Sababu zipi zinapelekea mwanamke kujifungua kwa operation

Sababu zipi zinapelekea mwanamke kujifungua kwa operation

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Habari wanaJF

Wapo wanawake ambao hujifungua kwa njia ya kawaida ila kuna wengine hujifungua kwa operation nini kinapelekea wanawake kujifungua kwa operation? Kwa wajuzi mnaweza mkatiririka
 
Habari wanajf

Wapo wanawake ambao ujifungua kwa njia ya kawaida ila kuna wengine ujifungua kwa operation nini kinapelekea wanawakee. kujifungua kwa operation kwa wajuzi mnaweza mkatiririka
Kujifungua kwa upasuaji huwa mbadala endapo njia ya kawaida imeshindikana.

Ijapokuwa kuna baadhi kwa sababu zao binafsi huchagua kujifungua kwa njia ya upasuaji, lakini sababu kuu huwa ni kwa ajili ya usalama wa mama na mwanae.

Sababu zifuatazo hupelekea mama kujifungua kwa upasuaji;
1. Mkao usio wa mtoto tumboni. Kufikia wakati wa kujifungua, ni mategemeo kuwa kichwa cha mtoto ndiyo kitatangulia. Sasa inapofika mgongo ndiyo unatangulia basi upasuaji unapaswa kufanyika ili kupunguza uwezekano wa complications na hivyo afya ya wahusika.

2. Huwa inatokea kondo la nyuma kuziba njia. Kitaalam tunaita abruptio placentae. Yaani kondo linakaba njia badaa ya kumruhusu mtoto kutoka. Basi upasuaji huwa njia pekee ya kuokoa maisha ya mama na mwanae.

3. Matatizo ya mtoto tumboni. Yaani mtoto anaanza kutaabika Mapigo ya moyo kudunda bila mpangilio. Maana yake tunaanini mtoto yupo kwenye tabu. Sasa kuanza tena harakati za kumsukuma na harakati zingine za kujifungua kwa njia ya kawaida, basi kuna nafasi kubwa sana ya kufika akiwa mauti. Hivyo, ili kuokoa maisha yake basi upasuaji huchukua nafasi.

4. Cephalopelvic disproportion, ambapo mtoto anakuwa na kichwa kikubwa na mwili mkubwa kiasi cha kushindwa kupita njia ya kawaida. Kulazimisha kumpitisha ni kuhararisha usalama wake. Hivyo daktari hu-opt kufanya upasuaji wa haraka.

5. Magonjwa ya mama na historia ya upasuaji. Wagonjwa wenye presha wanashauriwa kujifungua kwa upasuaji ili kuepusha changamoto ambanishi. Lakini endapo ulijifungua kwa upasuaji basi daktari atazipima sababu za kujifungua huko. Kisha kwa maoni yake huamua kukushauri.

6. Sababu nyinginezo ikiwemo multiple gestations, kukwama kwa uchungu, nk.

Muhimu sana kusikiliza ushauri wa daktari na wataalam wa afya. Jamii imejijengea tabia ya UBISHI. Kuwa, madaktari kwa sababu zao wanaendekeza sana upasuaji.

Kwamba njia ya upasuaji inawalipa zaidi kuliko njia za kawaida. Kama ni kweli wanapaswa kukemewa mara moja. Waachane na tabia hizo za kipuuzi.

Ila jamii inapaswa kujua kuwa upasuaji huwa ni very risky. Si kwa mama na mwanae tu. Hata daktari anayeufanya. Unahitaji umakini wa kiwango kikubwa.

Kukosea kidogo tu ni pigo kwa mama na mwanae pamoja nawe. Kufutiwa leseni uliyoisotea kwa miaka 19+ na pengine kufungwa ni kugusa tu.

Kwa hiyo sidhani kama mtu yupo tayari kurisky mambo mengi kwa ulaji wa elfu arobaini. Wote tunaongozwa na nia ya kuokoa maisha ya mama na mwanae kabla ya yote.

Kuna upasuaji tunafanya na hatulipwi hata mia. Ila una furaha umeokoa maisha ya mama na mwanae.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Kiingereza hatukiwezi!

Kiswahili shida!

Lugha za mama zetu ndo kabisaa!

Yaani tupo tupo tu 🙌
20240622_212646.jpg
 
Back
Top Bottom