Jaribu kunielewa, Tumerithi Baraka za Abrahamu kwa kuwa yeye alihesabiwa haki kwa Imani.
Kama Torati/Sheria ina umuhimu kwa nini Yesu alikuja?
Jaribu kunielewa, Tumerithi Baraka za Abrahamu kwa kuwa yeye alihesabiwa haki kwa Imani.
Mkuu, mimi naamini wewe ni mtu mzima kabisa tena mpaka upo hapa Jf. Unaniona mimi nipo tofauti na wewe ktk Imani, kadhalika na mimi pia. Mimi bhana nilikuwa ni Mkatoriki halisi kabisa, nilipoanza kusoma sana Biblia nikaona mahali nilipo si sahihi na nikasema moyoni nipo tayari kubadilika kutoka kwenye Ukatoriki.Mwaka 2011 nikawa nasikiliza mihadhara ya dini kati ya Wakristo na Waislamu, matokeo yake nikaona Uislamu hauwezi ukanisaidia maana walizidiwa sana kwa hoja, nikasema bora nibaki zangu RC. Muda ulipita kidogo kisha nikarudi tena kusoma Biblia, safari hii nikawa nasoma sana UFUNUO WA YOHANA ghafla nikajikuta kuna dhamiri inanisukuma niokoke. Sikutaka kubishana sana na ile dhamiri kwani ilikuwa inalia sana, ilianza kulia mwezi wa 6 mwaka 2011, nikaja Nikaenda Kanisani Nikaokoka mwaka 2012 mwezi wa 7. Nilibatizwa nikiwa mdogo ila wakaniambia haya ni mambo ya Dini na Madhehebu, na mimi nilikubali moja kwa moja kwasababu niliamini baada ya kusoma Biblia. Baada ya hapo nimejikuta nikibadilika sana, mi najiona niko sawa ila watu walionizoea wananiambia Ongea yangu na matendo yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana. Mkuu, amini ninachokwambia, R/Mtakatifu ANAONGEA TENA ANA SAUTI KABISA, SAUTI YAKE NI YA UPOLE NA UNYENYEKEVU WA HALI YA JUU. Wosia wangu wa mwisho kwako ni huu 'Soma waraka kwa WAGALATIA WOTE, una sura 6 tu, wala sio nyingi, nina imani 98% utakusaidia sana Mkuu. Mimi siwezi kuuacha wokovu milele, nampenda sana Yesu maana pasipo ile Damu yake nisingekuwa hapa.
yani nyie wote mnaotoa matusi mnatakiwa mtubu kwa mungu kwa dhambi mnazochuma, mnakaa na kuanza kujadili imani za watu? ingekua ni waislam msingethubutu ht kdgo kutoa matusi mtoayo,ila MUNGU atafanya kaz yake, sis wasabato c watu wa visasi na matusi
ila we unachekesha, unajua hii nchi ina uhuru wa dini, kuwepo kwa wasabato wachache si kigezo cha kuwakandamiza imani zao. kusoma, kufanya mitihani siku ya sabato ni dhambi kwa msabato yoyote, basi na jumapili watoe hyo mitihani ili kuwe na usawa.
hii imekaaje wakuu, katiba iliyopo inazungumziaje issue hii!
Yesu mwenyewe alijiita yeye ndie Bwana wa Sabato. Tena akaivunja Sabato na akasema 'Nahitaji Rehema'.
Nimefuatilia mjadala huu tangu mwanzo, ila nimegundua kuwa wapo watu wana ushabiki na chuki zaidi kwa imani za wengine;
Kumbukeni kwamba kila imani/dhehebu imejengwa kwa misingi, kanuni na sheria. Kila dhehebu lina sheria zinazoliongoza. Seventh day kama kanisa, lina misingi yake, na nina imani kwamba hata makanisa mengine yanaongozwa kwa imani, sheria na kanuni zake.
Moja ya kanuni na sheria za kisabato ni kuitunza siku ya saba ya juma, hii imetoka katika amri za Mungu ambazo Yesu alipokuja hakutengua hata amri moja, yeye mwenyewe alisema ni Bwana wa Sabato, aliponya siku ya sabato kwa sababu lilikuwa ni jambo jema, aliokoa siku ya sabato kwa sababu lilikuwa jambo jema, hata leo hospitali za wasabato zinatoa huduma za afya siku ya sabato... KWA SABABU NI VYEMA JUTENDA YALIYO MEMA SIKU YA SABATO! wasabato wanawatembelea wagonjwa, wanawatembelewa waliofiwa, walioko magerezani, kwa vile ni mambo mema.
Serikali yetu haina dini hivyo kutoa uhuru wa kuabudu siku na saa ambazo kila mmoja wetu anawiwa. Kusomea vyuo visivyo vya kisabato haina maana kuwa msabato asiruhusiwe kusali siku ya sabato, uhuru wa kuabudu ndio tunaotaka. tedo, jaribu kuacha chuki na ushabiki dhidi ya imani zingine! Tuishi kwa amani na upendo, mwisho wa yote we are all Tanzanians!
Asante sana Mkuu! Leo Hawa wanaoupinga ukweli ningependa waingalie Imani ya Yesu kutokana kutokana na maandiko! Na Kama wataweza kumtoa Yesu katika hivi vitu vitatu! Law, testimony, prophecy!
Ili uwe huru kwako, nakushauri uazime Bible hata kwa Jirani, soma Waraka wa Galatia wote. Una Sura 6 tu, wala sio nyingi, utakusaidia sana kama ukiifungua moyo wako.
Ili uwe huru kwako, nakushauri uazime Bible hata kwa Jirani, soma Waraka wa Galatia wote. Una Sura 6 tu, wala sio nyingi, utakusaidia sana kama ukiifungua moyo wako.
yani nyie wote mnaotoa matusi mnatakiwa mtubu kwa mungu kwa dhambi mnazochuma, mnakaa na kuanza kujadili imani za watu? ingekua ni waislam msingethubutu ht kdgo kutoa matusi mtoayo,ila MUNGU atafanya kaz yake, sis wasabato c watu wa visasi na matusi