Lengai Ole Sabaya ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha amefunga utetezi wake leo baada ya mawakili wa jamhuri kumaliza kumhoji huku akiieleza mahakama kuwa anamiliki silaha aina ya Glock-17 kwa ajili ya kujilinda kutokana na kutishiwa kuuawa.
Akihojiwa na wakili wa Serikali mkuu, Tumaini Kweka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Odira Amworo wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha,Sabaya ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, amesema silaha hiyo alianza kuimiliki Machi 24, 2021.
Hata hivyo Sabaya kabla ya kutaja aina ya silaha anayomiliki aligoma akidai hawezi kueleza aina ya silaha anayomiliki mahakamani,ndipo wakili wake Mosses Mahuna alipoingilia Kati na kumwamuru aitaje.
Sehemu ya mahojiano hayo alikuwa hivi;
Wakili: Tusaidie katika ushahidi wako wa msingi umeieleza mahakama unamiliki silaha
Sabaya: ni sahihi
Wakili: Unamiliki silaha ya aina gani
Sabaya: Hakimu kwa sababu ni kifaa cha moto sijui kitatumikaje nikieleza kilivyo.
Wakili: Nataka kujua ni silaha
Sabaya: Kwa usalama wa silaha hiyo na kwa sababu nipo gerezani naomba nisieleze silaha gani. Ni silaha ndogo inaitwa Glock 17
Wakili:Utakubaliana na mimi kwa Kiswahili inaitwa bastola
Sabaya: Hapana
Wakili: Ulikua unaimiliki kwa shughuli gani
Sabaya: matumizi ya ulinzi binafsi
Wakili: Unapokuwa wapi
Sabaya: Ninapokuwa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro
Wakili: Hai ulikuwa una maadui
Sabaya: Ndiyo mheshimiwa hakimu
Wakili: Ulianza kumiliki lini?
Sabaya: Nilianza kuimiliki Machi 24, 2021
Soma zaidi:Ole Sabaya asomewa maelezo upya, akana
Wakili: Kwenye ushahidi wako wa msingi siku ukiondoka kuja Arusha Februari 9, 2021 uliacha silaha yako nyumbani Bomang'ombe.Ni sahihi siku ile ulikuwa ukimiliki silaha?
Sabaya: Sikuwahi kumiliki silaha ya moto kwa wakati huo nilikuwa na silaha ila haikuwa silaha ya moto
Wakili: Una watoto wangapi
Sabaya:Kwa sababu nimeshasema familia iko kwenye risk. Naomba nisitaje watoto wala idadi
Wakili: Lengai nikurudishe kwenye swali dogo wakati unatoka Hai saa 9 kuja Arusha na hiyo timu yako ulipita wapi
Sabaya: Nilipitia Kia barabara ya Mirerani nikaja Arusha
Wakili: Kwanini ulipita huko usipite barabara ya kawaida Moshi -Arusha
Sabaya: Napitia barabara yoyote kwa usalama wangu kwa sababu natishiwa kuuawa
Wakili: Kwanini ulikuwa unatishiwa kuuawa na wewe ni kiongozi wa watu
Soma zaidi:Sabaya amkana mshirika wake katika kesi
Sabaya: Kwa sababu ya aina ya majukumu niliyokuwa nafanya siasa za Arusha na Hai
Wakili: Umefika Arusha mlipokuwa mnaenea na timu yako alimkuta shahidi wa nne Hajirin Saad Hajirin, ulimuona?
Sabaya: Ndio nilimuoma hapa mahakamani
Wakili: Wewe unafahamaniana naye
Sabaya: Hapana
Wakili: Una ugomvi naye
Sabaya: Kama simfahamu siyo rafiki wala adui
Wakili: Na yule shahidi wa pili kutoa ushahidi wake akasema alikuona Shahidi Store (dukani) una ugomvi naye au unamfahamu?
Sabaya: Simfahamu na hapo Shahidi Store sipafahamu
Sabaya amefunga utetezi wake Leo baada ya kukamilika mahojiano ya upande wa serikali na baadaye upande wa utetezi ,mshtakiwa wa pili Silvester Nyegu anafuatia Kwa ajili ya kujitetea.
Katika shauri hilo la jinai nambari 105/2021 Sabaya anashtakiwa na wenzake wawili Daniel Mbura na Nyegu Kwa makosa matatu likiwemo la unyang'anyi wa kutumia silaha .
Ends...
View attachment 1898082