Sabaya asomewa mashitaka ya uhujumu uchumu, Atinga mahakamani akiwa amenyoa Kipara

Sabaya asomewa mashitaka ya uhujumu uchumu, Atinga mahakamani akiwa amenyoa Kipara

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Jambazi Lengai Ole Sabaya na wenzake sita leo wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusomewa mashtaka 6 ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa.

Ijumaa Oktoba 15 mwaka huu, Sabaya alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela pamoja na wenzake wawili baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha na makosa mawili ya kuunda genge la ujambazi.

Wakili wa Serikali Tumaini Kweka, amemwambia Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Patricia Kisinda, kuwa Jamhuri imeandaa jumla ya mashahidi 20 na vielelezo 16 katika shauri hilo namba 27 linalohusu tuhuma za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha zinazomkabili Sabaya na wenzake.

Washtakiwa wote saba wanadaiwa kujipatia kiasi cha TZS 90M kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mrosso. Imeelezwa mahakamani hapo kuwa Sabaya akiwa na genge lake walienda ofisini kwa Mrosso eneo la Kwa Mrombo jijini Arusha wakiwa na silaha za moto, ambapo walimtuhumu kufanya biashara bila kutoa risiti za EFD, na kudai kuwa mfanyabiashara huyo anaingiza vifaa kutoka nje ya nchi pasipo kufuata taratibu za ulipaji kodi.

Sabaya akiwa na bastola, na John Awenyo akiwa na bunduki aina ya SMG walimtisha Mrosso na kutaka awapatie TZS 100M ili wasimpe kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa.

Mrosso alisema hana kiasi hicho na kuomba awapatie TZS 50M lakini walisisitiza kupewa 100M. Baada ya majadiliano Mrosso alikubali kutoa 90M. Akasindikizwa na vijana wa Sabaya hadi bank akatoa TZS 90M na kumpatia Sabaya.

Washtakiwa wengine walioshiriki katika ujambazi huo ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Sabaya na wenzake wanatetewa na mawakili watatu wakiongozwa na Mosses Mahuna. Wakili "msomi" Mosses Mahuna ndiye aliyemtetea Sabaya kwenye kesi yake ya kwanza aliyopatikana na hatia na kuhukumiwa miaka 30 jela.

Sabaya amefikishwa mahakamani hapo na wenzake akiwa amenyolewa kipara, vijana wanaita zungu la unga kama ambavyowafungwa huwa wanayolewa kwa mujibu wa taratibu za magereza.

Katika shauri hilo la uhujumu namba 27,2021 washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Kosa la kwanza ambalo ni kuongoza genge la uhalifu na kosa la tano ambalo ni utakatishaji fedha, ambapo washitakiwa wote saba wanadaiwa kujipatia Sh90 milioni huku wakifahamu ni kosa.

Katika shtaka la pili, la tatu na la nne Sabaya peke yake ameshitakiwa kwa makosa ya kujihusisha na rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Tsh milioni 90 na matumizi mabaya ya ofisi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Kesi hiyo imeahirishwa hadi saa nane mchana ambapo shahidi wa tano ataanza kutoa ushahidi wake.

2968086_Aliyekuwa_Mkuu_wa_Wilaya_ya_Hai2C_Lengai_Ole_Sabaya_na_wenzake_sita_wanaokabiliwa_na_k...jpg

FB_IMG_1634568473085.jpg
 
Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Jambazi Lengai Ole Sabaya na wenzake sita leo wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusomewa mashtaka 6 ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa.
Aisee bado wanae
 
Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Jambazi Lengai Ole Sabaya na wenzake sita leo wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusomewa mashtaka 6 ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa.
Aisee bado wanae
 
Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Jambazi Lengai Ole Sabaya na wenzake sita leo wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusomewa mashtaka 6 ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa.

Ijumaa Oktoba 15 mwaka huu, Sabaya alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela pamoja na wenzake wawili baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha na makosa mawili ya kuunda genge la ujambazi.

Wakili wa Serikali Tumaini Kweka, amemwambia Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Patricia Kisinda, kuwa Jamhuri imeandaa jumla ya mashahidi 20
Aisee
20211018_140403.jpg
 
kwakweli maisha hayana usawa kabisa....yani jamaa alikuwa anatembelea magari huku akilindwa na walinzi wenye bunduki...leo hii yeye ndie anaelindwa na bunduki ili asitoloke...tutendeane mema jamani kesho yetu hatuijui...kifo cha mwendazake kimekuwa pigo kubwa sana kwa wengi...sijui bwana albert bashite yupo na hali gani huko aliko...

maana kwa ninavyomjua mimi bashite hivi sasa atakuwa yupo kanisani anajiliza tu...!
 
Anatia huruma jamaa...kipindi cha mwanzo kama alikuwa na uhakika atashinda sasa mambo yamemuendea mrama pole sana kijana.
 
Back
Top Bottom