Sababu zinazoifanya Tanzania isiathiriwe sana na vimbunga

Kimbunga ni upepo unaozunguka kiini chenye mgandamizo Mdogo kinyume cha saa upande wa Kaskazini wa Dunia na kama saa upande wa kusini wa Dunia. Mantiki ya mzunguko hapa inajengwa na namna mshale wa saa unavyozunguka.

Upepo huu huongeza mwendokasi wake kadiri unavyozunguka. Inakadiriwa mwendokasi unaweza kufikia kilomita 150 kwa saa. Vimbunga katika ukanda wa kitropiki vinaweza kuendelea kuanzia masaa kadhaa mpaka wiki mbili. Wastani wa muda wa uhai wa kimbunga ni siku sita.

Bahari ni chanzo muhimu sana cha nguvu za vimbunga kwa kupitia njia ya kuzalisha joto katika nyuso zake " joto hisi" na pia kufukiza kwa maji. Joto hili na mvuke wa maji hugandamanishwa na kuzalisha "joto fiche".

Vimbunga vinaposafiri kuelekea Nchi kavu hupoteza joto fiche na hivyo mzunguko wake kudhohofika mara dufu.

Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazopitiwa na vimbunga mara chache sana kutokana na ukaribu wake na ukanda wa Kiikweta ambapo kani inayosukuma mzunguko wa hewa iitwayo Coriol ni ndogo mno. Hali hii huvifanya vimbunga kukosa nguvu ya kuzunguka zaidi na hivyo madhara huwa ni madogo.

Nguvu ya Coriol ni kani ya kufikirika inayoelezea mpindo wa vitu vinapotembea katika latitude ukiwianisha na kuviangalia city hivyo katika Dunia.

Tanzania inapaswa kuendelea kuchukua tahadhari kubwa hususani katika suala zima la kupunguza uchafuzi wa maji ya bahari ili kupunguza mazingira ya kuzaliwa kwa vimbunga au kuviongezea nguvu

Mwl. Mlaki
Geog dept, 2021
Utapanda daraja???
 
Mwendazake angekuwepo ...Angesema kijana jobo Ni beberu
Pia mwendazake angekuwepo,ungewasikia mapimbi kama akina msiba wanasema "tunashukuru sana serikali ya awamu ya tano ya Dr.John Joseph Pombe Magufuri,kimbunga hakikutokea"
 
MkuuMkuu tunaongelea matukioa ya kijiografia siyo haya unayoyaleta humu.
Pia mwendazake angekuwepo,ungewasikia mapimbi kama akina msiba wanasema "tunashukuru sana serikali ya awamu ya tano ya Dr.John Joseph Pombe Magufuri,kimbunga hakikutokea"
 
Kimbunga ni upepo unaozunguka kiini chenye mgandamizo Mdogo kinyume cha saa upande wa Kaskazini wa Dunia na kama saa upande wa kusini wa Dunia. Mantiki ya mzunguko hapa inajengwa na namna mshale wa saa unavyozunguka.

Upepo huu huongeza mwendokasi wake kadiri unavyozunguka. Inakadiriwa mwendokasi unaweza kufikia kilomita 150 kwa saa. Vimbunga katika ukanda wa kitropiki vinaweza kuendelea kuanzia masaa kadhaa mpaka wiki mbili. Wastani wa muda wa uhai wa kimbunga ni siku sita.

Bahari ni chanzo muhimu sana cha nguvu za vimbunga kwa kupitia njia ya kuzalisha joto katika nyuso zake " joto hisi" na pia kufukiza kwa maji. Joto hili na mvuke wa maji hugandamanishwa na kuzalisha "joto fiche".

Vimbunga vinaposafiri kuelekea Nchi kavu hupoteza joto fiche na hivyo mzunguko wake kudhohofika mara dufu.

Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazopitiwa na vimbunga mara chache sana kutokana na ukaribu wake na ukanda wa Kiikweta ambapo kani inayosukuma mzunguko wa hewa iitwayo Coriol ni ndogo mno. Hali hii huvifanya vimbunga kukosa nguvu ya kuzunguka zaidi na hivyo madhara huwa ni madogo.

Nguvu ya Coriol ni kani ya kufikirika inayoelezea mpindo wa vitu vinapotembea katika latitudo ukiwianisha na kuviangalia vitu hivyo katika Dunia. Kwa mfano ndege inapopaa ikiwa upande wa Kusini wa Ikweta huenda juu lakini si katika mstari mnyoofu ila kwa kupinda uelekeo kidogo kuelekea kushoto.

Tanzania inapaswa kuendelea kuchukua tahadhari kubwa hususani katika suala zima la kupunguza uchafuzi wa maji ya bahari ili kupunguza mazingira ya kuzaliwa kwa vimbunga au kuviongezea nguvu

Mwl. Mlaki
Geog dept, 2021
Kishki amesema Jobo imeondoka sababu ya Dua ya Jana uwanja wa taifa
 
Haya mambo kilamtu anayaangalia kwa kutumia muono tofauti, muono wake ni tofauti na wangu tunaweza tukatofautiana katika kuelezea kitu kilekile.

Back
Top Bottom