JAYJAY
JF-Expert Member
- Oct 31, 2008
- 8,191
- 8,490
Ukijiongeza wewe inatosha.Jiongeze sio kila kitu utaambiwa au kitaandikwa usome
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukijiongeza wewe inatosha.Jiongeze sio kila kitu utaambiwa au kitaandikwa usome
Yes nakumbuka alitiwa hatiani Bageni, ila Zombe yeye atakuwa anakula maisha tu.Koplo Sadi ndiye aliyewapiga Risasi ila kiongozi mtoa amri alikuwa Bageni ambaye kachezea maisha.
Inasikitisha sana, hawa askari wenye vyeo vya chini huwa wanaingia kwenye trap kwa kupokea order tu. Mwisho wa siku mambo yakibuma wanabaki wenyewe, vigogo wanapeta.Zzombie anakula bata mtaani na alichukua mafao yake kabisa. Tabia ya kutenda mambo kwa mkumbo au mhemko haijawahi kumuacha mtu salama.
Kama wasipomtaja inakuwaje au na binti nae asipomtaja??Mkuu ikiwa watuhumiwa watakana kutumwa na afande kwa kuwa aliwapa hela na kwa kuwa waliinjoi uloda, binti aliyefirwa na hao mabedui lazima atamtaja tu. Hakuna namna anvyoweza kuponyoka kutajwa isipokuwa akifikishwa mahakani ndipo atakapochomokea baada ya kushinda kesi.
Ungeweka hizo reference za hukumu ili tujiridhishe mkuu...Kama unadhani ni maoni yangu unakosea sana mkuu. Hizo references nimezitoa kwenye hukumu za mahakama za hapa nchini na zilizohukumiwa kwa kutumia sheria za nchi hii. Kama huamini hata matukio ya kweli, basi hilo ni tatizo lako binafsi mkuu.
Ila mkuu kumbuka huwezi mpeleka mtu mahakaman kwa hisia au fununu tu hata kama atatokea mahakamanHata binti asipomtaja, Madereka atamburuza mahakamani tu. Ushahidi upo. Lakini hatimaye ataachiwa huru kwa mujibu wa sheria mkuu.
Wewe hujui sheria kabisa. Ingekuwa hivyo drug lords wasingefungwa. Kasome accomplice /accessory to crimes conceptsRejea kesi mbili nilizotaja hapo juu halafu uje hapa tena mkuu. Sheria za nchi ndivyo zinavyosema. Labda kama wewe unasheria zako, ziweke hapa tuzidadavue.
Sikeeli kukiwq nanushahidi wa wazi mfano mawasiliano yakupanga au kuagiza basi utakamatwaSheria za nchi hazitambui mtu kutumwa mkuu. Hata ukituma wahalifu kumuua mtu na wahalifu kutekeleza mauaji, wewe mtumaji huna hatia hata kidogo.
Duh!Waliamua kumtoa kafara ili kumlinda Zombe aliyekuwa injinia mkubwa kwenye hili jambo.
Uko sawa, ila tunakukimbusha kua habari za kua na hatia ama kutokua na hatia uthibitika mahakamani. Ivyo basi kwasasa akamatwe na kufikishwa mahakamani mpaka itakavyokua proved kua hana hatia, ila sio polisi kumaliza juu kwa juu bila utaratibu wa kisheria kufuatwa.Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani
Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.
Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.
Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.
Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.
Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?
Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.
Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.
Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Nawasilisha.
Mkuu, kumpeleka mahakamani mtu ambaye una uhakika kuwa atashinda kesi ni kuchezea muda na rasilimali za umma. Aa chwe tu aendelee kula bata hadi sheria itakapobadilishwa. Ni nani alikuwa anajua kuwa Zombe na mke wa Msuya wangechomoka mahakamani? Sheria za nchi zinawalinda wahalifu na kuwafunga wasiokuwa na hatia.Uko sawa, ila tunakukimbusha kua habari za kua na hatia ama kutokua na hatia uthibitika mahakamani. Ivyo basi kwasasa akamatwe na kufikishwa mahakamani mpaka itakavyokua proved kua hana hatia, ila sio polisi kumaliza juu kwa juu bila utaratibu wa kisheria kufuatwa.
Asante.
Nikikutuma ukafanye mapinduzi ya nchi au ukafanye mauaji ya kiongozi muhimu na yakatekelezwa na ikabainika nimekutuma kwa hiyo mimi sitachukuliwa hatua yeyoteNaingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani
Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.
Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.
Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.
Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.
Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?
Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.
Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.
Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Nawasilisha.
Kwa mujibu wa sheria aliyerusha risasi, mkuki, mshale au bomu ndiye mwenye kosa. Yule aliyemtuma yupo huru kisheria. Ukienda kumshtaki mtumaji atachomoa kesi misa ya kwanza tu.Nikikutuma ukafanye mapinduzi ya nchi au ukafanye mauaji ya kiongozi muhimu na yakatekelezwa na ikabainika nimekutuma kwa hiyo mimi sitachukuliwa hatua yeyote