Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,812
- 107,628
Muziki, Muvi na series zikifutwa duniani sijui maisha yatakuaje upande wangu maana Muvi na Muzi ni vitu navyovipenda as entertainment for me...napenda sana kusikiliza muziki sidhani kama kuna siku inapita sijasikiliza muziki. Hua napenda nikilala muziki wa slow jams, flashback,afropop nyimbo za Enya ziwe zinalia. lakini kitu
kinachonishinda kusikiliza muziki usiku ni hali ya wimbo kua unaiimba kwa haraka haraka kuliko unavyolia mchana. hali hii hua inaua mood sana hasa kama ulitaka usikilize wimbo wa taratibu usiku halafu uanze kuimba in fastmode.....Natumaini wengi wenu mshaligundua hili jinsi nyimbo hua zinabadirika Tempre wakati wa usiku na kuimba haraka wakati wimbo huo huo hua unaimba taratibu wakati wa mchana
Beat Per Minute (BPM)
Sound Perception ni uwezo wa kukusanya na kutafsiri sauti, shughuli ya kukusanya sauti hufanywa na sikio la nje (Pina) na shughuli ya kutafsiri sauti hufanywa na ubongo. kama milango ya fahamu mingine ilivyo sikio pia hua haitambui ni kitu gani imekusanya inachojua yenyewe imeyakusanya mawaimbi ya sauti na kuyapeleka kwenye ubongo kupitia sikio la kati na sikio la ndani (choclea & Drum?), hivyo basi ubongo kazi yake ni kubadiri mawimbi ya sauti yawe taarifa za kiumeme (electrical signal) form 3 tuliita Impulses.
Ni kweli kabisa kisayansi muziki hua una tabia ya kubdirika tempre/speed yake wakati wa usiku, lakini sio kiuhalisia kabisa kwamba tempre hua imebadirika hapana hua iko vile vile 1x per minute. kuna sababu kadhaa hufanya muziki kusikilizika hivyo
Jotoridi (Temperature)
Mawimbi ya sauti husafiri taratibu taratibu kwenye baridi kuliko wakati wa baridi sababu molecules husafiri haraka wakati huo hivyo kufanya wimbo uende kwa kasi. Mind you sio kwamba wimbo ndio hua unaenda kasi hapana ni mawimbo ya sauti ndio huenda kasi lakini huko kwenye simu au redio wimbo uko vilevile. kama mtakumbuka tulisoma factor affecting Waaves/Sound Propagation. kama bado una notices unaweza kujisomea zaid
Time Perception
Masikio yangu hua nahisi yanasikia zaidi nikiwa nimelala kuliko nikiwa macho ndio maana napenda kusikiliza muziki nikiwa nimesinzia maana hua nasikia ukiimba, hata nilale vipi kama utaniita lazima nikusikie. wanasayansi wanasema kwamba ubongo wako hua ni upo makini zaidi (alert) wakati wa usiku hivyo basi ubongo husikiliza sauti ya kila kitakachopita ndio maana unaweza kusikiliza sauti ya kitu kilicho mbali zaidi wakati wa mchana.
Mapigo ya moyo
kama unakimbia au au unatembea haraka ukiwa umevaa earphones hata kama wimbo ulikua taratibu utasikia unaenda haraka kadri ya unavyokimbia, utaona kabisa unaenda na hatua zako unazopiga wakati wa kukimbia lakini wimbo huohuo ukiusikiliza ukiwa umetulia utasikia uanenda haraka ni kwasababu muziki pia hua unatabia ya kubadirika kutokana na kasi ya mapigo yako ya moyo.
Dihydroxyphethylamine
Ni kemikali/homoni inayozalishwa katika ubongo wa katikati kisha kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya ubongo, kwa lugha rahisi kemikali hii huitwa Dapomine. Kazi yake ni kuhamasisha mwili uendelee kufanya jambo ambalo linaupa mwili raha kama vile kula au kufanya mapenzi, kemikali hii ikipungua mwilini husababisha mtu kukosa hamu ya kutenda mambo kadhaa kama kufanya mapenzi, Kula, Kulala, kufurahi nk.
Kama unakua huna usingizi au huna hamu ya kula basi unaweza kutumia kemikali hii kukuongezea hamu kwa kuongeza kiwango cha uzalishwaji wake mwilini mwako. Unaweza kuiongeza mwilini kutumia njia zifuatazo.
Muziki
Tafiti zinaonyesha kwamba kusikiliza nyimbo unazozipenda husaidia Dapomine kuongezeka kwa 9%,Wanasayansi wanashauri kama libido yako ipochini basi sikiliza nyimbo uzipendazo hii itakusaidia kuongeza hamu zaidi ya kufanya Sex..Chakula cha kwemye sherehe hua kinakua kitamu sababu ya muziki wa taratibu unaokua unapigwa wakati wa kula.
NB: Be warned! Tabia ya kusikiliza muziki ukiwa sehemu na babe wako au kushea nae nyimbo ni nzuri sana ila mambo yakiharibika utajua hujui. Kila nyimbo utayoisikiliza itakua inakukumbusha moments ulizokua nae somewhere! Inauma, utazichukia nyimbo uzipendazo bure😟😂