Sababu za Tanzania kupitwa kimaendeleo na nchi nyingine

Angalia population ya na ukubwa nchi watu kisha ndio ulinganishe
 
Wakati JK anapambana kujenga shule za kata simlimuona mjinga!.
 
Hatuzalishi vitu vyenye thamani. Serikali inawajibu wa kuhakikisha nchi inazalisha vitu vy thamani, katika vionjo vya maendeleo tumekosa viongozi bora.
Tatizo halianzii kwenye vitu vya thamani peke yake tatizo ni ujinga na umasikini ndo bado vipo kwa watu wengi Kwanza serikali ikazane kuondoa ujinga kwa watu Ili waone umuhimu wa kutumia vitu vya kisasa alafu pale watu wanafanya kazi walipwe malipo mazuri kama ni wale wanaokosa mitaji na Nia ya kufanya biashara wanayo basi wakopeshwe mitaji kwa riba nafuu na popote panapohitaji pesa kama chuo na shule za elimu Bure pesa ipelekwe huko mfano Sasa hivi wanachuo wengi wanapitia maisha magumu kwa kukosa mikopo ya asilimia kubwa kitu kinachofanya wanashindwa kununua vitu vyenye thamani, wafanyakazi hivyo hivyo mpaka Leo mtu kama mwalimu anashindwa kununua hata mashine ya kufua nguo za familia yake inakuwa kama anasa Sasa hivyo vitu vya thamani vinakuwa kama vile ni vibaya au kama vile vina madhara kumbe ni ujinga na umasikini ndo kikwazo.
 
Kingereza kisingeweza kuunganisha makabila zaidi ya 100 yaliyopo hapa Tanzania. Wengi wangerudia kuongea lugha za makabila yao maana kingereza ni kigumu na ni lugha ya kigeni. Na hicho kingeleta ukabila alioupiga vita Nyerere.
Kiingereza kisiwe kwa kuunganisha makabila ila kiwe kwa kutuunganisha kimataifa ambayo ni level ya juu na kutusaidia kupata maarifa makubwa ya kimataifa maana ni lugha inayotumika kupata maarifa mengi tofauti na kiswahili kinachotuunganisha ndani ya Nchi peke yake, hivyo kufundisha watu wetu kiingereza bado ni jambo la muhimu sana na lazima pia.
 
Wakati JK anapambana kujenga shule za kata simlimuona mjinga!.
Ni kweli tunamshukuru kwa hilo hata hili la kuongeza vyumba vya madarasa pia tunashukuru litasaidia kuondoa ujinga ila bado shule za kata zinahitajika tena Nchi nzima maana zile za zamani zilijengwa kwaajili ya idadi ya waliokuwepo, na kingine Advance napo wamepasahau sana kama vipi wapafute wawekeze kwenye vyuo, ujinga siyo mzuri kabisa imagine mtu anadanganywa teknologia ni shetani na kwa kukosa elimu anakubali Ili na kuendelea kuishi kama mnyama wa msituni kitu kinacholeta ukosefu wa ajira maana hata watu wakiwekeza kama watu wanaogopa kutumia hivyo vitu kwasababu ya ujinga si biashara zitakufa?
 
Kingereza kisingeweza kuunganisha makabila zaidi ya 100 yaliyopo hapa Tanzania. Wengi wangerudia kuongea lugha za makabila yao maana kingereza ni kigumu na ni lugha ya kigeni. Na hicho kingeleta ukabila alioupiga vita Nyerere.
Huo muungano wa makabila zaidi ya 100 umesaidiaje Tz kutoka kwenye umasikini na kufanya ushindani wa uchumi wa maana?.......jilani wetu Kenya Gdp yake na jaribu mara mbili na ya kwetu, Sudani Ethiopia Tunisia Morocco Botswana Zimbabwe Angola wote wako juu kiuchumi kuliko sisi, bado tunasifia sera zatu zilizo tufanya tubaki nyuma wakati tunaongoza kwenye rasilimali.
 
I totally agree with you...
 

Tatizo kubwa ni uvamizi uliopewa Jina la muungano. Bila hili jinamizi kuondoka hakuna maendeleo yoyote yatayokuja
 
Tatizo kubwa ni uvamizi uliopewa Jina la muungano. Bila hili jinamizi kuondoka hakuna maendeleo yoyote yatayokuja
Sema tu siku tutakapo anza kikosowa sera mbovu za muasisi wa hi nchi hi na chama chake, ndo siku tukao anza tz mpya, yenye maono chanya, kusifi sifia ujinga wa viongozi wetu walio pita ndo kuna tuumiza na kutufanya masikini zaidi
 
Mfano wa Rwanda unatuambia “ili tuendelee tunahitaji uongozi bora”. Vita vya kimbari vilileta mauaji ya kutisha Rwanda 1994. Walichinjana watu laki nane.

Baada ya vita, Rais Kagame akachukua nchi. Ilikuwa kama failed state, lakini sasa ona waliko. UONGOZI BORA is the conditio sine qua non for development.

Rwanda haina ardhi kubwa. Wamebanana sana. Watu, ardhi na siasa safi siyo vitu vilivyoleta maendeleo Rwanada. Ni uongozi bora, full stop.
 
hv kenya na ss nani wanashabikia sana siasa.mm nadhani issue kubwa hapa kwetu ni katiba ndo inayotuharibia.tukipata katiba nzuri ya kuwajibishana tutakuwa sawa lkn haya malugha si ya maana sana sababu hata ujerumani ambao wako vzr hawayataki haya mavingereza pia ufaransa hawana haja na hayo malugha kwa hiyo tukomae kunadai katiba mpya.
 
Mada iko too general,ungespecify angle ambayo Tanzania inashindwa vibaya,kwa sababu kama ni GDP tz iko Top Ten Africa na ya 72 Dunia na katika nchi ulizotaja ni Ghana tu ndio ipo juu ya Tanzania in terms of GDP.Je unataka kulinganisha per capita income?GDP? au individual development? be specific please.
 
Swali la lugha sio kwamba tujue Kiswahili au Kingereza. It is not EITHER OR, but it is rather BOTH AND.
Watanzania wanaomaliza elimu ya sekondari na kuendelea waweze kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza.

Watoto wanaosoma international schools wanakuwa na hiyo hali ya kumudu lugha zote mbili. Na they are relatively highly employable.

Viongozi wetu wengi wanajua kwamba mtoto ni vizuri ajue lugha zote mbili kwa ufasaha. Ndiyo maana karibu wote wanasomesha watoto wao English Medium Schools. Wasidanganye wananchi kwamba Kiingereza sio muhimu.

Nimependekeza huko nyuma kwamba wafanyakazi wa serikali kuu lazima watakiwe kuwa fluent in both languages. This can be ensured during employment interviews.

Tutakuwaje taifa linalotegemea mchango mkubwa toka utalii wakati front line workers kwenye hiyo sekta (maofisa wa Uhamiaji, Polisi, people in the hospitality industry) ni zero kwenye luhga za kimataifa?
 
Kuna shida kubwa mahali ndo maana tubasogea taratibu taratibu, Jambo la muhimu ni kupiga chini watu ambao wamepewa dhamana muda mrefu wameshindwa kuonesha matokeo makubwa.

Jambo la pili, tunatakiwa kuwapa kipaumbele watu wabunifu hususani kwenye masuala ya teknolojia. Haiwezekani eti mtu anapanda cheo kisa kakaa muda mrefu kazini, kigezo kikubwa cha kupanda cheo kiwe mchango wa mtu wenye matokeo makubwa kwa jamii yake.

Zaidi, kwenye elimu inatakiwa watu wasome kweli kwa kuchimba na kutafuta ukweli juu ya changamoto zinazotukabili, mtu akiomba kwenda kusoma aeleze Kuna changamoto gani ambayo ameiona ndo anataka akaongeze elimu ili aje kuitatua, la sivyo hakuna haja ya kupoteza hela kusomesha watu ambao wanakariri vitu mwisho wanachukua degree, masters, PhD zao na kuja kupanda mishahara tu.

Kuna mengi ngoja niishie kwanza hapa.
 
Nini sababu ya nchi nyingine nazo kupitwa kimaendeleo na nchi nyingine ikiwemo Tanzania...
 
Nyerere alisema ili tuendelee twahitaji
Ardhi (tunayo)
Siasa safi (je tunayo?)
Watu (wapo au tupo. Ila tuna uwezo kiasi gani kuyatawala mazingira yetu kwa kukuza uzalishaji wenye tija)
Siasa safi (hapa tuna mjadala mkubwa sana. Polepole ameweka wazi siasa ndani ya chama cha zina mizengwe, uchawi, fitna; ukizubaa tu, ndio hivyo. JK wakati mmoja akiwa mkulu, aliweka wazi wanachama wa chama chake hawaachiani glass za vinywaji).

Ukiona tumefika pahala ambapo "kuna wale na sisi", tuna makundi ya Urais yalianza toka 1994 enzi za boys2men,wakaja wana-mtandao, mara mtandao ukafa kukawa na virungu chungu mzima, maana yake, nchi hii inahitaji reforms za "kufa mtu"

Rwanda PK kajitahidi sana kuiweka nchi kwenye ramani ya Afrika na ulimwenguni.

Tanzania tunakwama kwa kukosa nini kifanyike ili rasilimali watu izalishe kwa tija na kufanya biashara kukidhi mahitaji ya soko la ndani na then twende walau soko la EA na SADC.

Mpaka sasa elimu yetu ni a for apple na sio elimu yenye maswali kama apple zinatoka SA kuja hapa kwa miaka mingi, kwa ukubwa wa ardhi ya nchi hii ambayo ni virgin, nini tufanye ili ndani ya miaka 10 ijayo Tz iwe kwenye ramani ya exports ya apple zenye ubora kwa nchi zaidi ya 15 (8 za jirani & SADC)

Tuna viongozi wanaosaidia wakulu wenye fikra za nini nifanye niendelee kumpendeza mkulu. So, ni matamko, mipango, kuonekana kwa media ila ukipima kuna effors ndogo sana kukuza uzalishaji wa kibiashara.

Tunalima mahindi kila mwaka mpaka yanakosa soko, kwanini kusifanyike tafiti kule kwenye ukanda mahindi yanakubali tukazalisha breed inayokamuliwa mafuta ili ku-cover deficit ya mafuta ya kula worth 600bn kwa mwaka?
Watawala wetu badala ya kufikiri wa picha kubwa, wanawaza viwanda vidogo. Na kuna mmoja na masters holder akiwa waziri akawa anasema machine ya kuponda tofali au cherehani ni kiwanda kidogo. Very low sense of accountability.

Tukipata strategic thinkers kwenye leadership, tunaweza kusogea haraka sana. Ila kama ni hawa waimba hiena hiena na wale wanajiita "mimi ni chawa wa ...." mimi nina degree 4, tunazidi kuchelewa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…