Sababu zilizosababisha 'Upinzani' kufeli vibaya

Sababu zilizosababisha 'Upinzani' kufeli vibaya

Tuliwauliza makamanda mbona hata mabango na vipeperushi vy mgombea Urais Lissu amuweki.
wakajibu"Lissu ni rais wa mioyo ya watu wakati Magufuli ni Rais wa mabango"
kumbe bwana Mbowe kagoma kutoa fedha za chama kufanya kampeni.

Unataka kweli kuitoa madarakani CCM hata fedha za kampeni huna utaweza wapi. lichama lenyewe la CCM lishakita mizizi.
Bado una mtu anakuita mke wangu/ mume wangu kwa akili hizi ulizo nazo?
 
Kushindwa vibaya kwa upinzani hususani chama kikuu chadema, binafsi naziweka ktk sababu kuu mbili. Makosa ya kitaasisi (Chama) na makosa yanayofanywa na mgombea mwenyewe.

MAKOSA YA KITAASISI:
1. Chama kimeingia kwenye kinyang'anyio kikiwa hakijajiandaa. Kutojiandaa kumetokana na kupoteza muda mwingi kudhibiti migogoro ya ndani, hasa kuhusu ubadhirifu wa fedha. Kosa hili lilisababisha Mwenyekiti kutumia nguvu sana kudhibiti hata kukiuka mambo mengi ya kikatiba. Utaliona hili hata ktk uchaguzi wa ndani ya chama alipolazimisha nani awe kiongozi na na nani atoswe. Hata makamu wa mwenyekiti alIpatikana kwa tamko tu la mwenyekiti kuwa ameamua awe nani na akampelekea fomu huko alikokuwa.

2. Kosa kubwa jingine ni lile lililofanywa 2019 kususia Uchaguzi wa serikali za Mitaa na CCM Kuchukua mitaa yote. Chadema walikosa viongozi ktk base ya chini kabisa kama fulsa ya kufanya siasa za ushawishi.

3. Ususiaji wa vikao vya Bunge hasa wakati wa janga la Korona kulitoa taswira hasi kwa wapiga kura. Uchafuzi kwa mataifa na Shinikizo ulioshindwa, uliofanywa ndani na nje ya nchi na chama hiki kwa kuongozwa na kushikiwa kidedea na Lissu, lilifanya mtu huyu aonekane kama msaliti wa Taifa. Lissu alitiliwa mashaka na wapiga kura tangu alipoanza kuzunguka duniani akitoa kashfa kwa Taifa lake, inashangaza kwa nini chama kiliamua kumuingiza kwa nguvu katika mchakato wa kinyang'anyio cha ngazi ya juu ya uongozi wa nchi.

4. Kupinga maendeleo waliyoyaita ya vitu hali kuwa wananchi wamekomboka kwa vitu hivyo hivyo ni kosa jingine kubwa. Mbaya zaidi kutaka kuaminisha watu wa maeneo fulani hawastahili kupatiwa maendeleo hayo yanayofanywa maendeo mengine nchi nzima, kwa kigezo cha atokako Rais imekuwa kichekesho sana. hasa pale kwa watu wa eneo hilohilo unalodhani hawasitahili kupata vitu hivyo, ati unaenda kuomba kura.

MAKOSA YA MGOMBEA:
1. Kosa la kwanza la mgombea ni kutumia madhira ya kujeruhiwa kwa risasi 16 iwe ni kigezo cha kuchaguliwa. Kwa tukio hilo, alianza kampeni kwa kuaminisha wapiga kura kukosekana kwa Demokrasia haki na utawala wa sheria. Cha ajabu akililia hayo mwenyewe na mwenyekiti wake wakionekana mubashara wakiwafukuza waandishi wa habari na walinzi ktk mikutano yao, wakisahau kuwa nao pia ni wapiga kura. Wakipinga mambo ambayo yapo kisheria. Na muda mwingi akizungumzia Hayo bila kueleza atawafanya nini akishika madaraka.

2. Mgombea alijikita katika vitisho akidhani anaitishia serikali CCM na Tume ya uchaguzi. Asijue asijue wapiga kura sio wana CCM tu. vitisho hivyo vinamadhara mpaka wa wapiga kura watakaompigia kura yeye ktk kujitokeza kupiga kura. Alitaka kudanganya wapiga kura kuwa kwa kumtumia wakili wake toka ughaibuni serikali serikali imeingia woga wa kumuacha afanye atakavyo. Kumbe huyu amemharibia kwa kumjengea taswira ya kuwa na mamluki katika mapambano hayo kwa uhuru aliompatia kupambana na serikali kwa niaba yake.

3. Kosa la kiufundi la dakika ya 96 ni kumeza ndoana iliyorushwa na Mgombea wa CCM. Pale alipowaomba vijana wasijiingize kwenye vurugu zinazonadiwa na mgombe huyu sababu yeye ana tiketi ya kuondoka nchi akiwaacha wanashughulikiwa. Bila, kujua madhara yake akajitokeza na kukiri kuwa ni kweli ana tiketi hiyo na ataondoka baada ya uchaguzi. Hiyo pekee imepunguza kura na waliomshabikia kuona hakuna haja ya kusikiliza ushawishi wake wa kufanya vurugu. Hata maagizo ya kutokubaliana na matokeo yamekosa nguvu.

4. Kosa jingine. Alijikita kuaminisha kuonewa kwa Wafanyakazi, wafanya biashara na Wakulima. Kwa hili natawalaumu viongozi wa chama chake iwapo si kiburi cha mgombea wao. Hawaku mfahamisha, kwa miaka mitatu aliyokuwa ughaibuni Rais alishakutana wa makundi hayo na wakamueleza shida zao, wakulima wakafutiwa kodi zenye kero, road brock zikabaki kwa wakulima/wafanyabiashara wakubwa wa mazao. Wafanyabiashara wakaeleza na kutatuliwa matatizo yao na TRA. Wamachinga wakatatuliwa matatizo yao. Wachimbaji madini wakubwa kwa wadogo n.k. Tena kwa kero nyingine kutatuliwa papo kwa papo ktk mikutano yake na makundi hayo. Matokeo ndi yo hayo, makundi yote hayo yamemupuuza na kumchagua mgombea ambaye Lissu alidhani anamfitini nao

5. Tabia yake ya kumkosoa Rais na Serikali yake kwa kuzunguka katika mataifa mbalimbali duniani, imeongeza mtazamo hasi kwa wapiga kura wengi, ya kuoneka mtu huyu ni kibaraka asiyeitakia mema nchi yake. akitumia madhira aliyoyapata kupatia kipato bila kujali athari za kiusalama na kiuchumi kwa nchi yake
Kwa nondo kama hizi ,

Kibaraka wa lissu akija kupinga basi anapenda tu ubishani maana kuna watu kazi mkumbo tu hawajui lolote...zaidi ya kujifurahisha kwa maneno ila umeongea ukweli asilimia kiba100.

Kongole.
 
Sababu ni lukuki. Sababu nyingine ni USHOGA kwamba waTZ jambo hilo lilikuwa chukizo kubwa na hivyo liliwakimbiza wengi na kujiweka mbali na Mgombea pamoja na CDM yenyewe.
 
1. Vyama vingi kama sio vyote vya upinzani havina mizizi ngazi za chini badala yake vina majina makubwa ya viongozi pale juu wanaofanya propaganda kubwa.

2. Hakuna tafiti za kina zinazofanyika tokea chaguzi moja mpaka chaguzi nyingine nini hasa sababu ya kushindwa jambo linalopelekea kubakia na sababu moja tu ya kisingizio kuwa kura zimeibiwa.

3. Sera za kujiuza kwa wananchi zimechukuliwa na chama tawala( i.e Ufisadi) na kufanyiwa kazi nzuri na chama tawala. Upinzani umebaki na vitu vyepesi sana kama kuwaambia wananchi eti vitambulisho vya machinga kuwa eti wamepigwa!

Unaweza kuongezea.
Mtazunguka kote ila sababu iliyofanya upinzani kufeli vibaya ni moja tu ni hii 👇👇👇
View attachment 1618707



SORRY CHARLIE .

 
Bado una mtu anakuita mke wangu/ mume wangu kwa akili hizi ulizo nazo?
uwezi kuitoa madarakani CCM kwa mbwembwe za mitandaoni wala mbwembwe za wakina Armstadam.
maneno kama #Niyeye mara tunajamboletu mara sijui kapigwa risasi 16.ni upumbavu mtupu.
 
Sababu ni lukuki. Sababu nyingine ni USHOGA kwamba waTZ jambo hilo lilikuwa chukizo kubwa na hivyo liliwakimbiza wengi na kujiweka mbali na Mgombea pamoja na CDM yenyewe.


Huyu shoga aliyepewa uwaziri na Shoga mwenzake jee vipi ??


 
uwezi kuitoa madarakani CCM kwa mbwembwe za mitandaoni wala mbwembwe za wakina Armstadam.
maneno kama #Niyeye mara tunajamboletu mara sijui kapigwa risasi 16.ni upumbavu mtupu.

1604413383903.png
 
Mlishaambiwa kitambo anzisheni chama madhubuti cha siasa, na wala siyo kijikundi cha uanaharakati bandia. Mwisho wa kunuu.
 
uwezi kuitoa madarakani CCM kwa mbwembwe za mitandaoni wala mbwembwe za wakina Armstadam.
maneno kama #Niyeye mara tunajamboletu mara sijui kapigwa risasi 16.ni upumbavu mtupu.
Kweli sio rahisi kumtoa jambazi mzoefu kama hutatumia nguvu ya ziada

 
Hapana siyo kweli...
Ukweli ni kwamba hakuna chama tawala kitakaochokubali kuachia kiti kwa urahisi...



Cc: mahondaw
 
KAMA HUJAANDIKA DIKTETA UCHWARA JIWE NDIO SABABU ZA KUZURUMU USHINDI WA WAPINZANI BASIBUTAKUWA KICHWA MAJI.
 
1. Vyama vingi kama sio vyote vya upinzani havina mizizi ngazi za chini badala yake vina majina makubwa ya viongozi pale juu wanaofanya propaganda kubwa.

2. Hakuna tafiti za kina zinazofanyika tokea chaguzi moja mpaka chaguzi nyingine nini hasa sababu ya kushindwa jambo linalopelekea kubakia na sababu moja tu ya kisingizio kuwa kura zimeibiwa.

3. Sera za kujiuza kwa wananchi zimechukuliwa na chama tawala( i.e Ufisadi) na kufanyiwa kazi nzuri na chama tawala. Upinzani umebaki na vitu vyepesi sana kama kuwaambia wananchi eti vitambulisho vya machinga kuwa eti wamepigwa!

Unaweza kuongezea.

Acha hizo porojo Kwani miaka walipokuwa wanafanya vizuri walikuwa na mizizi huko vijijini. Kwanini watanzania wengi ni wanafki kiasi hicho. Kura zimepigwa nje ya vituo na nje ya utaratibu wa uchaguzi halafu unaongea huo ujinga. Ni wizi wa kura ndo uliofanyika, upinzani siyo viongozi wanaokubaliana na wizi ndo maana mafisadi yote yako CCM hayawezi kutoka wala kuachia serikali kwa hofu ya kushugulikiwa na mkono wa sheria. Kwa sasa hiki chama hakiwezi kuondolewa kwa sanduku la kura
 
1. Vyama vingi kama sio vyote vya upinzani havina mizizi ngazi za chini badala yake vina majina makubwa ya viongozi pale juu wanaofanya propaganda kubwa.

2. Hakuna tafiti za kina zinazofanyika tokea chaguzi moja mpaka chaguzi nyingine nini hasa sababu ya kushindwa jambo linalopelekea kubakia na sababu moja tu ya kisingizio kuwa kura zimeibiwa.

3. Sera za kujiuza kwa wananchi zimechukuliwa na chama tawala( i.e Ufisadi) na kufanyiwa kazi nzuri na chama tawala. Upinzani umebaki na vitu vyepesi sana kama kuwaambia wananchi eti vitambulisho vya machinga kuwa eti wamepigwa!

Unaweza kuongezea.

Wapinzani wameshindwa mbinu za wizi thus wameshindwa ndio jibu
 
Back
Top Bottom