Sababu za Wanaume kutonufaika na ndoa

Sababu za Wanaume kutonufaika na ndoa

Last KING Ontuzu

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
644
Reaction score
927
Wanaume hawanufaiki na ndoa!!!
1. Ana miaka 72.
2. Amestaafu kutoka katika huduma ya kazi.
3. Amejitolea maisha yake yote kuwalea watoto wake.
4. Amekataa starehe za maisha ili kugharamia ada ghali za shule na gharama za maisha ya watoto wake nje ya nchi.
5. Sasa wanaishi vizuri Ulaya, ama jijini Dar, Mwanza au Arusha
6. Mkewe, mwenye umri wa miaka 62, amehamia kuishi na watoto wao.
7. Yeye amebaki peke yake huko kijijini.
8. Watoto wake humpigia simu kidogo sana.
9. Anapaswa kuanza maisha upya kama mzalendo.
10. Anapambana na shinikizo la damu na magonjwa mengine yanayohusiana na uzee.
11. Atasurvive peke yake kwa muda gani zaidi?
12. Hii ndiyo hali halisi kwa wanaume wengi wa tabaka la kati: uzee wao mara nyingi ni wa upweke na, kwa visa vingi, huzuni.
13. Haijalishi jinsi mwanaume alivyo mzuri,aliyewajibika kwa familia yake, wanawake huonekana kuwapenda watoto wao zaidi ya waume zao. Kadri anavyozeeka, na waume zao kadri wanavyozeeka ndivyo inaonekana wana umuhimu mdogo kwao.
14. Kwa hivyo, wanaume wanufaikaje kweli na ndoa?
15. Wanatoa maisha mengi lakini wanapata kutambuliwa kidogo kwa kazi yao ngumu, huku mwanamke akionekana kuvuna faida zote.
Aliyeimba wanaume wameumbwa mateso kuhangaika huenda aliyaona haya pia .
Ukiwa kama mwanaume hali hii inaweza kuwa yako katika miongo michache ijayo.nini Unachofanya kuhusu hilo? Mpango wako wa kustaafu ni upi? Jali nafsi yako kama unavyojali familia yako. Jipende mwenyewe. Mungu akubariki.
 
1000011282.jpg
 
Wanajizima data 😹😹😹
Kuna mama mwanae kamuita Marekani kagoma kurudi tizii, mume analalamika watoto wamrudishie mkewe.!!
Mie siamini kama mtu umeishi vizuri na mke, na watoto haujawahi kumuabuse mke mbele ya watoto.....from no where tu wakutenge hii kitu haipo.

Ujue kumtandika mke (mama wa watu, na wenyewe wanakuona) sio jambo jema na hawasahau hata ipite miaka na miaka.
 
Ndio hivyo tatizo wanajisahulisha, ila hata ingekuwa mimi nishafika kwa Biden nirudi nchi ya tozo kufanya nini??
Huyo mume atajiju si ahudumie mifugo 😹😹😹
 
Ndio hivyo tatizo wanajisahulisha, ila hata ingekuwa mimi nishafika kwa Biden nirudi nchi ya tozo kufanya nini??
Huyo mume atajiju si ahudumie mifugo 😹😹😹
Kuna dingi angu (r.i.p), mambo ya ndoa ni magumu ila mzee alikuja kupata li jimama basi akawa analala huko eti lile lijimwanamke linafua nguo then linaleta pale home, kwenye misiba anaenda na jimama.....basi mkewe anafatafata nyuma kama mlinzi, watoto ni wakubwa kabisa na wana familia zao ila imagine sasa kuona hayo mama yao anatendewa.....

Weee saa ngapi wasimchukue, dingi alitelekezwa hii hali ilichangia sana kifo chake
 
Safi sana hiyo ndo dawa yao
 
Back
Top Bottom