SABC washangaa Rais Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake

SABC washangaa Rais Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake

Shirika la habari la South Africa walikuwa na mjadala kuhusu Mama Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake.

Hoja ya wachambuzi haikuwa kwa nini Tony Blair Bali ilikuwa credibility ya Tony Blair.

Wanasema Tony Blair hana credibility, hivyo kumteua kuwa mshauri ni kosa na wanashangaa imekuwaje Tanzania nchi iliyopigania ukombozi kufanya kitu kama hicho.

Mimi binafsi kwenye hili sijui hata nisimamie wapi maana sijui pa kuanzia, ngoja tuendelee kusubiri wajuvi wakilichambua kwa hoja.

View attachment 1987100
Tusiseme SABC bali tumlenge huyo Mama mwenye hoja. Sioni shida kupata ushauri kutoka kwa world reknown PR guru juu ya COVID 19 stance and other international relations issues especially kwa nchi ambayo 5 years ilichafuka kidiplomasia.

Whether Tony Blair aliunga mkono vita vya Ghuba kwa kumsapoti USA hilo ni suala jingine na halimfanyi asiwe consultant mzuri kwenye firm yake.

Lastly SA wana matatizo makubwa sana ya uchumi kuwa mikononi mwa weupe wachache, huku wao wanishia kuwa walevi na wavivu. At the same time migrant labour toka Zimbbwe, Mozambique na nchi zingine za kusini wakipata kazi na kutajirika wanawachukia na kuwafukuza au kuwaua.
 
Huo ni wivu tu,tony ni mjanha sana katika kutafutia nchi miradi na fedha

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Upo nchi gani wewe..? Hii picha si ya mwaka huu huyo muisrael ndo anaongoza ile tour ya mama ya kuutangaza utalii.. lile igizo sijui litatoka lini.

Hakuna utata hapo...😂
Hio style ya kushikana mikono haina utata??
 
Hivyi Corona ya Tanzania kweli ni ya kutafuta mshauri? Kumbe hiyo tume ya Corona ilikuwa na mazuzu watupu, ndio kaamua kuajili mzungu ambaye hata siyo daktari?

Atalipwa shikingi ngapi?
Huku ni kujipendekeza kwa wazungu matapeli.

Mzee wa Msoga unamuharibia Sana huyu mama.
 
Tusiseme SABC bali tumlenge huyo Mama mwenye hoja. Sioni shida kupata ushauri kutoka kwa world reknown PR guru juu ya COVID 19 stance and other international relations issues especially kwa nchi ambayo 5 years ilichafuka kidiplomasia.

Whether Tony Blair aliunga mkono vita vya Ghuba kwa kumsapoti USA hilo ni suala jingine na halimfanyi asiwe consultant mzuri kwenye firm yake.

Lastly SA wana matatizo makubwa sana ya uchumi kuwa mikononi mwa weupe wachache, huku wao wanishia kuwa walevi na wavivu. At the same time migrant labour toka Zimbbwe, Mozambique na nchi zingine za kusini wakipata kazi na kutajirika wanawachukia na kuwafukuza au kuwaua.
Hoja ya Tonny Blair haiishii hapo tu. Blair ndio alituuzia rada kwa Bei kubwa hadi waingereza wenzake wakaingilia kati
 
Kuna tatizo kubwa kama Mkuu wa nchi atakuwa na washauri peke yao walioelimishwa kwa fedha za multilateral institutions au taasisi za magharibi!!! Mlengo wao mara nyingi sio kuwa independent thinkers bali to always lean towards western interests na sio interests za nchi zao!!! Ni vema kama kiongozi akiwa na jopo [ diversity] la washauri hasa kwenye mambo ya uchumi kuliko kumtegemea kiumbe mmoja!!

Kuhusu uteuzi wa Tony Blair, mimi binafsi sina tatizo kutegemeana na nchi inataka nini kutokana na uteuzi huo. Katika miaka hii ya utawala wa Magufuli nchi yetu haikuwa na uhusiano mzuri na mataifa mengi hasa ya Ulaya na Marekani; hivyo ikaonekana kutokana na historia ya huko nyuma enzi za Mkapa, mtu pekee ambae anaifahamu vizuri nchi yetu na angeweza kutusaidia kurudisha uhusianao mzuri na nchi za nje ili kupata misaada hasa wa kupambana na covid 19 ni taasisi ya Tony Blair.
Tukumbuke kuwa huko nyuma akiwa Waziri Mkuu enzi ya Mkapa nchi yetu ilikuwa na ludo la madeni ya nje na ni huyu huyu Tony Blair aliyetusaidia kuwashawishi wadeni wetu kupunguza na hata kuyafuta madeni na nchi ikapata afueni. Ni kufuatana na historia hiyo na matatizo tuliyonayo na covid 19 ndio maana ikaonekana kuwaomba taasisi ya Tony Blair kutusaidia ni jambo la busara. Tukumbuke pia kuwa hizi chanjo za covid19 zinapatikana hasa kwenye nchi zilizoendelea na hasa marekani hivyo tunahitaji mtu anayekubalika na BIDEN iili kupata hizo chanjo!!!!

Tanzania sio nchi pekee ya Africa inayomtumia Tony Blair kwa ushauri. Majirani zenu wa Rwanda wamekuwa wanamtumia kwa muda mrefu sasa na wana matokeo mazuri
Uchambuzi mzuri unaoonyesha dalili zote za mtu aliyesoma halafu akaelimika. Nakuombea Mama akukumbuke siku moja hata kwenye post ya ubalozi mdogo ili ukasaidiane na Balozi wetu huko New York City
 
Bahati yako enzi ya JIWE ungewekwa kwenye kiroba!!! Mama amewafungulia sasa mnajinafasi sio nyie mabwege?
Ingekuwa hivyo humu kusingekuwa na watu kabisa. Jf imebaki salama siku zote, ndio maana hata wakati wa Jiwe tulimtukana vizuri tu humu.
Mama hajamfungulia yoyote, ukitaka kujua hilo tumia jina halisi Facebook au Instagram uone Kama atakuacha.
Juzijuzi tu katoka kukamatwa mchora katuni, yule daktari n.k
 
Wengine tulishaliona hapa na kuandika, hii ni fedheha sana,Blair ni tapeli la kimataifa, yeye ni mtu wa kupiga dili tu hana lolote, ana historia mbaya sana na hizo dili zake na hata Pandora Papers yumo kaficha pesa zake anazopata kwa kula rushwa .Na hiyo pesa ya msaada kwa ajili ya COVID itaishia kumlipa Blair. Sijui huyu tapeli atamshauri nini raisi wetu ambacho washauri wa raisi wetu wameshindwa kumshauri au hawakijui.
😁😁 Eti kwny Pandora yumo kaficha pesa zake za kula rushwa?Mlipoambiwa elimu elimu elimu mlibisha.Jifunze tofauti Kwanza Kati ya Tax Avoidance vs Tax Evasion.
 
Uchambuzi mzuri unaoonyesha dalili zote za mtu aliyesoma halafu akaelimika. Nakuombea Mama akukumbuke siku moja hata kwenye post ya ubalozi mdogo ili ukasaidiane na Balozi wetu huko New York City
Muongo huyo anasema kipindi Cha mkapa Tony Blair katusaidia kupunguza madeni wakati ndio alituuzia rada kwa Bei kubwa hadi waingereza wenzake wakaingilia Kati.
 
Hiyo TV inaongoza kwa ubaguzi walimfukuza kazi Robert Malawa kisa baba yake alikua Mzimbabwe na pana mpasuko na rushwa za kumwaga hapo ipo Tume iliundwa kuchunguza matatizo ya SABC sijafatilia majibu yake na taarifa za Xenophobia kipindi mashaba ndio meya wa Johannesburg hiyo TV ndio walikua wasambazaji wakuu wa uchochezi zile fujo hata mambo ya ukabila sijui Wakhosa na Wazulu zipo hapo siwafatilii kama TBC tuu wahuni hao...
 
Back
Top Bottom