Sabaya aliwahi nikata makofi wakati sikuwa mkosaji. Nimemsamehe

Sasa anakunasaje vibao bila kosa na wewe unamuangalia tu?! Ningekua mimi leo ningeshaua na mm nafia jela au tushazikwa wote
 
hahaha kama vifurushi ni bei chee namna hii kwanini wewe huvitumii na unatumia namba ya simu ya nje ya nchi??
 
Dah huyu jamaa alinidhalilisha sana. Sjui kwa nn aliamua kunifanyia hvo. Wakat sjawah shiriki kwenye vikund vya siasa. Ila saahiz ukimuona anatia huruma sana bwana Sabaya

Unaona Sabaya ana dalili za kujutia kwa dhati makosa yake? Au huoni tabu akiachiwa akaja kukuzaba “shavu la pili”.
 
Sabaya afungwe maana katesa sn watu
Hivi katika uongozi wake aliishia kutesa tu watu bila kutatua kero zao?

Maana kila comment hapa ni mwendo wa kumlaani tu.

Ndo najiuliza hakuna aliowatendea mema wajitokeze na kuutetea wema aliowatendea?
 
Alikuzaba vibao vingap
 
Sasa anakunasaje vibao bila kosa na wewe unamuangalia tu?! Ningekua mimi leo ningeshaua na mm nafia jela au tushazikwa wote
Mkuu unazabwa makofi kama kawaida, utajichekeleza na kuondoka ukijipukuta vumbi na hauwezi kufanya chochote.

Kila sehemu mkuu wa wilaya anapokwenda huwa anatembea na timu yake ya ulinzi na usalama inayojumuisha DAS, msh JA, OCD,DSO na kakundi ka polisi wachache wenye silaha na pingu pamoja na mgambo viherehere, huwa hatembei peke yake.

Unapozabuliwa vibao na kuonesha kiburi ama hasira, utashangaa unavyopigwa kipopopo na mgambo viherehere wanaotaka sifa.

Fahamu na hasira zitakapokushuka utajikuta unachungulia kwenye tundu dogo la selo, uanze juhudi za kubembeleza kutolewa.

Tofari la chuki ulilolijenga moyoni litabomolewa pindi utapotolewa ndani na kuambiwa umesamehewa na usirudie tena ujinga wako.
 
Amini usiamini, kwa lofa kama Sabaya ninavomjua anichape kibao na nipo kwenye upeo wa 18 zangu nakuhakikishia ningempa mbata hilo potelea pote. Mkuu unafikiri kila mtu anaogopa mahabusu au je? Hamza alibeba SMG mchana kweupe na hakuogopa kitu.

Inapokua suala la kulinda na kutetea haki aisee dont underestimate response/reaction ya mtu.

Mzee ruksa mwenyew alikula kelbu sembuse sabaya?!?
 
Teh teh[emoji23][emoji23][emoji23]! Nimecheka sana waalah!

Hapo nilijaribu kukupa mbinu wanazotumia kudhibiti raia, kwa sababu mawilayani nimekaa sana na ninajua.

Kufanya ubabe kama unaousema ni sharti uwe umejiandaa kwa shari.

Lakini mtoa mada alikuwa ni kizurule hana hili wala lile maskini ya Mungu.

Ni ngumu sana mkuu kupigana na kundi ukiwa peke yako na ukashinda, ni ngumu sana.
 
Hivi si ni leo walisema hukumu yake, imekwendaje?
 
Kama vipi wafungwa wote waachiwe au vipi mkuu tuwasamehe
 
Kama vipi wafungwa wote waachiwe au vipi mkuu tuwasamehe
Sio hivyo mkuu saa nyingine tunasamehe tu. Sabaya anatia huruma sana na bahati mbaya alijizidisha mabaya sana tena kwa watu wengi sana. Atajibu siku ya kiama tu. Sabaya kwa waliokaa Hai ndo wanamjua ubovu wake. Yule jamaa sijui saikolojia yake iliyumba vipi. Ilifikia muda akikugundua wewe ni chadema analamba na wewe sahani moja. Kwangu mimi nilishangaa maana alivonikurupukia wakati sijawahi kuwa mfuasi wa siasa zozote pale Hai.
 
Na walioko huko sero wanatia huruma mkuu wengine wamekaa huko miaka zaidi ya 20, tuwasamehe wote mkuu watalipa siku ya kiama.
 
Na walioko huko sero wanatia huruma mkuu wengine wamekaa huko miaka zaidi ya 20, tuwasamehe wote mkuu watalipa siku ya kiama.
Sio kwa kusema wasamehewe wafungwa wote la hasha. Siko hapa kumuombea sabaya aachiwe na jamuhuri. Mimi nazungumzia tu upande wangu kuwa nimesamehe kwa ile dharau na udhalilishaji aliowahi kunitendea wakati sikuwa na kosa lolote ila hisia zake zilimtumaje sjui. Yeye akibambwa na majanga yake huko na akahukumiwa ni shauli yake lakin kiukweli upande wangu nmemsamehe huyu fedhuli
 
Watesi wa sabaya ivi wanakunywa bia leo Bar gani?
Na wale wasio wanywaji Wanatoa sadaka ya shukrani kwa miungu Gani.


Karma ni kiboko bwasheee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…