SoC01 Sababu za partnership kufeli katika biashara na mbinu za kutumia ili kudumisha ushirika katika kufanya biashara

SoC01 Sababu za partnership kufeli katika biashara na mbinu za kutumia ili kudumisha ushirika katika kufanya biashara

Stories of Change - 2021 Competition

Inck

New Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
2
Reaction score
2
Habarini wanaJamiiForums

Ni imani yangu mko salama. Leo napenda kuangazia suala zima la collabo au partnership katika kutafuta mitaji. Kutokana na ugumu uliopo katika kupata mtaji wa kuanzishia biashara, hasahasa kwa wahitimu wa chuo, collabo baina ya watu wawili au zaidi inakuwa ni moja ya njia ambazo mtu anaweza kuzitumia ili kukusanya mtaji.

Kwanini partnership nyingi zinafeli?

Mbinu ya partnership ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo sambamba na uwepo wa mwanadamu lakini swali linabaki kwanini baadhi ya watu wanafanikiwa nayo na wengine hawafanikiwi?

Partnership inataka washirika (partners) ambao wana uelewa wa jinsi ya kuendesha partnership. Miradi mingi ya partnership inafeli kutokana na washirika kutokuwekeana bayana majukumu yao. Katika partnership nyingi, huwa kuna malalamiko ya kila mshirika kujihisi kuwa yeye ndio anatumika zaidi kuliko wengine. Malalamiko haya yanaweza kukomeshwa kwa kutengeana majukumu kwa kila mshirika, kwa mfano kama mradi ni ufugaji wa nguruwe basi majukumu kama ulishaji wa nguruwe, utafutaji wa masoko, ulinzi na mengineyo ni lazima yagawanywe kwa kila mshirika kwa usawa ili kusiwepo na lawama za kiuwajibikaji.

Je, unawezaje kupata partner aliye bora?

Kuna usemi usemao kwamba "wazo la mradi lapaswa litangulie kabla ya uteuzi wa partners". Dai hili ni kweli japo kinyune chake pia chaweza kuwa sawa pia kulingana na ubora wa washirika.

Partner bora ni yule anayeamini katika mipango ya muda mrefu, mvumilivu, muwajibikaji, na pia awe na uwezo wa kusimamia lengo kuu la mradi huku akitekeleza kwa ufanisi malengo mahususi ya mradi husika.

Je, unamtambuaje mtu huyo?

Katika maisha huwa tunapata nafasi ya kukutana na watu wa aina mbalimbali aidha katika mazingira ya kazi au hata katika mazingira ya kawaida. Watu hawa huwa na vipawa na tabia tofauti ambazo huwa tunaziona kwao. Tabia hizo hutuvutia na zingine hutukera. Kupitia watu hao sasa ndimo tunaweza kupata partners tunaowatafuta kwasababu tumeweza kuwajua katika kipindi ambacho walikuwa katika uhalisia wao na hivyo tabia hizo ndizo tabia zao hasa.

Katika kumtathmini partner unayemuhitaji, jikite katika katika uwezo na ubora wake na si katika madhaifu yake. Yawezekana mtu huyo ni kiwete lakini anao uwezo mkubwa wa kufikiri na kuja na mawazo mazuri katika kutatua matatizo mbalimbali ya mradi, basi mtu huyo anaweza kufaa zaidi.

Usichague partner kwasababu tu unaweza kumpelekesha. Katika partnership zenye mafanikio na zenye kudumu mpaka mwisho, huwa hakuna utiifu uliokithiri bali huwa na majadiliano na ubishani mzito katika kutafuta njia sahihi ya kufanya jambo fulani. Hii ni muhimu kwasababu kupitia ubishani huo ndimo hasa kila mshirika ataridhika na suluhisho litakalofikiwa.

Je, ni kwa namna gani migogoro ya partnership inapaswa kushughukikiwa?

Ikumbukwe kuwa kama ilivo katika kila jumuiya, migogoro huwa haikosekani, basi katika partnership tarajia uwepo wa migogoro ya hapa na pale. Katika partnership ni muhimu kupongezana katika jambo zuri lililofanywa na mmoja wa washirika na kukosoana vilevile. Migogoro inapaswa kushughulikiwa kwa partners wote kukaa pamoja na kujadili malalamiko yaliyopo na kutafuta usuluhishi kwa pamoja huku mapendekezo ya mlalamikaji yakizingatakiwa kwa kulinganisha na lengo kuu la mradi.

Je, nini cha kufanya endapo mshirika atataka kujitoa kwenye partnership?

Si vema kutoa sehemu ya rasilimali za mradi na kumpa mtu anayetaka kujitoa. Kwa kufanya hivo kutapelekea mradi kukosa nguvu ya kujiendesha na hatimaye kufa. Lazima partners wakumbuke kuuweka mradi mbele kabla ya mihemko yao. Ikiwa tarehe ya kuhitimisha mradi iko bayana basi mshirika anayetaka kujitoa, ataruhusiwa kujitoa ila atatakiwa kusubiri mpaka mwisho wa mradi ili apate sehemu yake.

Hitimisho

Partnership sahihi inasaidia sana katika kufukia madhaifu ambayo sisi kama binadamu tunayo. Yaweza kuwa wewe si mzuri katika mauzo yaani sales ila upo vizuri katika technicality labda katika upishi basi unapaswa kutafuta partner ambaye atakusaidia katika kufanya sales. Partner ni tofauti na mwajiriwa, mwajiriwa anafanya kazi ili alipwe ila partner anawajibika na mafanikio mazima ya mradi na anakuwa anamiliki sehemu ya mradi husika.

Makampuni makubwa duniani kama Apple, Google, HP, Facebook, McDonald naengineyo mengi yalianzishwa kupitia partnership kwahiyo partnership yaweza isiwe kuwa ni njia ya kutafutia mtaji bali ikawa ndio njia ya kutafutia hatma nzima ya maisha yako. Ahsante.​
 
Upvote 1
Back
Top Bottom