Kuna movie ingine bab kubwa imetoka hivi karibuni inaitwa INSIDE THE MIND.
Humo wamo Gary Oldman, Tommy Lee Jones, Kevin Costner and binti Gal Gadot.
Hii movie inahusu harakati za CIA za kutaka kukwamisha shambulio la ugaidi, na tegemeo lao linawekwa kwa mfungwa mmoja ambae amepandikizwa kumbukumbu kwenye ubongo wake.
Hizo kumbukumbu ni za jasusi wa CIA ambae alikufa zamani akiwa kwenye harakati na aliecheza huyo jasusi anaitwa Ryan Raynolds.
Movie inaanza na Quaker Wells (Gary Oldman) ambae anacheza kama bosi wa CIA na anataka Jericho (yule mfungwa) afanyiwe majaribio ya kupandikizwa ubongo wa jasusi aliekufa.
Tatizo ni kwamba kila mbinu ambao Quaker anatumia basi Jericho yupo mbele hatua mbili.
Ni bosi kamili kabisa akiwa mjuzi wa kukabiliana na uhalifu lakini anakuja na hilo wazo la kupandikiza ubongo na anamtaka daktari wa upasuaji Dr Franks ( Tommy Lee Jones) afanye kazi hiyo.
Nae Dr Franks akiwa mwanasayansi anapenda ufundi wa kuchanganya mambo na majaribio na wazo la kuweka ubongo kutoka mwili wa marehemu kwenda kwa mwanadamu na hili lina matokeo yake ambayo hayatabiriki.
Akiwa ndani ya jela kwa muda mrefu akitumikia kifungo, Jericho Stewart (Kevin Costner) hakuona taabu ya kupewa nafasi ya kuonja jua la nje ya jela lakini kwa masharti ya kupandikizwa DNA na kuja kuwa jasusi wa CIA aliekufa ambae aliitwa Bill Pope ( Ryan Raynolds).
Lakini mambo yanabadilika kabisa kwa Jericho na anaona kila kitu tofauti na kuchanginyikiwa na hapo ndipo movie inapofikia kileleni pale anapokutana na Jill Pope (Gal Gadot) ambae alikuwa ndie mke wake Bill Pope.
Kwa kweli mwisho wa movie hii ni kinyume kabisa na matarajio ya Stewart na Dr Franks.
Movie hii bado haijafika kwa wingi kwenye soko la kimataifa lakini ipo njiani.