SABATO SABATO SABATO wanafunzi 8 wa teku wafukuzwa baada ya kukaidi kufanya mtihani jumamosi!

SABATO SABATO SABATO wanafunzi 8 wa teku wafukuzwa baada ya kukaidi kufanya mtihani jumamosi!

Status
Not open for further replies.
c umeona unarudi palepale kumbuka yesu alitoa msaada kwa kuponya siku ya sabato, vivyo hvyo hata leo, umeuguliwa na ndugu au jamaa waweza kumpeleka hospitali siku ya sabato kwani co kazi bali ni msaada. hlf kaka samahani me sio boya
 
Mkuu wasabato sio wakristu!!
Hivi Wasabato ni Wakristu?Anyway hata mimi wakati niko Mlimani miaka ile kuna wasabato waligomea mtihani jumamosi na waka-disco,walilalamika na kushauriwa kuwasilisha malalamiko yao kwenye senate,siku senate imekaa kupitia appeal yao proffesor mmoja akaomba tarehe ya barua ya malalamiko iangaliwe,ikakutwa barua hiyo iliandikwa siku ya Jumamosi,kumbe walivyotoka ibada siku hiyo ndi walikaa na kuandika appeal yao.Rufaa ikatupliwa mbali kwamba huyo ni Mungu gani anayezuia kufanya mitihani Jumamosi lakini akawaruhusu kuandika barua Jumamosi!
 
Umetoa maelezo mazuri sana kwa mtu mwenye hekima hawezi kukurupuka na kuanza kuwashambulia hao vijana na imani Yao! Na kuna mtu mmoja yuko hapa na mafungu Yake ya Wagalatia! Anapingana Na sheria! Nataka kumwambia hivi, kosa la wana wa Israel lilikua ni kumkataa Yesu mwokozi wao na kumsurubisha! Na kosa la wakristo wa Leo ni kuzikataa Amri za Mungu ambao ndo msingi wa Dunia na juu mbiguni! Sasa kazi Kwao hao wanaotaka kupingana na huu ukweli!

Sio mimi ila ni Paul ndiye aliyeandika.
 
Kati ya watu ninaowasoma hapa JF wanaoonyesha kuwa na chuki na wasabato wewe unaongoza, si mara ya kwanza hii issue ya wanafunzi wasabato kufukuzwa TEKU inaletwa hapa, na mara zote umekuwa mstari wa mbele kuwatukana kila aina ya matusi wasabato.Hivi inakusaidia nini unapoamua kuwaporomoshea matusi ama kuwakashifu watu ambao hawajakukosea chochote? ndio ustaarabu wa dini yako unavyokuelekeza au ni wewe mwenyewe umekengeuka?

Nataka nikufahamishe kwamba hayo ni mapito tu ya dunia na hao wanjafunzi unaowadhihaki Mungu atawafungulia mlango mwingine na watafanikiwa maishani. Tatizo kubwa ninaloliona kwako sawa na wenzako ni kutekwa na wimbi la ukristo mamboleo kiasi kwamba mnajikuta mnaisomma na kuitafsiri Biblia jinsi mnavyotaka ninyi ama mnavyofundishwa katika dini zenu na madhehebu yenu.

Watu wengi mnachanganya mambo kwa makusudi ama kwakutojua, unaposema ya kaizari mpe kaizari na ya Mungu mpe Mungu, hivi mnaelewa vizuri hicho kifungu cha Biblia ama mnajisikia tu kukiandika ili kukidhi haja zenu?

Umetoa mfano mzuri wa Chuo cha wasabato cha Arusha, je wanafunzi wanaosoma pale wanalazimishwa kuwa wasabato? Je wanafunzi wanaosoma pale wanalazimishwa kuingia madarasani ama kufanya mitihani siku za jumapili kwa nia ya kuwakomoa wale ambao ni wakristo wanaosali jumapili ilki wasiweze kwenda makanisani mwao kufanya ibada?

Natambua kwamba kuna baadhi ya watu wa dini fulani fulani hasa wanajiita wakristo lakini wanachuki mbaya dhidi ya wakristo wenzao hata kuliko wapagani ama waislamu. Na huu ndio mfano halisi wa watu wenye chuki na roho mbaya kwa kufurahia kuona wakristo wenzao wakinyanyaswa kwa sababu ya imani yao.

Wakati unapoendelea na kejeli na majivuno dhidi ya vijana wenzako wa kitanzania jaribu kusoma neno la Mungu kwa unyenyekevu na msaada wa Roho mtakatifu ili upte maarifa ya kulielewa neno la Mungu bila kulipotosha.

Kitabu cha Kutoka 20 kuanzia fungu la 8-11 kinasema hivi:

8Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, 10lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.

Mwita maranya! Pamoja sana Mkuu! Wale wote waliokua wanauponda usabato naona kasi Yao imeanza kupungua! Moreover.I also gave them my Sabbaths, to be a Sign between them and Me, that they might know that I am the Lord who sanctifies them! Ezekiel 20:12. Kumbe sabato ni njia ya kuweza kupata utakaso wa Mungu?! Haya kazi kwenu mnaopinga huu ukweli!
 
Hahha,haya mkuu,profesa,kuona mbali inategemea ni muono upi,anaweza kuwa kweli anaona mbali,lakini swali Je ni katika direction gani???
Ha ha ha ha ha Mkuu mi sicheki kuwa ni mazuri ila huyo Profesa anaona mbali sana.
 
Mwanakwetu ushie? Mli mwinza mwendi? Uli wha whi, karibu idimi mi msafwa niwe na ugomvi na nani?

Indaga. Khaya wha whirambo. Ngoja niache kuongea hiki kijrerumani nisije nikapigwa ban! Tuko pamoja.
 
kwa nini hao wasabato wasiende kusomea uinjilisiti ili wawe wahubiri? Ya kaisari wamwachie kaisari! Hivi hao wasabato wakiugua jumamosi hawaendi hospitali? Stupid kabisa!!!!!!!

Stupid_kabisa ndugu hilo tusi naimani mungu atakuwa na kufanya juu yako. Tusirumbane.
 
Last edited by a moderator:
SABATO!! Hii ndiyo dini ya ajabu kabisa duniani na ndiyo iliwafanya Wajita kuwa wabishi, majivuno, ujuaji, kudharau dini za wenzao na zaidi ya yote kuwa masikini. Wapare wana nafuu kidoogo maana kuna dini nyingi kubwa huko Upareni kama KKKT. Wao Wapare walibaki na ubahili ingawa ubishi pia wamo. Mimi siyo Mkabila lakini ukweli hiyo Sabato ilikoanzia imewaathiri watu wengi.
 
ila we unachekesha, unajua hii nchi ina uhuru wa dini, kuwepo kwa wasabato wachache si kigezo cha kuwakandamiza imani zao. kusoma, kufanya mitihani siku ya sabato ni dhambi kwa msabato yoyote, basi na jumapili watoe hyo mitihani ili kuwe na usawa.
Huwa tunafanya sana mitihani Jumapili, na Ijumaa pia. Sijawahi sikia wanafunzi wanakataa kufanya mitihani Jumapili sababu ni siku ya Bwana.
hawa Wasabato ndo zao kwenye vyuo vingi tu..... wanajidai wao ndo Wakristu kuliko Yesu Mwenyewe. Yesu alifanya kazi siku ya Sabato na hakuhesabiwa kuwa ni dhambi, sembuse wao.
 
ila we unachekesha, unajua hii nchi ina uhuru wa dini, kuwepo kwa wasabato wachache si kigezo cha kuwakandamiza imani zao. kusoma, kufanya mitihani siku ya sabato ni dhambi kwa msabato yoyote, basi na jumapili watoe hyo mitihani ili kuwe na usawa.

I second you.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom