Sabaya atoa machozi Mahakamani, adai aliweka rehani uhai wake kuitumikia Serikali mpaka akatumiwa watu kumuua

Mkuu Utingo ,sio kupenda kazi.
Kwenye kazi ya ukuu wa wilaya hakuna kutesa,kutishia,kula rushwa,kubaka,kudhulumu n.k.
Hiyo ilikuwa ni takwa na tamaa zake tuu.
Wapo Watanzania wengi wanapenda sana kazi lakini hawafanyi unyama wa huyo kilaza.
ni kweli usemayo lakini mengi ya uliyosema yanategemea na mtu mwenyewe. Unapokuwa na katiba inamruhusu dc amsweke mtu ndani kwa 24hrs kwa utashi wake tu. Unadhani ukipata dc kichaa hawezi akakusweka ndani ili tu pengine amtongoze/alale na mkeo?

DC wa sasa wa Hai alitoka katika mojawapo ya wilaya za mkoa wa songwe, huko aliacha kundi kubwa na watanzania waumini wa siasa za chadema, wakiwa lockup amewasingizia kesi ya kuua, akiulizwa mpaka leo walimuua nani, hawezi kuwa na jibu.

Hawa vijana wanapenda sana kazi na wanadhani wasipotesa watu wataondolewa katika kazi hizo. maana hata wakubwa wao wanapenda wanapoona vijana wao wanatesa wapinzania wao wa siasa.
 
ni kweli usemayo lakini mengi ya uliyosema yanategemea na mtu mwenyewe. Unapokuwa na katiba inamruhusu dc amsweke mtu ndani kwa 24hrs kwa utashi wake tu. Unadhani ukipata dc kichaa hawezi akakusweka ndani ili tu pengine amtongoze/alale na mkeo...
Watanzania tuamke tudai katiba mpya kwa nguvu zote
 
Anatafuta huruma, kulitumikia taifa kwa kuumiza watu na kupora mali zao pumbafu kabisa, nilichokiona ni kuwa ameamua kuondoa unyonge kama alikuwa nao awali ameamua apasue maana kama jela tayari anahukumu mkononi
 
Alitakiwa ajue. Kwa serikali yeye ni tool tu. Anaweza kuwa replaced and vanished muda wowote.
Inaonekanaalijiwekea uhakika 100%. Ndio haya yana mkuta
Alifikiri mtu aliyemchagua ataishi miaka yote ya "kipindi cha halali" na Ile miaka waliyokuwa wanapanga kumlazimisha aendelee nayo hapa duniani, ndiyo maana alijitanua kifua mno kwa sababu yupo wa kumkinga,na kuwaona wengine ni takataka.

Viongozi waliokuwepo awamu ya 5 wametunyanyasa sana kwa matendo na maneno yao,siku hizi kidogo kelele zimewapungua. CCM wasituletee tena viongozi wa aina Ile.
 
Watanzania tuamke tudai katiba mpya kwa nguvu zote
Tatizo viongozi wetu wanapandikiza maneno mabaya,eti katiba ni matakwa ya wapinzani sisi tunaleta maendeleo. Maendeleo yanakujaje wakati wanaofuja mali za umma sheria kwao hazina nguvu na haziwafanyi chochote?

Sasa kwa vile wananchi wengi hawajui maana na katiba ni kitu gani,ndiyo ugumu unapokuja wananchi hawana mori wa kudai katiba mpya. Wananchi wangekuwa na uelewa mkubwa na elimu juu ya katiba wote tungeimba wimbo mmoja: katiba mpyaaaaaa
 
Alitakiwa ajue. Kwa serikali yeye ni tool tu. Anaweza kuwa replaced and vanished muda wowote.
Inaonekanaalijiwekea uhakika 100%. Ndio haya yana mkuta
"MTUMISHI NI TOOLS YA SEREKALI,FUATA KANUNI NA MIONGOZO YA KAZI,UKIENDA NJE YA MIONGOZO NA KANUNI ZA KAZI, UKAPOKEA ZAIDI VIMEMO VYA FANYA HIVI FANYA VILE,HAPO BAADAE UTAUMIA TU MAANA UMEENDA NJE YA KANUNI ZA KAZI NA MISINGI YAKE"
 
Awataje hao watu ni kina nani na walitumwa na kina nani ili kumtoa uhai?Je,utumishi aliojitolea ni pamoja na kuwapora Watanzania wachapa kazi wanaojitafutia riziki zao kama kina Mrosso na wenzake?Alipewa na nani idhini ya kushawishi na kupokea RUSHWA?

Sabaya ni Afisa Mhalifu kwa vigezo vyote na hakustahili kuwa mtumishi wa serikali.

Eti DC Sabaya!
 
Alitakiwa ajue. Kwa serikali yeye ni tool tu. Anaweza kuwa replaced and vanished muda wowote.
Inaonekanaalijiwekea uhakika 100%. Ndio haya yana mkuta
Kuitumikia serikali ni kama mahusiano ya kimapenzi ya vijana siku hizi, kila mmoja amtumie mwenzake kwa timing,
 
Kabisa asee
 
Yakobo 1
13 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.

14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

Neno la Mungu!
Tumshukuru Mungu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…