Sababu zifuatazo zinaweza kumfanya mteja avuliwe ufalme

Mteja ni mfalme ila kuna wakati naye huzingua na kujikuta kajivua au kuvuliwa ufalme wake na kuonekana kenge tu. Sababu zinaweza kuwa hizi.

1. Mteja anayeona duka linafanya SALE ila bila aibu anaomba apunguziwe tena bei.

2. Mteja ambaye baada ya kupewa bei hujibu "nyie bei ghali sana kwa fulani tunapata kwa bei hii"..😡

3. Mteja anayeuliza bei za karibu vitu vyote dukani halafu hanunui chochote.

4. Mteja ambaye kwenye maduka ya nguo anaomba kujaribisha hadi chupi au boxer kama inamtosha. Kuna mdada alinitaka kunirudishia boxer anasema imembana mumewe. Nusura nimtukane ila akawa mjanja kutojibu ovyo nilivyomwambia huwa hazirudishwi.

5. Mteja ambaye anajua kabisa kuna vitu haviwezi kabisa kuwepo kwenye duka alilopo ila ataulizia tu kama vile kujikweza.
 
Attachments

  • SGN_05_04_2024_1714832545958.png
    SGN_05_04_2024_1714832545958.png
    213.5 KB · Views: 3
Mkuu wewe unaonekana sio mfanyabiashara ni mteja kama wateja wengine ngoja nikupe story kidogo

Mm nafanya biashara z wakati naanza nilikuwa na iyo tabia simuachi mteja hata kama nimefunga madirisha nafungua moja kumhudumia kumbe jamaa wananichora

Kuna siku walikuja jamaa wawili nyakati za kufunga wakawa wanaitaji huduma nikasema ngoja nisiache hela walikaa pale kuzuga kama dk 5 ivi au kumi kumbe wanawasiliana, basi wakafanya huduma wakoandoka nikafunga

Huwa sipitiagi njia moja nikienda kwangu basi nikabadili njia ila kuna kama mmoja nilimuona ivi amesimama si karibu na ofisini kwangu ila sikumtilia maanani aisee kwenda mbele nilikutana na jamaa kama sita ivi mmoja kashika kisu kuanza kunikaba bakhat nzuri sikuwa hata na simu wala hela nilikuwa na kibegi ambacho niliweka vikolokolo wakachukua wakasepa

Kwaiyo kwa mteja hawezi jua hizi risk anajua yeye alivyo wote ni sawa wengine wanatumia mianya kusoma ramani mfanyabiashara siku zote unatakiwa kuwa makini
Mkuu ulikutana na wezi pole sana…ila nakwambia chunga sana attitude yako dhidi ya wateja, wao ndo wana iyo ela unayoitaka na kumbuka iyo bussines sio kwamba unayo peke yako Tz nzima kuna vitu vidg vidg sana vitakutofautisha na competitors wako…mimi ni mfanyabiashara ni nimefanya kazi kwenye makampuni makubwa najua how customer anavyoheshimiwa no matter what, na anavyoangaika kutafutwa watu wanalipia millions of money kuhangaika kufanya matangazo ili kumvuta uyo mteja…naelewa ivi vitu mzee! Kaulize watu wanaofanya kazi za customer care za mitandao uone?? Hutakiwi kumjibu mteja ovyo ata akutukane…wanajua wanavyolipia matangazo kila siku ili kumpata na hawataki kumpoteza sasa hiyo ndo proffesional na saikolojia ya kuhandle customer sasa ww nenda kienyeji
 
So mkuu izo ulizoandika alo juu ndo sheria unazotambia kwamba mtu hakudharau..poa fanya ivi biashara ni huria weka bango tu kwenye biashara yako kuanzia point ya kwanza kwamba rule #1. Nikikutajia bei si ruhusa kuomba bagenii #.2 ukiulizia kitu lazima ununue #.3 ukijaribu lazima ununue #4. Si ruhusa kuuliza bei ya bidhaa ya vitu vyote dukani

Afu uku pembeni wamachinga wanamforce mtu ata ashike nguo ili aongee nae tu uku iliari mtu ataki kununua ila anamwambia kuona bure kujaribu bure kasoro kuondoka nayo tu ndo na ela
Mkuu unaweza ukafanya hivyo na bado watu wakafurika inategemea unauza nini na wapi. USIKARIRI
 
Mkuu kwenye biashara uki torture watu sana wakapata mpinzani utapata anguko baya sana in a longrun, nakupa mfano dodoma kuna bar moja inaitwa bambaraga huyu jamaa kipindi anatamba enzi izo ukienda bodaboda walinzi wanakataza usiingie wanakufukuza. akati ww unaenda kutumia ela mle sasa badae akaja rainbow utashanga siku ni jmos au ijumaa rainbow imejaa bambaraga hamna raia u see what i mean
 
Kwa waswahili ,ulivyosema kuvuliwa Ufalme nikajua mwanaume kuachia mlango wake.
 
Mkuu kwenye biashara uki torture watu sana wakapata mpinzani utapata anguko baya sana in a longrun, nakupa mfano dodoma kuna bar moja inaitwa bambaraga huyu jamaa kipindi anatamba enzi izo ukienda bodaboda walinzi wanakataza usiingie wanakufukuza. akati ww unaenda kutumia ela mle sasa badae akaja rainbow utashanga siku ni jmos au ijumaa rainbow imejaa bambaraga hamna raia u see what i mean
Hakuna wateja wanafiki kama wateja wa Bar.. hata ungekuwa unawahudumia kiasi gani ikifunguliwa bar nyingine wanahama. Tumia mfano mwingine
 
Mkuu ulikutana na wezi pole sana…ila nakwambia chunga sana attitude yako dhidi ya wateja, wao ndo wana iyo ela unayoitaka na kumbuka iyo bussines sio kwamba unayo peke yako Tz nzima kuna vitu vidg vidg sana vitakutofautisha na competitors wako…mimi ni mfanyabiashara ni nimefanya kazi kwenye makampuni makubwa najua how customer anavyoheshimiwa no matter what, na anavyoangaika kutafutwa watu wanalipia millions of money kuhangaika kufanya matangazo ili kumvuta uyo mteja…naelewa ivi vitu mzee! Kaulize watu wanaofanya kazi za customer care za mitandao uone?? Hutakiwi kumjibu mteja ovyo ata akutukane…wanajua wanavyolipia matangazo kila siku ili kumpata na hawataki kumpoteza sasa hiyo ndo proffesional na saikolojia ya kuhandle customer sasa ww nenda kienyeji
Mkuu wateja huwa wastaarabu wanapoface customer care wa makao makuu au sehemu yenye hadhi mfano ofisi kubwa lakini hizi ofisi zenye vumbi za uswazi wanakuwa na nyodo sana na wahuni wengi na wadokozi sio sawa na izo kampuni kubwa

Mtu akienda kwenye kampuni kubwa au makao ya mtandao fulani ananyenyekea kila atakachoambiwa kama ataleta challenge ni ndogo kulinganisha na wakala wa mtaani

Sasa ukisema nimekutana na wezi unamaanisha nini? asa mteja mwizi na asie mwizi utamjuaje?
 
Mteja hajawahi kuwa mfalme. Hiyo ni lugha ya kibiashara kumvutia atoe hela yake tu.
Nakubalina na wewe.

Anakuwaje mfalme wakati kinachofanyika hapo ni mabadilishano? Yeye anatoa pesa mimi nampa bidhaa au huduma, hata kama sio kwangu popote pale itabaki kuwa hivyo. Kwahiyo kila mtu anamhitaji mwenzie.

Kwa maana hiyo kauli "Mteja ni mfalme" ipo kwaajili ya kumvimbisha kichwa tu na haina uhalisia wowote.
 
Wateja wanaokuja kwa makundi kutafuta kitu kimoja na wateja wanaokuja na washauri, wanakuwaga miyeyusho sana
 
5. Mteja ambaye anajua kabisa kuna vitu haviwezi kabisa kuwepo kwenye duka alilopo ila ataulizia tu kama vile kujikweza.
Enzi za balehe nilisumbua sana watu na hii kitu. Unaenda duka la madawa unaomba wakupimie maharage ½ kilo.
 
Na kiingereza chako cha juhudi binafsi unaona umeandika point. Kulikuwa kuna haja gani ya kubandika bei kama sio lazima? Wateja pia akiona uko cheap hata kwenye sheria ulizojiwekea ndo wanakuwa hawaji wanaenda kwingine. Arusha kulikuwa na wahindi ambao ukitaka kuongeza sukari kwenye chai unalipia kijiko Tsh 50 na watu walikuwa wanajaa.
Siyo maneno yangu tu ni msimamo wa sheria.
 
So mkuu izo ulizoandika alo juu ndo sheria unazotambia kwamba mtu hakudharau..poa fanya ivi biashara ni huria weka bango tu kwenye biashara yako kuanzia point ya kwanza kwamba rule #1. Nikikutajia bei si ruhusa kuomba bagenii #.2 ukiulizia kitu lazima ununue #.3 ukijaribu lazima ununue #4. Si ruhusa kuuliza bei ya bidhaa ya vitu vyote dukani

Afu uku pembeni wamachinga wanamforce mtu ata ashike nguo ili aongee nae tu uku iliari mtu ataki kununua ila anamwambia kuona bure kujaribu bure kasoro kuondoka nayo tu ndo na ela
Ajaribu aone
 
Mteja ni mfalme ila kuna wakati naye huzingua na kujikuta kajivua au kuvuliwa ufalme wake na kuonekana kenge tu. Sababu zinaweza kuwa hizi.

1. Mteja anayeona duka linafanya SALE ila bila aibu anaomba apunguziwe tena bei.

2. Mteja ambaye baada ya kupewa bei hujibu "nyie bei ghali sana kwa fulani tunapata kwa bei hii"..😡

3. Mteja anayeuliza bei za karibu vitu vyote dukani halafu hanunui chochote.

4. Mteja ambaye kwenye maduka ya nguo anaomba kujaribisha hadi chupi au boxer kama inamtosha. Kuna mdada alinitaka kunirudishia boxer anasema imembana mumewe. Nusura nimtukane ila akawa mjanja kutojibu ovyo nilivyomwambia huwa hazirudishwi.

5. Mteja ambaye anajua kabisa kuna vitu haviwezi kabisa kuwepo kwenye duka alilopo ila ataulizia tu kama vile kujikweza.
Jibu ni Moja tu I like challenge
 
Back
Top Bottom