TAARIFA HABARI YA USIKU ITV - MZEE ABDALLAH SABODO (Mwana-CCM tangu enzi za Baba wa Taifa) amekimwagia tena Chama cha Ukombozi wa Tanzania - CHADEMA mamilioni yapatayo 100 kwa ajili ya kukamilisha ukombozi wa Taifa hili.
MALAIKA WA MUNGU WANAZIDI KUJIDHIHIRISHA katika kukamilisha harakati hii ya kulikomboa taifa la Mungu lililoharibiwa kwa muda mrefu.
Mzee SABODO, anafaa kuitwa ni 'BABA MLISHI WA TAIFA HILI...Mpambanaji na kipenzi cha Ukombozi wa nchi hii'.
Mchango wake na dhamira yake nyeupe ni Baraka kamili na hii inaashiria nini?
* CCM wamepigwa na 'anguko kuu', na uchochezi wao eti CHADEMA ina mambo ya udini au ukabila ni kwamba wame-expire, maana Sabodo ni Muislam kamili, mzaliwa wa Lindi (na sio Kilimanjaro kama Mbowe au Ndesa) - na yeye ni mpinga Ukabila toka enzi za Baba wa Taifa, ndio maana yeye na Baba wa Taifa walikuwa pete na kidole. Kamwe hangeweza kutoa mchango kwa Chama chenye Ukabila au Udini!
* Wale Wafanyabiashara na Mafisadi wanaojipendekeza kwa CCM ndiyo wamepigwa na mshale wa moto kuwaonyesha kuwa Taifa litapata ukombozi kupitia gharama halali na nguvu halali ya Umma unaochangiwa na mtanzania wa kila rangi bila ufisadi.
* UCHOCHEZI SASA UMEFUNIKWA NA CHADEMA ni Chama cha Watanzania wote wenye dhamira njema, na hivyo kila mwenye Utashi mwema anapaswa kuutoa urithi au jasho lake halali kustawisha mafanikio ya Ukombozi na ujenzi wa Taifa letu na sio kupindisha ukweli, hila na unafiki.
MUNGU IBARIKI NCHI YETU, MBARIKI MKOMBOZI - DR SLAA, MJALIE MZEE SABODO NGUVU TELE, APATE KUFURAHIA UTAWALA MPYA UJAO ULIOJAA UMAKINI, AMANI NA USTAWI.