Sababu zinazopelekea Jasusi (Spy) kuisaliti nchi yake

Nilipata kufadhiliwa na mfuko fulani wa maendeleo ya watu wa Nchi fulani ya magharibi kusoma kozi fupi.....wakati wa weekend wanatuchukua na kututembeza sehemu mbalimbali na kutupa starehe za kila aina kama vile Disko, Ulabu, dada poa na kadha wa kadha yote hayo mbantu mie sikupenda...........Muda mchache kabla ya kuondoka walitoa vyeti vya ziada (kwa maana ya Tabia)....Mimi walikomment ati Looks like AGENT nilishangaa sana na nikaamua kukiacha Hotelini nikiwa nimekichana.........Nilipo safiri kurudi TZ nikiwa Nchi fulani karibu niache na Ndege ya kuja TZ kwani nilizuiwa nikiwa na mdada wa kidhungu ambaye machoni pangu nilimuona kama Agent wakapekuwa begi la yule dada akaruhusiwa ikaingia zamu yangu......walipekua zaidi ya mara 4 bila ya kunieleza wanatafuta nini?.......Hatimaye nami wakaniachia.........Nikahisi walikuwa wanatafuta kile cheti aaaaaahhh ilikula kwao........

ulipishana na hela kichwa nazi
 
Kuna nyakati Jasusi anatoa siri za Nchi au taasisi bila kujua. Inaweza kuwa kwa ushawishi usiokuwa wa moja kwa moja au bahati mbaya tu!

Imetokea mahali Watu watano wamekaa wakipiga story na kunywa bia. Wawili kati yao ni 'Undercover spies' wa Nchi fulani, mmoja ni rafiki wa karibu wa hao wawili akiwajua kwa kazi yao inayofahamika na siyo ile haswaa, mwingine ni Raia lakini akiwa 'maamuma tu kwenye maongezi. Huyo mmoja aliyebakia ndiye mlengwa, yeye ni Jasusi wa Nchi X, hao 'Undercover' wanajua kabisa wapo na Mtu gani na nini wanachokitaka toka kwake.

Kadri flow ya mazungumzo inavyokwenda ndivyo wanavyoanza kuchimba, kwa bahati mbaya sana kwao ni kuwa pamoja na kwamba walikuwa makini kupata taarifa lakini walikosea kitu kidogo tu, walizidisha 'umakini' wakati wa mazungumzo. Jasusi X kengele ikaanza kulia kichwani, 'why katika hali hii ya unywaji hawa watu wawili wapo makini sana katika baadhi sehemu za mazungumzo?'

Jamaa najua mpaka leo wnajing'ata vidole kwa kosa la kiufundi walilolifanya.
 
Dah,nimemkumbuka Double Agent wa Ukweli Robert Hanssen jina la Ujasusi Bob Hanssen ambae kwa sasa anatamikia kifungo cha Maisha Jela without Parole huko Marekani alichohukumiwa 2001. Jamaa alikuwa Jasusi wa F.B.I but ilipofika Mwaka 1986 akaanza kuwa Double Agent wa K.G.B USSR ya zamani for Money motives mpaka pale alipokamatwa 2001,lakini cha kushangaza na kustajaabisha sasa jamaa wa K.G.B walikuwa hawamfahamu kwa kumuona kwa sura wala kujua jina lake halisi hata siku moja mpaka pale alipokamatwa Mwaka 2001 ndio wakafahamu Mtu aliekuwa anawapa taarifa,na huyu ndio alietoa siri za ile Tunnel ya C.I.A waliyochimba kwa ajili ya kuchukua siri/taarifa chini ya Ubalozi wa USSR Jijini Washngton DC.
Wamarekani walishangaa sana jinsi siri za tunnel ya cia zilivyojulikana
 
You are very pro active, that's why you LOOK LIKE AGENT!!
Mkuu ilitokea tu It was self-initiated and change-oriented behavior in situations only, ni swala la Logic tu kile Cheti kingenisaidia nini? na ningekipeleka wapi?......
 
Mada nzuri sana hii ! CIA wanatabia ya kutumia hela kukufanya uisaliti nchi yako.Wanaweza kukuambia uwe double agent afu wanakujengea nyumba Mbezi Beach

Watu hatari sana wale
.....and how did the Russians manage to convince Edward Snowden to defect?
 
Jasusi ni mtu anayechukua au kukusanya taarifa za nchi nyingine zinazochukuliwa kuwa ni siri bila ya ruhusa. kwa upande wa anakopeleka taarifa hizo huwa ni faida lakini kwa upande anakozichukua huwa ni hasara kulingana na taarifa ziilizochukuliwa.

Jasusi huyo anaweza kuwa wakigeni, yani kutoka nje ya nchi au wanyumbani yani wa nchi husika ambaye hugeuka kuwa Double agent na huyu ndio huwa hatari zaidi hasa anapokuwa katika nafasi ambazo zinamuwezesha kuzipata taarifa mbalimbali kwani anakuwa ameaminiwa na huwa vigumu kumgundua japo hupatikana kulingana na ubora wa counter-intelligence measures za nchi husika,lakini kama hakuna tips au viashiria vyovyote kumgundua mwingine anaweza hadi kufa au kustaafu na asijulikane. tabia ya majasusi kuiba siri za nchi nyingine ni sehemu ya maisha yenyewe ya ujasusi, jinsi gani upo smart kupata taarifa za mwenzako either adui, au jirani au mshindani ndio jinsi utakavyokuwa bora.

hawa double agent wanapatikana kwa kuwa spotted na maadui kwa kuchunguzwa vizuri na kisha kufuatwa au wenyewe ku-offer service kwa kujipeleka kwa sababu mbalimbali. sehemu nyingie mabao hawa double agent hupatikana ni pale nchi zetu zinazoendelea zinavyopeleka atu wetu nje kupata mafunzo zaidi kama vile MAREKANI, UINGEREZA n.k kwa vile wao ndio wanaendesha mafunzo ni rahisi kuwa-spot wale ambao ni the best kisha kuwa-approach wakijua watakuja kupata nafasi nzuri na nyeti sana katika taasisi zetu

hawa wa nje wapo tu hawazuliki, wengine wafanya biashara, wanafunzi, wanadiplomasia, kwenye mashirika ya kimataifa, NGO's n.k. hakuna jinsi ya kuwazuia wakija kwa njia hii suala huwa ni kulimit tu wasipate taarifa za ndani, hawa wanaweza kupata taarifa za kawaida kupitia vyanzo vya wazi kama kupitia mitandao, magazeti,midahalo, bunge, n.k mfano yanayoendelea sasa kuhusu mijadala ya muungano wetu n.k ni wazi yanajulikana tu.

sasa hawa wa ndani, ambao huigeuka nchi yao na kuisaliati kwa kutoa siri ndio hatari zaidi kulingana na nafasi aliyopo,kiasi cha mda wa usaliti wake na uwezo wake wa kujificha asijulikane. hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea jasusi kuisaliti nchi yake.

1.PESA
Hii ndio motivating factor kubwa kabisa ya jasusi kuisaliti nchi yake kwa nchi nyingine,ndio maana hawa jamaa hulipwa vizuri kadri inavyowezekana. sasa ikitokea either haridhiki na anachokipata kwa sababu zake binafsi kama vile kutaka kuishi maisha ya gharama au tu anahisi mshahara haumtosholezi hivyo wakitokea watu wakumuahidi kiasi kikubwa cha pesa anaona atoe siri apate hizo pesa. mfano ni jamaa mmoja John Walker alikuwa mtaalamu wa mawasiliano mwenye cheo cha Warrant Officer katika jeshi maji la marekani ambaye alipatakana na hatia ya ku-spy kwa ajili ya soviet( Russia ya zamani) kuanzia mwaka 1968-1985. Motive yake ilikuwa pesa kwani alikuwa na matatizo ya kiuchumi.

2. MTIZAMO, UZALENDO,IMANI NA UTAMADUNI
kutofautiana kimtazamo na either jinsi nchi inavyoongozwa au sera zinazoongoza nchi mfano Kim Philby alikuwa agent wa shirika la kijasusi la uingereza MI6 aliamua ku-spy kwa ajili Soviet union kwa kuwa alikuwa akiamini katika ukomunist, mwingine ni Fritz Kolbe alikuwa mwanadiplomasia katika wizara ya mambo ya nje ya ujerumani, aliamua ku-spy kwa ajili ya wamarekani katika vita ya pili ya dunia kwa kuwa hakukubalina na sera za u-nazi.

Jonathan Pollard mmarekani mwenye asili ya uyahudi aliamua kuiba siri kuhusu jeshi la marekani kuzipeleka Israel akiwa katika kitengo cha intelijensia ya jeshi mwaka 1987 . alipewa kifungo cha maisha ila natarajiwa kutolewa mwakani.

pia hii ya uzalendo, imani na utamaduni ndio silaha kubwa iliyotumiwa na Isreal kupata majasusi wengi katika nchi nyingi maadui zake hasa nchi za kiarabu ambao walikuwa wakipeleka taarifa na ikawa moja ya sababu ya kushinda kwa urahisi kabisa vita vile vya siku sita, kwani wahusika walijishi wayahudi zaidi kuliko utaifa wa mataifa waliyozaliwa. na ndio sababu pia Israel ilikuwa ikiwachunguza sana waisrel waarabu kiasi cha kutengeneza kikosi maalum kilichopelekwa kujipenyeza katika jamii hizo za kiarabu, japo ni raia waisreal lakini walihofiwa kutumiwa na mataifa ya kiarabu kutokana na uarabu wao.

nadhani ndio maana kipindi fulani tuna uhusiano wa kusuasua na nchi moja jirani watu walianza kuhoji wale wenye asili ya huko walio sehemu nyeti kama ikulu, ni kwa sababu kama hii

3.KULAZIMISHWA KWA KUTISHWA
Kutishiwa maisha ya familia yake au uhai wake. akaambiwa alete taarifa au siri juu jambo fulani ili yeye au familia iwe salama. mfano Mathilde Carre alikuwa member wa french resistance waliokuwa wakipamabana ufaransa uvamizi wa wa-nazi wakati wa vita ya pili ya dunia alikamatwa na nazis wamtishia maisha na akatakiwa akacukue taarifa awaletee wao.

4.KUTOKUTHAMINIWA
inaweza kujitokeza pale mtu anajihisi anafanya kazi nzuri na kubwa akihitaji kuthaminiwa lakini hawi appreciated akionekana mtu mdogo tu huku yeye akijiona bora kuliko wanaomzunguka. anaweza kuamua kwenda kwa mshindani ku-offer his service. mfano ni Robert Hanssen,alikuwa agent wa FBI akaamua ku-spy kwa ajili ya warusi kuanzia mwaka 1979-2001. huyu ni katika doube agent aliyeiumiza sana marekani kwa kuiba siri nyingi na kupeleka urusi, mfano kipindi hicho warusi walijua siri nyingi za kijeshi kiasi kama wangeingia vitani basi ilikuwa shughuli nzito sana kwa marekani. warusi walijua kila submarine ya marekani ilipo.

karibuni kwa michango

Asante kwa kutoa elimu mkuu
 
Kuwa Double Agent ni kitu hatari sana mkuu hawa Spies wakigunduliwa huwa wanauwawa kikatili sana...mfano mzuri ni Yule jamaa Aliyekuwa Spy wa RUSSIA then akaisaliti Moscow na kujiunga na Uingereza.

Alipewa sumu yenye mionzi na mpaka Leo CIA na MI6 YA uingereza wanatafuta clue jinsi alivyouawa lakini hawajaweza, wamebaki kuilalamikia RUSSIA tu!

Wadau mnaweza kuzigoogle picha zake mumcheki alivyoharibika Kia full story ipo Wikipedia[emoji3] [emoji3]
 
Nimeona sana CIA jinsi wanavotengeneza agent! Hasa double ajent kwanza wanastudy maisha ya MTU personal/private life then wanatumia zile sir nzito ulizokua ukizficha ktk maisha yako!

Hasa wenye siri kubwa ndo wapo kwenye risk!! Ukikataa wanakinukisha utakubali tu kama unataka ubaki kwenye cheo chako
 
Kwa kuongezea, kiujumla kuna scenario mbili za double agents,

Ya kwanza
kuna yule ambaye anajulikana yupo katika agency X na yuko loyal kwa agency X, ila anakuja kutokea agency Y na kumshawishi awape taarifa wao kwa sababu kama alizozitoa mleta mada (pesa, Sifa n.k). Hii huwa ni rahisi kwa mhusika kwani anakuwa huru kiasi fulani katika kuuza ama kupitisha taarifa zake kwa agency Y.

Ya pili
Hii inakuwa ni kwa wale maagent wanaokuwa katika agency X na anapretend kuwa yupo na X katika kila jambo wakati kiuhalisia yupo loyal na agency Y na anavujisha taarifa za X kwa Y bila X kujua. Hii aproach ni ngumu na inabidi ifanywe kwa ustadi mkubwa sana as agant huyu anakuwa hatarini sana katika kumaintain cover yake.

Ili kufanikisha hili kuna agency hufikia hata kurecruit/kupandikiza agents tokea wakiwa wadogo katika nchi ambazo wanataka kuvuna taarifa. Ili kufanikisha cover ups, kuna wakati taarifa zilizovunwa na undercover agent zinaweza zisitumiwe ili tuu coverup ya agent wao isigundulike huku wakizihifadhi taarifa hizo kwa matumizi ya baadae.
Hapa umenikumbusha strike back tv show season 5, hiyo case ya pili uliyoisema ni sawa kabisa na kiukweli ilikua ngumu sana sana waingereza kumgundua muhusika kwasababu alifanikiwa mpk kuwa mke wa balozi wa uingereza nchini Thailand kumbe behind the scene ni agent wa north korea alipofanikiwa alichokua anatafuta alirud kwao ingawa alikuwa ashashtukiwa.

Huyo mama alipandikizwa toka akiwa mtoto kwa manufaa ya taifa lake, aiseee strike back acha kabisa hii tv show, one of my best tv show!
 
Mada kama hizi naona zinaanza kuota ndevu humu mitandaoni,wenye kuona mbali watakua wamenielewa.

Dreva wa Carina na Dreva Volvo long -nose hawafanani taswira zao ingawa barabara ni ileile. eti unashare.
 
Kwa hizi nchi masikini hawa double agent nadhani wako wengi mno!!

Ila uzalendo ndio kinga mwafaka
 
Back
Top Bottom