Sabaya aliwahi nikata makofi wakati sikuwa mkosaji. Nimemsamehe

Riz king

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
276
Reaction score
549
Ilikuwa 2019 maeneo ya kwa sadala wilayani Hai kule kilimanjaro. Baada ya mkutano wa sambaratisha CHADEMA akiwa na wenzake Sabaya huenda alinifananisha na adui yake kisiasa. Aliniita kwenye gari lake pindi alivyomaliza mkutano. Aliniuliza maswali kadhaa kuhusu mikakati inayofanyika na CHADEMA huko maeno ya boma Ng'ombe, sasa nilikataa maana sikuwa najua lolote.

Ile sijakaa sawa aliniziba kibao cha usoni huku baadhi ya watu wakishangaa. Sikuwahi kuwa CHADEMA wala kujihususha na siasa. Nilisikitika na kulaani hilo tukio la kuaibishwa mbele ya umati. Sabaya akawasha ndinga lake v8 nyeusi huyo akatokomea.

Sabaya alivyokamatwa nilishangilia sana na kushukuru mtesi wangu huyu sasa apate cha moto kwa uonevu. Lakini hivi sasa nimejikuta namuonea huruma sana Sabaya, tumeumbwa kutolipiza. Koroho safi namuombea Sabaya anusurike na haya matatizo, kwani naamini kashajifunza sana na anayajutia aliyowahi yatenda.

Nimemsamehe kabisa kwa moyo mweupe Sabaya.
 
Ndio ubinadamu huo..
 

Afungwe maisha pumbavu mkubwa huyu, mbwa na nusu
 
JF imekuwa kama instagram nayo sasa. Soon kwenye comments tutaanza kuona matangazo ya vumbi la congo na waganga wa kienyeji kama mods wakifungia macho hawa watu.
 
Hivi kumbe Bado Mpo siyoeee
 
Ili uje uchapwe makofi Tena,

Huruma huwa ina mipaka yake usihurumie mijitu mingine isiyojielewa Wala kujitanbua utapata tabu Sana.
 
Nikikumbuka alichonitendea Lusubilo J. Mwakabibi nachagua kukaa kimya tu, sikuwahi kuwa na roho ya kisasi ila mabaya ya kuwakuta hawa mafedhuli kamwe hayatonipa huzuni
 
Asee pole sana mkuu kwa kudhalilishwa,, mungu analipa hapa hapa, si unaona na yeye wale mabwana zake aliokuwa akiwatumikia wamemlia mikabinyau kama hawamuoni vile
 
Wachaga kwenye kulinda CHADEMA mko imara Sana , kumbe ma-DC wanaendesha magari siku hizi

USSR
 
Asee pole sana mkuu kwa kudhalilishwa,, mungu analipa hapa hapa, si unaona na yeye wale mabwana zake aliokuwa akiwatumikia wamemlia mikabinyau kama kama hawamuoni vile
Dah huyu jamaa alinidhalilisha sana. Sjui kwa nn aliamua kunifanyia hvo. Wakat sjawah shiriki kwenye vikund vya siasa. Ila saahiz ukimuona anatia huruma sana bwana Sabaya
 
Wachaga kwenye kulinda CHADEMA mko imara Sana , kumbe ma-DC wanaendesha magari siku hizi

USSR
Mkuu sjawahi linda interest ya chama chochote.
 
Akafie jela mfiraji huyu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…