Sababu zinazopelekea Jasusi (Spy) kuisaliti nchi yake

Sababu zinazopelekea Jasusi (Spy) kuisaliti nchi yake

mngony

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
5,555
Reaction score
6,972
Jasusi ni mtu anayechukua au kukusanya taarifa za nchi nyingine zinazochukuliwa kuwa ni siri bila ya ruhusa. Kwa upande wa anakopeleka taarifa hizo huwa ni faida lakini kwa upande anakozichukua huwa ni hasara kulingana na taarifa ziilizochukuliwa.

Jasusi huyo anaweza kuwa wakigeni, yaani kutoka nje ya nchi au wanyumbani yaani wa nchi husika ambaye hugeuka kuwa Double agent na huyu ndio huwa hatari zaidi hasa anapokuwa katika nafasi ambazo zinamuwezesha kuzipata taarifa mbalimbali kwani anakuwa ameaminiwa na huwa vigumu kumgundua japo hupatikana kulingana na ubora wa counter-intelligence measures za nchi husika, lakini kama hakuna tips au viashiria vyovyote kumgundua mwingine anaweza hadi kufa au kustaafu na asijulikane.

Tabia ya majasusi kuiba siri za nchi nyingine ni sehemu ya maisha yenyewe ya ujasusi, jinsi gani upo smart kupata taarifa za mwenzako either adui, au jirani au mshindani ndio jinsi utakavyokuwa bora.

Hawa double agent wanapatikana kwa kuwa spotted na maadui kwa kuchunguzwa vizuri na kisha kufuatwa au wenyewe ku-offer service kwa kujipeleka kwa sababu mbalimbali. Sehemu nyingie ambazo hawa double agent hupatikana ni pale nchi zetu zinazoendelea zinavyopeleka watu wetu nje kupata mafunzo zaidi kama vile MAREKANI, UINGEREZA n.k kwa vile wao ndio wanaendesha mafunzo ni rahisi kuwa-spot wale ambao ni the best kisha kuwa-approach wakijua watakuja kupata nafasi nzuri na nyeti sana katika taasisi zetu.

Hawa wa nje wapo tu hawazuliki, wengine wafanyabiashara, wanafunzi, wanadiplomasia, kwenye mashirika ya kimataifa, NGO's n.k. hakuna jinsi ya kuwazuia wakija kwa njia hii suala huwa ni kulimit tu wasipate taarifa za ndani, hawa wanaweza kupata taarifa za kawaida kupitia vyanzo vya wazi kama kupitia mitandao, magazeti, midahalo, bunge, n.k mfano yanayoendelea sasa kuhusu mijadala ya muungano wetu n.k ni wazi yanajulikana tu.

Sasa hawa wa ndani, ambao huigeuka nchi yao na kuisaliti kwa kutoa siri ndio hatari zaidi kulingana na nafasi aliyopo, kiasi cha muda wa usaliti wake na uwezo wake wa kujificha asijulikane. Hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea jasusi kuisaliti nchi yake.

1.PESA
Hii ndio motivating factor kubwa kabisa ya jasusi kuisaliti nchi yake kwa nchi nyingine, ndio maana hawa jamaa hulipwa vizuri kadri inavyowezekana. Sasa ikitokea either haridhiki na anachokipata kwa sababu zake binafsi kama vile kutaka kuishi maisha ya gharama au tu anahisi mshahara haumtoshelezi hivyo wakitokea watu wakamuahidi kiasi kikubwa cha pesa anaona atoe siri apate hizo pesa. Mfano ni jamaa mmoja John Walker alikuwa mtaalamu wa mawasiliano mwenye cheo cha Warrant Officer katika jeshi la maji la Marekani ambaye alipatikana na hatia ya ku-spy kwa ajili ya Soviet( Russia ya zamani) kuanzia mwaka 1968-1985. Motive yake ilikuwa pesa kwani alikuwa na matatizo ya kiuchumi.

2. MTIZAMO, UZALENDO,IMANI NA UTAMADUNI

Kutofautiana kimtazamo na either jinsi nchi inavyoongozwa au sera zinazoongoza nchi mfano Kim Philby alikuwa agent wa shirika la kijasusi la uingereza MI6 aliamua ku-spy kwa ajili Soviet union kwa kuwa alikuwa akiamini katika ukomunist, mwingine ni Fritz Kolbe alikuwa mwanadiplomasia katika wizara ya mambo ya nje ya ujerumani, aliamua ku-spy kwa ajili ya wamarekani katika vita ya pili ya dunia kwa kuwa hakukubalina na sera za u-nazi.

Jonathan Pollard mmarekani mwenye asili ya uyahudi aliamua kuiba siri kuhusu jeshi la marekani kuzipeleka Israel akiwa katika kitengo cha intelijensia ya jeshi mwaka 1987, alipewa kifungo cha maisha ila anatarajiwa kutolewa mwakani.

Pia hii ya uzalendo, imani na utamaduni ndio silaha kubwa iliyotumiwa na Isreal kupata majasusi wengi katika nchi nyingi maadui zake hasa nchi za kiarabu ambao walikuwa wakipeleka taarifa na ikawa moja ya sababu ya kushinda kwa urahisi kabisa vita vile vya siku sita, kwani wahusika walijihisi wayahudi zaidi kuliko utaifa wa mataifa waliyozaliwa na ndio sababu pia Israel ilikuwa ikiwachunguza sana waisrael waarabu kiasi cha kutengeneza kikosi maalum kilichopelekwa kujipenyeza katika jamii hizo za kiarabu, japo ni raia waisreal lakini walihofiwa kutumiwa na mataifa ya kiarabu kutokana na uarabu wao.

Nadhani ndio maana kipindi fulani tulikuwa na uhusiano wa kusuasua na nchi moja jirani watu walianza kuhoji wale wenye asili ya huko walio sehemu nyeti kama ikulu, ni kwa sababu kama hii.

3.KULAZIMISHWA KWA KUTISHWA
Kutishiwa maisha ya familia yake au uhai wake, akaambiwa alete taarifa au siri juu jambo fulani ili yeye au familia iwe salama. Au una siri fulani ambayo hutaki Mwajiri wako(Shirika lako la kijasusi) aijue na inawezekana wakiijua ajira imekwisha, unaamwa tuoe tasrifa kuhusu kitu fulani, ukishapeleka tu wanaweza kusema uendelee kuwaletea usipofanya hivyo watatoa siri kuwa ulifanya uhaini kwa kuwaletea siri pale mwanzo inakuwa ndo tayari maisha yako u double agent. mfano Mathilde Carre alikuwa member wa french resistance waliokuwa wakipambana ufaransa dhidi ya uvamizi wa wa-nazi wakati wa vita ya pili ya dunia alikamatwa na nazi wamtishia maisha na akatakiwa akachukue taarifa awaletee wao. Akakubalia akawa anawaletea taarifa kwa ajili ya kuhofia vitisho vyao

4.KUTOKUTHAMINIWA
Inaweza kujitokeza pale mtu anajihisi anafanya kazi nzuri na kubwa akihitaji kuthaminiwa lakini hawi appreciated akionekana mtu mdogo tu wa kawaida, huku yeye akijiona bora kuliko wanaomzunguka na amekuwa akifanya makubwa. Anaweza kuamua kwenda kwa mshindani ku-offer his service. mfano ni Robert Hanssen, alikuwa agent wa FBI akaamua ku-spy kwa ajili ya Warusi kuanzia mwaka 1979-2001 alijion hapewi thamani a kuchukuliwa umuhimu kwa kazi aliyokuwa akifanya(aliona anafaya makubwa lakii anaonekana mdogo). Alikuwa Arrogant sana na ni katika doube agent aliyeiumiza sana marekani kwa kuiba siri nyingi na kupeleka Urusi, mfano kipindi hicho Warusi walijua siri nyingi za kijeshi kiasi kama wangeingia vitani basi ilikuwa shughuli nzito sana kwa marekani, warusi walijua kila submarine ya marekani ilipo.

Karibuni kwa michango
 
Mada nzuri sana hii ! CIA wanatabia ya kutumia hela kukufanya uisaliti nchi yako.Wanaweza kukuambia uwe double agent afu wanakujengea nyumba Mbezi Beach

Watu hatari sana wale

ndio hivo unakuta anachoahidiwa ni zaidi ya mara 10 ya kile anachopewa kwa mwezi tena anapewa kwa wiki. na uaambiwa sisi tunataka tu kujua kinachoendelea mtu anakubali
 
Dah,nimemkumbuka Double Agent wa Ukweli Robert Hanssen jina la Ujasusi Bob Hanssen ambae kwa sasa anatamikia kifungo cha Maisha Jela without Parole huko Marekani alichohukumiwa 2001.

Jamaa alikuwa Jasusi wa F.B.I but ilipofika Mwaka 1986 akaanza kuwa Double Agent wa K.G.B USSR ya zamani for Money motives mpaka pale alipokamatwa 2001, lakini cha kushangaza na kustajaabisha sasa jamaa wa K.G.B walikuwa hawamfahamu kwa kumuona kwa sura wala kujua jina lake halisi hata siku moja mpaka pale alipokamatwa Mwaka 2001 ndio wakafahamu Mtu aliekuwa anawapa taarifa, na huyu ndio alietoa siri za ile Tunnel ya C.I.A waliyochimba kwa ajili ya kuchukua siri/taarifa chini ya Ubalozi wa USSR Jijini Washngton DC.
 
Dah,nimemkumbuka Double Agent wa Ukweli Robert Hanssen jina la Ujasusi Bob Hanssen ambae kwa sasa anatamikia kifungo cha Maisha Jela without Parole huko Marekani alichohukumiwa 2001. Jamaa alikuwa Jasusi wa F.B.I but ilipofika Mwaka 1986 akaanza kuwa Double Agent wa K.G.B USSR ya zamani for Money motives mpaka pale alipokamatwa 2001,lakini cha kushangaza na kustajaabisha sasa jamaa wa K.G.B walikuwa hawamfahamu kwa kumuona kwa sura wala kujua jina lake halisi hata siku moja mpaka pale alipokamatwa Mwaka 2001 ndio wakafahamu Mtu aliekuwa anawapa taarifa,na huyu ndio alietoa siri za ile Tunnel ya C.I.A waliyochimba kwa ajili ya kuchukua siri/taarifa chini ya Ubalozi wa USSR Jijini Washngton DC.

wanasema alikuwa akilipwa vizuri tu, ila he was so arrogant..alijihisi ni bora zaidi na mchango wake kama vile hauthaminiwi, japo alifurahia pesa alizokuwa akipewa na alipoulizwa alitaja motivation yake ni pesa. alitumia Ramon Garcia kuwaliana na contacts wake
 
wanasema alikuwa aikilipwa vizuri tu, ila he was arrogant..alijihisi ni bora zaidi na mchango wake hauthaminiwi japo alifurahia pesa alizokuwa akipewa na alipoulizwa alitaja motivation ya pesa. alitumia Ramon Garcia kuwaliana na contacts wake

Yap,huyu Jamaa mpaka leo simpatii picha kabisa hasa kwenye issue yake ya Ndoa sababu wakati alipokuwa anafanya Mapenzi na Mke wake alikuwa anachukua Video kwa siri bila Mke wake kujua then akiwa Ofisini au na Marafiki zake anawaonyesha Video nzima akifanya mapenzi yeye na Mke wake
 
Kama Pesa ni kigezo kikubwa, sijui majasusi wa nchi yetu wapo katika hali gani!! nadhani wao wanaongoza kwa kuwa double agents.

wengine watiifu na wazalendo, sidhani km wote hukubali wengne hukataa.
 
Kwa hiyo mtoa wazo unalenga nini? Unawataka watanzania kuwa Double Agent? Mafunzo mengine ni ya JANDONI KABISA SIO KILA MAHALI.
 
Kwa hiyo mtoa wazo unalenga nini? Unawataka watanzania kuwa Double Agent? Mafunzo mengine ni ya JANDONI KABISA SIO KILA MAHALI.

sina lengo baya, mimi naipenda nchi yangu. Nimeleta tu mada ku-share kama ambavyo zinaletwa mada zingine. Lengo ni ku-share tu,kuna wasiojua, wanaojua kiasi na wanaojua sana! Ni mjadala wa kawaida tu hakuna cha ajabu, hata ukienda kwenye vitabu, mitandaoni unapata ipogolo
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuongezea, kiujumla kuna scenario mbili za double agents,

Ya kwanza
kuna yule ambaye anajulikana yupo katika agency X na yuko loyal kwa agency X, ila anakuja kutokea agency Y na kumshawishi awape taarifa wao kwa sababu kama alizozitoa mleta mada (pesa, Sifa n.k). Hii huwa ni rahisi kwa mhusika kwani anakuwa huru kiasi fulani katika kuuza ama kupitisha taarifa zake kwa agency Y.


Ya pili
Hii inakuwa ni kwa wale maagent wanaokuwa katika agency X na anapretend kuwa yupo na X katika kila jambo wakati kiuhalisia yupo loyal na agency Y na anavujisha taarifa za X kwa Y bila X kujua. Hii aproach ni ngumu na inabidi ifanywe kwa ustadi mkubwa sana as agant huyu anakuwa hatarini sana katika kumaintain cover yake.

Ili kufanikisha hili kuna agency hufikia hata kurecruit/kupandikiza agents tokea wakiwa wadogo katika nchi ambazo wanataka kuvuna taarifa. Ili kufanikisha cover ups, kuna wakati taarifa zilizovunwa na undercover agent zinaweza zisitumiwe ili tuu coverup ya agent wao isigundulike huku wakizihifadhi taarifa hizo kwa matumizi ya baadae.
 
Kama Pesa ni kigezo kikubwa, sijui majasusi wa nchi yetu wapo katika hali gani!! nadhani wao wanaongoza kwa kuwa double agents.

Sio suala la pesa tu kama rushwa ya barabarani kuna kuchungwa na kufuatiliwa mienendo kwa hali ya juu kabisa!

Adhabu yake iko wazi kabisaaa so ku trade maisha na kukiuka kiapo sio jambo dogo pia!!!! Haswa kwa anayefahamu consequences just in case...

Kumbuka Rais wa nchi jirani katoa salamu gani kwa wasaliti wake? Sasa imagine hadharani kasema hivyo,covert part ikoje?

Kuna mmoja alihisiwa tu anavujisha alikiwa jeshini nchi fulani ,advertise ya kwanza aliuliwa mkewe na kupigiwa simu aseme kalikisha file gani na kwa nchi gani? Kwa kuwa hakuwa amefanya ilibidi ampeleke mwanaye kituo cha polisi say (Oysterbay) akamtelekeza hapo kwa usalama naye akaenda mji mwingine say Arusha na kujisalimisha polisi akaeleza kila kitu isipokuwa tu kazi yake (ya ndani)!!!

Na kusisitiza kuwa kaenda kusalimisha uhai wake sababu akiwa nje ya pale atakufa tu iwavyo vyovyote!!!

So pamoja na donge nono,hatari yake ni zaidi ya hatari!
 
Sababu yaku saliti kubwa sana ni kutokwajibika kwa Agency Administrators, Kanda za Africa kuchaguliwa kwajasusi (selection of operatives) ufatilia mkondo wakifisadi (corruption i.e nepotism etc).

Sasa hawa jama serve themselves not there repective country's
 
Kwa kuongezea, kiujumla kuna scenario mbili za double agents,

Ya kwanza
kuna yule ambaye anajulikana yupo katika agency X na yuko loyal kwa agency X, ila anakuja kutokea agency Y na kumshawishi awape taarifa wao kwa sababu kama alizozitoa mleta mada (pesa, Sifa n.k). Hii huwa ni rahisi kwa mhusika kwani anakuwa huru kiasi fulani katika kuuza ama kupitisha taarifa zake kwa agency Y.


Ya pili
Hii inakuwa ni kwa wale maagent wanaokuwa katika agency X na anapretend kuwa yupo na X katika kila jambo wakati kiuhalisia yupo loyal na agency Y na anavujisha taarifa za X kwa Y bila X kujua. Hii aproach ni ngumu na inabidi ifanywe kwa ustadi mkubwa sana as agant huyu anakuwa hatarini sana katika kumaintain cover yake.

Ili kufanikisha hili kuna agency hufikia hata kurecruit/kupandikiza agents tokea wakiwa wadogo katika nchi ambazo wanataka kuvuna taarifa. Ili kufanikisha cover ups, kuna wakati taarifa zilizovunwa na undercover agent zinaweza zisitumiwe ili tuu coverup ya agent wao isigundulike huku wakizihifadhi taarifa hizo kwa matumizi ya baadae.

ahsante mkuu, nimejfunza kitu kutoka kwako. Ila kumhandle double agent ni sensitive sana kwa sbb mda wowote royalty yake inaweza kubadilika na asijulikane. Hasa km huko watamgundua, anaweza kupewa wrong information azifeed
 
Sio suala la pesa tu kama rushwa ya barabarani kuna kuchungwa na kufuatiliwa mienendo kwa hali ya juu kabisa!!!!

Adhabu yake iko wazi kabisaaa so ku trade maisha na kukiuka kiapo sio jambo dogo pia!!!! Haswa kwa anayefahamu consequences just in case...

Kumbuka Rais wa nchi jirani katoa salamu gani kwa wasaliti wake???!!! Sasa imagine hadharani kasema hivyo,covert part ikoje???!!!!

Kuna mmoja alihisiwa tu anavujisha alikiwa jeshini nchi fulani ,advertise ya kwanza aliuliwa mkewe na kupigiwa simu aseme kalikisha file gani na kwa nchi gani?!! Kwa kuwa hakuwa amefanya ilibidi ampeleke mwanaye kituo cha polisi say (Oysterbay) akamtelekeza hapo kwa usalama naye akaenda mji mwingine say Arusha na kujisalimisha polisi akaeleza kila kitu isipokuwa tu kazi yake (ya ndani)!!!

Na kusisitiza kuwa kaenda kusalimisha uhai wake sababu akiwa nje ya pale atakufa tu iwavyo vyovyote!!!

So pamoja na donge nono,hatari yake ni zaidi ya hatari!!!!!

aiseeni zaidi ya hatari, unatembea kulia kwako hela kushoto kifo. vip kuhusu kubalishana wafungwa wa kijasusi ipo hapa kwetu? unakuta tumemkamata wa nchi fulani ila kwa kuwa kutoka nchi hiyo tuna wa kwetu tunaamua kubadilishana, tunamrudisha wa kwao wanamrudisha wa kwetu
 
Back
Top Bottom