Sababu za waimbaji wengi kufilisika Duniani kulipa watu ovyo

Sababu za waimbaji wengi kufilisika Duniani kulipa watu ovyo

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Mnafikiri pesa za kulipa vitu vyote visivyo na maana zinatoka wapi. Dunia nzima hii ndiyo sababu ya kufilisika kwa waburudishaji wengi. Oprah alisema wengi wao hata matumizi na checks hawaandiki wenyewe😲

 
Hawana maisha kiivyo wasanii Ila wanajikuza sana waonekane kama maisha wameyapatia.Hebu jiulize kama watu walivyokuwa wanafikiria harmonize ana pesa kumbe masikin mwenzangu tu anasema ameuza nyumba tatu kwa ajili ya kulipa million 500 na bado anadaiwa hebu jiulize vp kwa wasanii wengine ambao tunaona wana maisha mazuri.

Harmonize kuna kipindi alisema amezawadiwa SAA ya sh.million 400 na mpenzi wake Sarah hivi kwa safari anazofanya hata nje ya nchi kweli yeye ni wa kukosa million 500 hapo ndio napata jibu kuwa wasanii wetu wanatumika kama punda kusafirisha mizigo ya watu nje huko.

Hata Diamond platnumz huyu ambae Leo tunamuona ana ukwasi akipata shida let'say anadaiwa million 800 na kampuni flani kama fidia usishangae anarudi kwa wananchi kuomba msaada
 
Uzuri ukiona limekufika ujue ni saizi yako.
Wewe unaemwambia mwenzako kuwa yeye angetoa ikweta, huo ndio mwisho wako wa kufikiri katika kujikwamua na ndio mana tuna makaka poa. Waliwawazia wenzao hivyohivyo, siku yalipowakuta wao wakajikuta wanatekeleza kwa vitendo wao wenyewe mawazo yao
 
Kaka Mshana hoja yako naipinga kwa asilimia 95,,Usiseme wasanii duniani afadhali ungesema wasanii wa kibongo,vilevile hata wasanii wa kibongo sio wote wana akili hio ni baadhi yao
Kama vile Mr Nice,alikuwa na wapambe kiasi kwamba akisafiri ktk show zake mikoani,wapambe tu wanajaa ndani ya costet[emoji38]
TID alikua akienda sehem msafara kuliko wa waziri mkuu[emoji38]
Lkn kuna wasanii waliotuliza akili zao kama vile sugu,profesa J,diamond,lady jdee na wengineo hao walikuwa wakiwekeza wakati wana make money
Walifungua miradi biashara.na maisha yaliendelea
Leo masanja mkandamizaji kila msimu wa kilimo cha mpunga hakosi gunia elf na kuendelea
 
Mimi ushauri wangu ni hawa vijana wapunguze wapambe ambao wanaliipwa bila sababu hawa wote wanaotwmbea naye mnafikiri wanaishi vipi? Baada ya miaka kumi wote wanakukimbia. Lakini wahakikishe malipo yote wanajua nani analipwa kupunguza kuibiwa. Ni wazo tu
 
Wivu tu mwache Konde Boy afanye yake....Hata mie nikipata mkwanja nitafanya zaidi ya Konde Boy #KONDE_GANG_UNO
 
Wivu tu mwache Konde Boy afanye yake....Hata mie nikipata mkwanja nitafanya zaidi ya Konde Boy #KONDE_GANG_UNO

Ni ushauri tu kuhakikisha hafilisiki ndugu. Sina sababu yeyote ya kumuonea wivu maana kila mtu ana maisha yake na sitabadilisha maisha yangu kwa lolote lile. Hakuna watu wawili sawa Duniani ni kushauriana tu ili twende mbali zaidi na tufanye makubwa zaidi.
 
Majuz juz niliona baadhi ya mastaa kma shikole na lemutuz wakipost vimjengo vyao vya kawaida mpka nikawaza kwa umaarufu wote na show zote ndio kwanza kamjengo kamoja kama lemutuz ata kumalizia nyumba bado tena mtoto wa waasisi wa chama na taifa
 
Majuz juz niliona baadhi ya mastaa kma shikole na lemutuz wakipost vimjengo vyao vya kawaida mpka nikawaza kwa umaarufu wote na show zote ndio kwanza kamjengo kamoja kama lemutuz ata kumalizia nyumba bado tena mtoto wa waasisi wa chama na taifa
kwa wasanii wa bongo sijaona mwenye mjengo wa maana wote wana mapagale tu.
 
Back
Top Bottom