawa vibaka ni wajedaa?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndio maana nimepiga marufuku watoto wangu kusomea sheria au kuwa polisi. Na Mungu mkubwa wote wanajua sana hesabu.
 
Back
Top Bottom