Sabaya afikishwa Mahakamani, Mawakili wake wasema Sabaya ni mgonjwa, yaahirishwa hadi Juni 20, 2022

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
KESI ya uhujumu uchumi na rushwa inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne, itatajwa kwa mara ya pili leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.

Ole Sabaya na wenzake, ambao ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antoro Assey, wanakabiliwa na mashtaka mapya saba, ikiwamo kuongeza genge la uhalifu, utakatishaji wa fedha, vitendo vya kuomba na kupokea rushwa pamoja ukiukwaji wa maadili ya kiutumishi.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, kosa la kwanza katika kesi hiyo ambalo linawahusu washtakiwa wote ni la kuongoza na kushiriki genge la uhalifu katika Wilaya ya Hai, Februari 2, mwaka jana.

Shtaka la pili, linamkabili mshtakiwa wa kwanza, Lengai Ole Sabaya, ambalo anadaiwa kulifanya Februari 22, mwaka jana, kwa kuomba rushwa ya milioni 30 kutoka kwa Godbless Swai katika eneo la Bomangombe, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Katika shtaka la tatu, Ole Sabaya peke yake, anadaiwa kujipatia rushwa ya milioni 30 kutoka kwa Elibariki Swai, kwa nia ya kuzuia taarifa za uchunguzi zilizohusiana na ukwepaji wa kodi.

Wakati shtaka la nne na la tano, linawakabili mshtakiwa wa pili, tatu, nne na tano, ambalo ni kumsaidia mshtakiwa wa kwanza (Ole Sabaya), kushawishi na kujipatia manufaa asiyostahili ya Sh. milioni 30 kutoka kwa Alex Swai, huku akijua ni kinyume na sheria.

Shtaka la sita linamkabili mshtakiwa wa kwanza (Ole Sabaya), ambalo ni ukiukwaji wa maadili ya utumishi, akiwa ni mtumishi wa umma katika Wilaya ya Hai, na shtaka la saba ni utakatishaji wa fedha, ambalo linawakabili washtakiwa wote.

========================

KESI INAYOMKABILI SABAYA YAAHIRISHWA HADI JUNI 20, 2022

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake 4 imeahirishwa mpaka Juni 20, 2022 kwa ajili ya kutajwa. Kesi hiyo imeahirishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Moshi Salome Mshasha.

Mawakili upande wa utetezi wakiongozwa wameiomba Mahakama kuharakisha upande wa Jamhuri kukamilisha ushahidi wao ili mtuhumiwa namba moja Sabaya akatibiwe uvimbe uliopo kichwani baada ya kupata ajali pindi akiwa kazini kwa kuwa ni mgongwa.

#JamiiForums
 
Yule wakili mrembo anayechangisha pesa ya mawakili wa Sabaya hajambo?
 
Kesi kubwa aliokuwa nayo Sabaya ni ile alioshinda rufaa. Hizi zingine ni kesi uchwara za kumchelewesha kurudi uraiani.
 
Mashtaka ya kitoto sana.
Heeh,ya kitoto wakati mwenzio analala sakafuni pale Jela Karanga,hata alipofikishwa Mahakamani mara ya kwanza Mei mwaka jana mlisema hivyohivyo kwamba Mashtaka ya kitoto lakini ameshamaliza mwaka mmoja Jela,jiridhisheni tu huku mitandaoni
 
Hata mimi nashangaa,unasema Mashtaka ya kitoto wakati mwenzako analala saa 12 jioni kwa Filimbi na kuamshwa saa 12 asubuhi kwa Filimbi,lile Bata alilozoea kulila pale Arusha kwenye mahoteli na maeneo mbalimbali ya starehe halipo tena halafu wewe unasema Mashtaka ya kitoto,akili zako zipo matakoni
 
Kesi kubwa aliokuwa nayo Sabaya ni ile alioshinda rufaa. Hizi zingine ni kesi uchwara za kumchelewesha kurudi uraiani.
Kumbuka Hukumu ya Kesi nyingine ile ni keshokutwa Ijumaa tarehe 10,iwe jua iwe mvua lazima agongwe miaka 30 Jela,wakati huohuo hii Kesi ya Moshi ndio kwanza inatajwa,kazi mnayo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
KESI ya uhujumu uchumi na rushwa inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne, itatajwa kwa mara ya pili leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.

Ole Sabaya na wenzake, ambao ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antoro Assey, wanakabiliwa na mashtaka mapya saba, ikiwamo kuongeza genge la uhalifu, utakatishaji wa fedha, vitendo vya kuomba na kupokea rushwa pamoja ukiukwaji wa maadili ya kiutumishi.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, kosa la kwanza katika kesi hiyo ambalo linawahusu washtakiwa wote ni la kuongoza na kushiriki genge la uhalifu katika Wilaya ya Hai, Februari 2, mwaka jana.

Shtaka la pili, linamkabili mshtakiwa wa kwanza, Lengai Ole Sabaya, ambalo anadaiwa kulifanya Februari 22, mwaka jana, kwa kuomba rushwa ya milioni 30 kutoka kwa Godbless Swai katika eneo la Bomangombe, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Katika shtaka la tatu, Ole Sabaya peke yake, anadaiwa kujipatia rushwa ya milioni 30 kutoka kwa Elibariki Swai, kwa nia ya kuzuia taarifa za uchunguzi zilizohusiana na ukwepaji wa kodi.

Wakati shtaka la nne na la tano, linawakabili mshtakiwa wa pili, tatu, nne na tano, ambalo ni kumsaidia mshtakiwa wa kwanza (Ole Sabaya), kushawishi na kujipatia manufaa asiyostahili ya Sh. milioni 30 kutoka kwa Alex Swai, huku akijua ni kinyume na sheria.

Shtaka la sita linamkabili mshtakiwa wa kwanza (Ole Sabaya), ambalo ni ukiukwaji wa maadili ya utumishi, akiwa ni mtumishi wa umma katika Wilaya ya Hai, na shtaka la saba ni utakatishaji wa fedha, ambalo linawakabili washtakiwa wote.
Mashitaka mazuri sn
 
Kesi kubwa aliokuwa nayo Sabaya ni ile alioshinda rufaa. Hizi zingine ni kesi uchwara za kumchelewesha kurudi uraiani.
Wewe wasema. Vilio vya wahanga wa mateso yake havitamuacha salama. Angetumia muda wake mwingi kuwaomba msamaha wahanga wa akili zake mbovu.
 
Mahakama imeombwa kusikiliza kwa haraka Kesi ya mh Ole Sabaya kwa sababu mtuhumiwa huyo ni mgonjwa.

Wakili wa Ole Sabaya amesema mteja wake ana uvimbe kichwani alioupata akiwa kazini

Source ITV habari
 
Nijuwavyo, mshitakiwa akiugua kesi inasogezwa mbele au inaghairshwe hadi apone... Hili la kusikiliza kesi kwa mwendokasi kisa mshitakiwa mgonjwa kwangu ni jipya.. Nirekebishwe kama nimekosea
 
Mahakama imeombwa kusikiliza kwa haraka Kesi ya mh Ole Sabaya kwa sababu mtuhumiwa huyo ni mgonjwa.

Wakili wa Ole Sabaya amesema mteja wake ana uvimbe kichwani alioupata akiwa kazini

Source ITV habari
Watu wanarahisisha kama vile wamempima na kuona anachoumwa, amesema anaumwa apewe nafasi ahudumiwe na madaktari,
 
Back
Top Bottom