Kuna tatizo kubwa kama Mkuu wa nchi atakuwa na washauri peke yao walioelimishwa kwa fedha za multilateral institutions au taasisi za magharibi!!! Mlengo wao mara nyingi sio kuwa independent thinkers bali to always lean towards western interests na sio interests za nchi zao!!! Ni vema kama kiongozi akiwa na jopo [ diversity] la washauri hasa kwenye mambo ya uchumi kuliko kumtegemea kiumbe mmoja!!
Kuhusu uteuzi wa Tony Blair, mimi binafsi sina tatizo kutegemeana na nchi inataka nini kutokana na uteuzi huo. Katika miaka hii ya utawala wa Magufuli nchi yetu haikuwa na uhusiano mzuri na mataifa mengi hasa ya Ulaya na Marekani; hivyo ikaonekana kutokana na historia ya huko nyuma enzi za Mkapa, mtu pekee ambae anaifahamu vizuri nchi yetu na angeweza kutusaidia kurudisha uhusianao mzuri na nchi za nje ili kupata misaada hasa wa kupambana na covid 19 ni taasisi ya Tony Blair.
Tukumbuke kuwa huko nyuma akiwa Waziri Mkuu enzi ya Mkapa nchi yetu ilikuwa na ludo la madeni ya nje na ni huyu huyu Tony Blair aliyetusaidia kuwashawishi wadeni wetu kupunguza na hata kuyafuta madeni na nchi ikapata afueni. Ni kufuatana na historia hiyo na matatizo tuliyonayo na covid 19 ndio maana ikaonekana kuwaomba taasisi ya Tony Blair kutusaidia ni jambo la busara. Tukumbuke pia kuwa hizi chanjo za covid19 zinapatikana hasa kwenye nchi zilizoendelea na hasa marekani hivyo tunahitaji mtu anayekubalika na BIDEN iili kupata hizo chanjo!!!!
Tanzania sio nchi pekee ya Africa inayomtumia Tony Blair kwa ushauri. Majirani zenu wa Rwanda wamekuwa wanamtumia kwa muda mrefu sasa na wana matokeo mazuri