Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi Wasabato ni Wakristu?Anyway hata mimi wakati niko Mlimani miaka ile kuna wasabato waligomea mtihani jumamosi na waka-disco,walilalamika na kushauriwa kuwasilisha malalamiko yao kwenye senate,siku senate imekaa kupitia appeal yao proffesor mmoja akaomba tarehe ya barua ya malalamiko iangaliwe,ikakutwa barua hiyo iliandikwa siku ya Jumamosi,kumbe walivyotoka ibada siku hiyo ndi walikaa na kuandika appeal yao.Rufaa ikatupliwa mbali kwamba huyo ni Mungu gani anayezuia kufanya mitihani Jumamosi lakini akawaruhusu kuandika barua Jumamosi!
Dini TUMELETEWA
Afande sele na mdogo wake Belle 9
Umetoa maelezo mazuri sana kwa mtu mwenye hekima hawezi kukurupuka na kuanza kuwashambulia hao vijana na imani Yao! Na kuna mtu mmoja yuko hapa na mafungu Yake ya Wagalatia! Anapingana Na sheria! Nataka kumwambia hivi, kosa la wana wa Israel lilikua ni kumkataa Yesu mwokozi wao na kumsurubisha! Na kosa la wakristo wa Leo ni kuzikataa Amri za Mungu ambao ndo msingi wa Dunia na juu mbiguni! Sasa kazi Kwao hao wanaotaka kupingana na huu ukweli!
Sheria ya Mungu mpaka Leo zinafaya kazi!
hii imekaaje wakuu, katiba iliyopo inazungumziaje issue hii!
Mkuu wasabato sio wakristu!!
Kati ya watu ninaowasoma hapa JF wanaoonyesha kuwa na chuki na wasabato wewe unaongoza, si mara ya kwanza hii issue ya wanafunzi wasabato kufukuzwa TEKU inaletwa hapa, na mara zote umekuwa mstari wa mbele kuwatukana kila aina ya matusi wasabato.Hivi inakusaidia nini unapoamua kuwaporomoshea matusi ama kuwakashifu watu ambao hawajakukosea chochote? ndio ustaarabu wa dini yako unavyokuelekeza au ni wewe mwenyewe umekengeuka?
Nataka nikufahamishe kwamba hayo ni mapito tu ya dunia na hao wanjafunzi unaowadhihaki Mungu atawafungulia mlango mwingine na watafanikiwa maishani. Tatizo kubwa ninaloliona kwako sawa na wenzako ni kutekwa na wimbi la ukristo mamboleo kiasi kwamba mnajikuta mnaisomma na kuitafsiri Biblia jinsi mnavyotaka ninyi ama mnavyofundishwa katika dini zenu na madhehebu yenu.
Watu wengi mnachanganya mambo kwa makusudi ama kwakutojua, unaposema ya kaizari mpe kaizari na ya Mungu mpe Mungu, hivi mnaelewa vizuri hicho kifungu cha Biblia ama mnajisikia tu kukiandika ili kukidhi haja zenu?
Umetoa mfano mzuri wa Chuo cha wasabato cha Arusha, je wanafunzi wanaosoma pale wanalazimishwa kuwa wasabato? Je wanafunzi wanaosoma pale wanalazimishwa kuingia madarasani ama kufanya mitihani siku za jumapili kwa nia ya kuwakomoa wale ambao ni wakristo wanaosali jumapili ilki wasiweze kwenda makanisani mwao kufanya ibada?
Natambua kwamba kuna baadhi ya watu wa dini fulani fulani hasa wanajiita wakristo lakini wanachuki mbaya dhidi ya wakristo wenzao hata kuliko wapagani ama waislamu. Na huu ndio mfano halisi wa watu wenye chuki na roho mbaya kwa kufurahia kuona wakristo wenzao wakinyanyaswa kwa sababu ya imani yao.
Wakati unapoendelea na kejeli na majivuno dhidi ya vijana wenzako wa kitanzania jaribu kusoma neno la Mungu kwa unyenyekevu na msaada wa Roho mtakatifu ili upte maarifa ya kulielewa neno la Mungu bila kulipotosha.
Kitabu cha Kutoka 20 kuanzia fungu la 8-11 kinasema hivi:
8Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, 10lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.
Unasoma Biblia?
Ha ha ha ha ha Mkuu mi sicheki kuwa ni mazuri ila huyo Profesa anaona mbali sana.
Aleyn! Nakuomba niendelee kufanya kazi! Ntarudi kwako Leo saa mbili na nusu usiku! Nakuomba uwepo on line! Thx
Mwanakwetu ushie? Mli mwinza mwendi? Uli wha whi, karibu idimi mi msafwa niwe na ugomvi na nani?
Indaga. Khaya wha whirambo. Ngoja niache kuongea hiki kijrerumani nisije nikapigwa ban! Tuko pamoja.
kwa nini hao wasabato wasiende kusomea uinjilisiti ili wawe wahubiri? Ya kaisari wamwachie kaisari! Hivi hao wasabato wakiugua jumamosi hawaendi hospitali? Stupid kabisa!!!!!!!
Huwa tunafanya sana mitihani Jumapili, na Ijumaa pia. Sijawahi sikia wanafunzi wanakataa kufanya mitihani Jumapili sababu ni siku ya Bwana.ila we unachekesha, unajua hii nchi ina uhuru wa dini, kuwepo kwa wasabato wachache si kigezo cha kuwakandamiza imani zao. kusoma, kufanya mitihani siku ya sabato ni dhambi kwa msabato yoyote, basi na jumapili watoe hyo mitihani ili kuwe na usawa.
Yesu mwenyewe alijiita yeye ndie Bwana wa Sabato. Tena akaivunja Sabato na akasema 'Nahitaji Rehema'.
ila we unachekesha, unajua hii nchi ina uhuru wa dini, kuwepo kwa wasabato wachache si kigezo cha kuwakandamiza imani zao. kusoma, kufanya mitihani siku ya sabato ni dhambi kwa msabato yoyote, basi na jumapili watoe hyo mitihani ili kuwe na usawa.