econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Mshitakiwa namba moja Lengai Ole Sabaya katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili na wenzake amejikuta akitokwa na machozi mahakamani wakati akitoa ushahidi wake kama sehemu ya utetezi wake.
"Niliweka uhai wangu rehani kwa kufanya kazi za serikali,mpaka nikatumiwa watu kuniua" https://t.co/HkwBRDIo86View attachment 2088232
Cha kumshauri Sabaya aende kwa Hawa watu wawili Magesa Mulongo na Ndugai. Hawa watampa ushauri mzuri kuhusu CCM na serikali yake.
1. Magesa Mulongo alipambana na CHADEMA Arusha lakini alipotumbuliwa kwa kupigana na katibu tawala wa mkoa kwenye kikao hakuna anayemkumbuka kabisa amebaki Kama toilet paper.
2. Spika Ndugai alipambana na CHADEMA bungeni na kuwafanyia dhihaka za Kila aina na aibu zote ikiwemo kumtimua Lissu kwenye ubunge akidhani anaifurahisha CCM. Lakini siku alipoteleza ulimi, Ni CCM hao hao walimgeuka na kutaka ajiuzuru pamoja na kuomba msamaha lakini hakusamehewa.
Ukipewa nafasi serikalini watumikie wananchi sio chama.