Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Tanzania, kwa historia yake, rasilimali zake (watu na mali) na amani yake ingekuwa moja ya nchi tano Afrika zinazoongoza. Lakini kiuhalisia, inashindwa mbali na vinchi kama Senegal, Cote d'Ivoire, Botswana, Ghana. Ingawaje tuna GDP kubwa kuliko nchi hizo.
Hakuna mchawi, isipokuwa tumeanza vibaya baada ya kupata uhuru, na hadi sasa baadhi ya makosa yaleyale tunaendelea nayo. Makosa makubwa:
1 - Kushabikia mno siasa kuliko uchumi
2 - Kupuuza elimu na rasilimali watu
3 - Kupuuza kilimo ambacho ndiyo mategemeo ya wengi
4 - Kutokuwa na viongozi wengi wenye upeo wa fikra na exposure (matokeo yake kiongozi mmoja anadiriki kudai kujua kila kitu, mungu mtu)
5 - Kutokuwa na dira, stability ya sera za uongozi (kila kiongozi anaanza upya)
6 - Kupuuza Kiingereza (hii watu hawataifahamu, lakini ni kweli nchi za Afrika ambazo raia wake wengi wanafahamu Kiingereza,
Kifaransa, Kireno, Kijerumani, Kispaniola, Kiarabu, huwa akili zao, taste zao zimeendelea zaidi kwa vile wana nchi za kuiga zilizoendelea kuliko wao.
Hii ni kwa sababu raia hao ni rahisi ku 'incoporate' fikra mpya kama zile zilizoko kwenye nchi hizo zilizoendelea. Katika nchi za Afrika zilizoendelea sana katika kukumbatia fikra mpya: Social media, capital ventures, masoko ya hisa, Bitcoin na innovations za aina mbali mbali ni zile zenye uelewa mkubwa wa lugha hizo.
Nimetazama katika nchi 15 za Afrika zinazotabiriwa kuona mapinduzi makubwa ya 'start up tech ventures' Tanzania haimo! Hakuna shaka ni kwa sababu ya lugha. Ukitazama matumizi ya Twitter, WhatsApp, na social platforms nyingine katika nchi za Kenya na Uganda utaona namna gani Tanzania iko nyuma. Lugha!
Hii haina maana tusijivunie Kiswahili na tusifundishe kwa Kiswahili. Tatizo ni kwamba bado hatujakifanyia kazi Kiswahili kiasi ambacho kinastahiki kuwa lugha ya kufundishia. Huwezi kupata hata vitabu 10 vya rejea kwa katika fani yeyote!