Sabaya mahakamani tena akiwa peke yake

Sabaya mahakamani tena akiwa peke yake

Dpp Kweka anatumiwa na matajiri wa kichaga kumchafua Sabaya wakati hana ushahidi wowote.

Mbowe alikutwa na kesi ya kujibu kutokana na ugaidi wake
Pole Sana mjane wa Sabaya
 
Usije ukakosa kujitokeza kukiwa na tangazo la kuwataka wenye matatizo ya akili kupewa matibabu bure.

Kukosa kuelewa hata kinachojadiliwa kinaashiria upungufu mkubwa katika utendaji kazi wa akili.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hii nchi vichaa ni wengi
 
ni mfano mzuri kuwa mbowe alikutwa na makosa vipi yupo nje
Kukutwa na kesi ya kujibu maana yake amekutwa na makosa? Hahaha...

Hii taaluma ya sheria tuwaachie wenyewe maana ni aibu kwa layman wa sheria kama wewe kwa hiki ulichoandika.
 
Jamani sasa basi kwa huyu kijana, yaani inatosha walahi
Ehh Mwenye Enzi Mungu mhurumie Sabaya ili aweze kuwa huru jamani uwiii [emoji31]
 
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Jumatatu Septemba 26 amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi akiwa peke yake.

Sabaya anakabiliwa kesi namba mbili ya uhujumu uchumi ya mwaka 2022, huku wenzake alioshitakiwa nao wakiwa wameachiliwa huru baada ya kukiri kosa na kuachiliwa huru Septemba 6 mwaka huu.

Washirika hao ni pamoja na Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey aliokuwa.

Makosa waliyokiri ni pamoja na kujitwalia madaraka isivyo halali na kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Alex Swai na kula njama, kumnyima na kukandamiza haki yake.

Mahakama hiyo iliwatia hatiani na kutoa amri ya kulipa kila mmoja faini ya Sh50,000 na fidia ya Sh1milioni kwa mlalamikaji Alex Swai.

Mwananchi
Kama kuna uonevu na kisasi ni kesi ya Sabaya. Wanaojidai kutetea haki za binadamu ndiyo wanazivunj. Huyu mkuu wa mashitaka hana aibu kuitumia offisi ya mashitaka kama mali yake. Ninayemulaumu ni Rais Samia kukaa kimya wakati watu aliyewapa madaraka wakionea Watanzania wenzao. Gaidi Mbowe alishitakiwa Kwa kutaka kuuwa viongozi wa serikali, Sabaya akiwa mmojawapo. Leo Mbowe yuko huru Kwa kutetewa na wazungu. Sabaya pamoja na serikali kukosa ushahidi inaendelea kumuweka Sabaya gerezani bila ya hatia Kwa miaka. Kisha, wanataka kumulazimisha akubali mashitataka ili wampe fine. Ni nani atakataa baada ya mateso hayo yote? Haki iko wapi? Kisha Rais anawaambia mawakili wasimamie haki huku yeye kama Rais haki invunjwa mbele yake bila ya woga!. Ni fedha za Mbowe na chuki Kwa Hayati Magufuli ndiyo vinavyomutesa huyu kijana? Ikiwa wapigaji wakubwa walioitia hasara Tanzania Kwa mabilioni Rugemalila na Sethi Wote wameachiliwa. Mukwepa kodi Mbowe karudishiwa pesa zake, Je Tanzania kuna sheria mbili? Za matajiri na masikini? Watamuweka Sabaya jela mpaka lini?
 
Back
Top Bottom