Sababu za Tanzania kupitwa kimaendeleo na nchi nyingine

Mfano wako wa Rwanda. Umeharibu point zako nzuri!
Rwanda kilicholeta maendeleo ni matumizi Bora ya ardhi ya Congo DRC, full stop!

Wamejua kuitumia DRC!
Mkuu Bambushka,

Ujue ardhi ya DRC ilikuwepo siku zote. Kama ndiyo iliyowapaisha Rwanda, basi ujue ni alipopatikana kiongozi mzuri ndipo ilipotumika vizuri hiyo ardhi.
 
Safi kabisa
 
Ajabu nyingine ni kwamba mahakama zetu, maagizo mengi ya serikali, hukumu muhimu, vitu muhimu vinaandikwa Kiingereza wakati wengi hawajuhi hata wamehukumiwa nini, document zinasema nini? Mawakili nao wana- struggle to intepret hukumu.
Sure!
 
Nchi zote za afrika ya weusi uchumi wa mtu mmoja unafanana.
Mazingira, mifumo ya maisha wote ufanana.

Wengi hawajatoka hata nje ya mikoa yao wanajua kulalamika tu.

Mtu anakuja kusifia Senegal bila aibu. Rwanda ukitoa Kigali kwingine kote ni vijijini tu, Kigali yenyewe haiingii hata kwa Arusha zaidi ya usafi.
 
miaka 40 tangu vita ya kagera hatuja rekabisha uchumi watu kweli, kipindi hicho nchi nyingi kama Zimbabwe SA nk zilikua hazijapata uhuru, zimepata uhuru na kutupita, kwanini Tz hatuende mbele kiuchimi?

I reckon you know nothing about SA na Zim. Hakuna siku ambayo tumewahi kuipita SA kwa uchumi/maendeleo, matter of fact, SA imepitwa GDP na Nigeria kwa mara ya kwanza a few yrs ago.

Afu unajua SA ilipata uhuru lini? Au unaongelea 1994 Mandela alipopewa urais hata hapo SA tayari ilikua mbali sana. Urais wake ulikua ceremonial tu.
 
Elimu si tatizo, tatizo ni aina gani ya elimu unawapa watu wako.
Elimu ya sasa ni takataka imepitwa na wakati si tija kwa kizazi cha sasa zaidi ya kuwafanya watz wawe masikini tu.
Mfumo wa elimu wa mkoloni ndio mfumo sahihi zikiwemo mitaala yake.
 
Uongozi ndio tatizo bado atujapata kiongozi anaejua watz wanataka nini tangu UHURU,bali ni aina ya viongozi wanaotulazimisha vile watakavyo
 
Pia baadhi ya wananchi kupenda kulalamikia serekali pasipo kujituma na kusubiri kufanyiwa kila kitu
 
Sababu kubwa ni ufisadi uliojikita katika ngazi za juu👇🤡🤡🤡
Your browser is not able to display this video.
 
Yaani kama ulikuwa kwenye kichwa changu. Uliyosema yote ni kweli kabisa. Nini kifanyike? Misingi imekosewa tayari.
 
Njia pekee ni kwa watawala kuwaogopa wananchi kwamba wanaweza kuwaondoa madarakani pale wanapoleta ujinga kama huu wanaofanya ccm, sasa kwa bahati mbaya sana Tanzania ccm hawana hiyo hofu kwa sababu wanafahamu fika kwamba wananchi hawana jeuri ya kuwaondoa kwa sababu nchi imefikia hatua ambapo sasa hata uchaguzi haupo tena ni uhuni tu unafanywa.
 
Yaani kama ulikuwa kwenye kichwa changu. Uliyosema yote ni kweli kabisa. Nini kifanyike? Misingi imekosewa tayari.
Nini kifanyike?
Hili ni swali kila mtu ana maoni yake. Kama vile ugonjwa wa kansa, kuna wengine watapendelea kuichoma na wengine watasema tuikate!
Binafsi nimeshaona kuwa kipaumbele cha kuirekebisha nchi hii kwa hivi sasa ni KATIBA kwanza. Katiba itakayowapa raia madaraka ya kugeuza uongozi. Ni dhahiri Katiba tuliyonayo haikidhi jambo hilo. Tukiwa na Katiba inayowapa raia nguvu, angalau (angalau) twaweza kuzungumzia kuirekebisha nchi hii. Katiba hiyo iruhusu mgombea huru na kura ya maoni kwa maamuzi makubwa. Nadhani tuanzie hapo. Wengine huenda wakaja na mapendekezo mengine ambayo pia yanaweza kufaa. Kansa haina matibabu ya aina moja!
 
Can u imagine nchi inapiga marufuku watumishi wake kusafiri nje ya nchi...unategema watatunga sera gan kama sio kuimba mapambio ya gwajiboy
 
Kingereza kisingeweza kuunganisha makabila zaidi ya 100 yaliyopo hapa Tanzania. Wengi wangerudia kuongea lugha za makabila yao maana kingereza ni kigumu na ni lugha ya kigeni. Na hicho kingeleta ukabila alioupiga vita Nyerere.
Kiswahili lugha ya nani?
 
Matatizo ya Taifa hili ni[emoji116]
-Ccm na viongoz wake.

-Aina ya uongozi(democracy), hii haiwez leta maendeleo ktk taifa hili bila kutumia udicteta, maana kuna wapuuzi wachache wanaohujumu hili taifa wanatakiwa kushughlikiwa bila kujali Haki za kibinadamu na mashirika ya magharibi yatazungumzaje.

-Mifumo mibovu na hovyo ya Elimu

-ukoloni mamboleo, hapa unajionea mwnyewe yaan saut za mataifa ya mbali yananguvu kulko saut ya viongoz wa ndani ya nchi,
yaan mpka sas bado wageni wanaitawala hii nchi kiuchumi, kitechnolojia, kisiasa na kijamii, em fikil kuhusu suala la maadili ya wananchi wa taifa hili yanapokengeukwa na waTz wanapojarbu kukemea kuna hayo mashirika yenye nguvu tokea izo nchi babe yanakuja kutetea uovu na kuupa kinga mfano Ushoga,usagaji, malez mabaya ya watoto,
Pia bado sauti za hawa mabeberu zinanguvu kuikandamiza hii nchi kupitia vibaraka wao wanaojiita wawekezaji wanaokomba resources za nchi na kubakisha umasikin.

-Dini na imani ngeni, hapa ndpo tulpo harbu kwa kuikataa Nguvu ya Uungu ya kwel na kukubali Miungu migeni itutawale na kukumbatia utandawazi, jambo lililopelekea kupoteza ukuu wetu na nguvu zetu za akili na uvumbuzi,
kwa hil linaweza kuwa ndio jambo la kwanza sababishi la unyonge wa nchi ya Tz na nchi zote za watu weusi, maana maendeleo yanahitaji akili na maarifa, sasa sie tutapata wapi maarifa kama ubongo/bongo zetu zimekuwa washed na kuwa outdated kwa kuzipa kipaumbele imani zisizo zetu.

Acha tuendelee kupigika mpka tutakapoijua kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…