Utingo
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 10,266
- 8,085
ni kweli usemayo lakini mengi ya uliyosema yanategemea na mtu mwenyewe. Unapokuwa na katiba inamruhusu dc amsweke mtu ndani kwa 24hrs kwa utashi wake tu. Unadhani ukipata dc kichaa hawezi akakusweka ndani ili tu pengine amtongoze/alale na mkeo?Mkuu Utingo ,sio kupenda kazi.
Kwenye kazi ya ukuu wa wilaya hakuna kutesa,kutishia,kula rushwa,kubaka,kudhulumu n.k.
Hiyo ilikuwa ni takwa na tamaa zake tuu.
Wapo Watanzania wengi wanapenda sana kazi lakini hawafanyi unyama wa huyo kilaza.
DC wa sasa wa Hai alitoka katika mojawapo ya wilaya za mkoa wa songwe, huko aliacha kundi kubwa na watanzania waumini wa siasa za chadema, wakiwa lockup amewasingizia kesi ya kuua, akiulizwa mpaka leo walimuua nani, hawezi kuwa na jibu.
Hawa vijana wanapenda sana kazi na wanadhani wasipotesa watu wataondolewa katika kazi hizo. maana hata wakubwa wao wanapenda wanapoona vijana wao wanatesa wapinzania wao wa siasa.