SoC01 Sababu zinazochangia kuua elimu Tanzania

SoC01 Sababu zinazochangia kuua elimu Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

HIBISCUS 80

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2020
Posts
1,058
Reaction score
1,218
Natumaini mnaendelea vema na shughuli za ujenzi wa familia zenu
Leo napenda kuongelea sababu zinazochangia kuua elimu katika nchi yetu ya TANZANIA
Nitaongelea sababu hizo kutokana na uzoefu wangu katika sekta ya elimu

SHULE ZINAZOMILIKIWA NA WATU BINAFSI
Shule ZINAZOMILIKIWA na watu binafsi zimechangia sana kuua elimu ya TANZANIA kwani malengo makubwa ya wamiliki wa shule binafsi ni kupata faida.

Pamoja na kwamba wanatoa elimu lakini lengo kuu ni kupata faida kwa kupata wanafunzi wengi.
Ili shule ipate wanafunzi wengi ni lazima. Shule ipate matokeo mazuri katika mitihani ya Taifa.

Sasa basi Mambo yanayofanyika Ili kupata hayo matokeo mazuri li shule ijulikane Mambo yafuatayo yanafanyika shuleni

1. Wanafunzi wanakaririshwa na kufundishwa kujibu mitihani pekee
Walimu tunafundisha ku solve past papers badala ya kufundisha watoto topics ziinazotakiwa.

2. Walimu wanahimizwa kumaliza topics haraka halafu wanafunzi waanze kusolve past papers. Sababu kubwa za kusolve past papers ni kuwa baraza la mitihani linarudia maswali kila mara .

3 Pia mwalimu ukionekana unafundisha watoto kwa kina wenzako wanaku discourage na kukwambia usihangaike kufundisha hiyo topic kwani hiyo haijawahi kutoka kwenye national exams Sasa unajiuliza kwani hii topic haiwezi kumsaidia mwanafunzi katika maisha yake ya kila siku?na kwa Nini Iko kwenye mtaala?mfano mwalimu mwenzako anakwambia usihangaike kufundisha kuhusu sikio baraza la mitihani halitoagi maswali hayonasiku swali likitoka linakuwa na marks kidogo angalia topics zenye marks nyingi.Kwa vile wewe unataka ugali inabidi uguate mkuu wa idara anavyosema

4. walimu tunakomaa kufundisha maswali Ili watoto wakariri maswali wafaulu uonekane mbele ya bosi kwamba unafaulisha Ili mwaka unaofuata upewe Tena mkataba , kwani wanafunzi wakifeli unaondolewa kazini,
kazi za walimu wengi katika shule za binafsi ni za mwaka mmoja mmoja
Hili jambo limesababisha wanafunzi wanasoma muda wote hakuna likizo watoto wanasoma mpaka usiku wamekaa madarasani TU
Wakati watoto wanatakiwa baada ya muda wa masomo wasome kwa kufanya activities zinazohusiana na masomo waliyosoma darasani

BARAZA LA MITIHANI TANZANIA
Baraza la mitihani linachangia sana kuua elimu ya nchii yetu katika nyanja zifuatavyo

1. Namna wanavyopima wanafunzi na kutoa majibu. Kuwe na upimaji mwingine wa watoto katika uwezo (skills) wao mwingine kama sanaa, uchoraji, kujieleza ,kushona ,kupika, mapambo, muziki, uongozi, uaminifu,nk
Nakumbuka wakati nasoma kulikuwa na masomi ya cookery, fineart, music ,nnedle work na yalikuwa yanapimwa kitaifa na mtu anapata marks kwenye cheti chake

2. Utungaji wa mitihani sio mzuri, kuna baadhi ya topics au sub topics huwa haziguswi kabisa kwa miakana miaka

Au siku swali likitoka basil litatoka swali la ssction A hii inafanya walimu na wanafunzi kupredict maswali na walimu wanawaambia kabisa watoto usihangaike kusoma hiyo topic haitoki.

Sasa kwa nini hiyo topic iwwpo kwenye mtaala?Sasa elimu sio kusolve past papers, elimu inatakiwa ikukomboe kama mtu amesoma kuhusu magonjwa basil atumie elimu yake kujikinga na magonjwa na sio kujibu mtihani
Utungaji wa mtihani wa darasa la saba ni mbovu kabisa. Hivi kweli mwanafunzi wa darasa la saba anajibu maswali 45 ya kuchagua TU?

Mtoto anashindwa kujieleza kwenye mtihani?Hili inachangia sana wizi wa mitihani kwani mtoto anakaririshwa majibu yote ya kuchagua au mwalimu anakaa chooni anawapa watoto majibu kwani majibu yote ni ya kuchagua

3. Baraza linapotoa majibu na kueleza shule kumi bora za kwanza nafikiri kuwe na shule kumi bora katika skills mbalimbali hvyo tutapata makundi mbalimbali ya shule kumi bora , tunawwza kuwa na makundi ya shule kumi bora katika sayansi, sanaa, hesabu nk

4. Baraza linaweza likasimamia uandaaji wa mitihani lakini kila mkoa ukawa na mtihani wake Mambo ya mtihani wa taifa yafutwe

5. Kwa miaka zaidi 30 nimeona kuna mapungufu sana katika utungaji wa mitihani ya vitendo katika masomo ya sayansi, kuna topics ni lazima Itoke Kila mwaka katika masomo hayo mfano volumetric katika chemistry, mechanics katika physics na classification katika biology sijaqahi kujua hasa kwa Nini topics hzo ni compulsory katika mitihani ya taifa Hivi kweli Baraza la mitihani limeshindwa kabisa kabisa kuwa na practicals tofauti tofauti kutoka topics zingine? Jinsi maendeleo ya technology yanavyoenda kwa Kasi!!!

Hivi baraza limewahi kutoa elimu kwa walimu kwamba hizo practicals lazima zifanyike ili ziwasaidie watoto kwa namna gani katika maisha Yao ya Kila siku?

OFISI YA UKAGUZI AU WANAJIITA UDHIBITI UBORA
hawa wakifika mashuleni ni kukagua lesson plan za walimu , wakijitahidi sana wataingia darasan mara moja wanaandika ripoti
Mm nafikiri kuwe na zaidi ya hayo kwanza kwenye shule za serikali na binafsi

1. Kuwe na ukaguzi wa utunzaji wa vifaa vya maabara kwani niliwahi kuingia maabara ya shule Fulani yaani vitu vimetupwa tupwa ilimradi TU

2. Kuww na ukaguzi wa kazi mbalimbali za miko o za wanafunzi ambazo waliwahi kufanya

3. Kuwe na ukaguzi wa walimu wanaofundisha masomo je wamesomea masomo hayo?

4 tangu miaka na miaka wakaguzi wakija mshuleni ni kukagua lesson plan TU watamkagua na mkuu wa shule kidogo wanapewa posho zao imetoka, hebu kuwe na bamna zaidi ya ukaguzi kwa karne hii ambayo tuko

TAASISI YA UKUZAJI MITAALA
Mittala ya Tanzania kwa upande wa masomo ya sayansi ndio nitakayoizungumzia kwani ndio eneo langu

1.somo la sayansi shule ya msingi lianze darasa la kwanza

2 Kuwe na ulazima kwa mwalimu anapofundisha topic na sub topic atoe maelezo ya kina kwa Nini anafundisha hivyo sub topic
Ina umuhimu gani katika maisha ya Kila siku kwa mtoto, kwa Nini mtoto ajifunze , hyo ielezwe katika Kila syllabus na iwe katika Kila sub topic sio unamwambia mwanafunzi general importance of studying Biology huko ndani unamfundiaha brain inatakiw umwambie kwa undani kwa Nini nakufundisha kuhusiana na parts of the brain, na kazi za brain
Mfano mwingine unapomfundisha mtoto kuhusu mashairi, au hotuba mwambie anaweza kuitumia wapi elimu ya kuandika hotuba
Mtu anaweza kujiajiri kwa uandishi wa hotuba
Anaweza akawa anawaandikia wanasiasa hotuba akalipwa
Au kwenye mashairi akawa anawatungia wanamuziki mashairi ya nyimbo zao
Iwe ni lazima na TIE isimamie Hilo kikamilifu

2.Ktika mtaala wa shule ya msingi katika shule za kingereza hawaruhusiwi kufundishwa SoMo la kiswahili kwa darasa la kwanza na la pili lakini utashangaa shule zimeingiza lugha ya kichina na kifaransa na kijerumani kwa darasa la kwanza na la pili sasa SI bora watoto wetu wajifunze lugha yetu ya kiswahili

Hebu ona kiswahili kilivyoharibika siku hizi

4. Masomo ya sayansi yafundishww kwa vitendo tangu kidato Cha kwanza , practicals ziww nyingi zaidi kwani katika sayansi kila topic ina activities za kutosha sana

Kwani sayansi Iko kila sehemu
Science skills are life skills
Unapolula, unapotembea, unapopika ,unapolala, unapoimba nk vyooooooote ni sayansi
Elimu ya vitendo iwe
katika kila topic na sub topic ya sayansi

Mtaala wa sayansi shule za msingi haujitoshelezi
Hili nikianza kuongea hapa ni topic nyingine ndefu sana

6. Walimu wa sayansi kwa shule za msingi waww wamespecialize kwenye sayansig

nimewahi kushuhudia mwalimu akifundisha kitu tofauti kwa sababu hakuwa mwalimu wa sayansi na amepewa afundishe darasa la tatu, je ni watoto wangapi wamedanganywa

7 Njia za ufundishaji na upimaji zibadilishwe
Tuwapime watoto katika vitu walivyofanya na walivyobuni
Ufundishaji uwaongoze atoto katika ubunifi na sio kijibu maswali

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Isimamie walimu wapewe semina mbalimbali za mara kwa mara
Wawe karibu na walimu kujua changamoto wanazopitia
Serikali itenganishe wizara

Kuwe na wizara ya elimu ya juu na wizara ya elimu na mafinzo ya fundi

Kwa Leo naomba niishie hapa
Asanteni
 
Upvote 1
Elimu ya TANZANIA Iko kinadharia sana Kiko vitendo
Kupambana watoto wafaulu TU mtihani inachangia sana wizi wa mitihani
 
Back
Top Bottom