Sabaya yupo ndani, Mbowe yupo ndani na sasa Makonda anaelekea ndani

Sabaya yupo ndani, Mbowe yupo ndani na sasa Makonda anaelekea ndani

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Nilikuwa sielewi ule usemi wa sharia ni msumeno unakata ukienda na unakata ukirudi au unakata kote kote, sasa nimeelewa kumbe msumeno pia unakata nje hata ndani.

Tanazania inazidi kujipambanua kuwa nchi ya haki kwa mahakama zake kutenda haki bila kuangalia unatokea wapi.

Ole Sabaya mkuu wa mkoa mstaafu na kijana mchachali mchapa kazi sana na jeuri sana lakini vyote leo yupo katika mikono ya Pilato na tayari kala mvua ya miaka 30.

Freeman Mbowe ambaye amewai kuwa mfalme wa anga na mwenyekiti wa maisha wa chama cha Democrasia na maendeleo Chadema ambaye huko nyuma alikuwa aguswi lakini naye pia ameangukia katika mikono ya Pilato kwa kesi ya ugaidi inayomkabili.

Paul Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa mstaafu wa Dar es salaam ambaye alitamba katika medani za siasa za Tanzania kupitia ukuu wa mkoa leo amekuwa kipusa anasakwa kwa hudi na uvumba afike kwa pilato tayari kwa maisha ya kutumia ndoo kujissaidia kama wenzake.

Kwakuwa kesi zipo mahakamani, uharifu hauna chama, dini, kabila wala dhehebu pilato ndiyo kapewa lungu yeye ataangalia pa kupiga kama utosini, kiunoni hatujui au puani anajua yeye ila kwa sasa ngoma droo na maisha yanakwenda kwa kasi ya ajabu sana bandugu.
 
Makonda yupo mbali sana duniani anawacheki tu kwa binocular.. mnajipangaje 😉😉😉
 
Back
Top Bottom