Kabisa Mkuu tizama walivyoisambaratisha Tanesco kwa kuingiza siasa ili walazimishe mikataba yao mbali mbali ya kifisadi. Mikataba ya IPTL, Escrow, Richmond, Umeme wa gas etc yote hii ilijaa ufisadi wa kutisha na haikuwa na maslahi yoyote kwa Watanzania bali kwa hili genge la wahuni ndani ya Serikali kuanzia fisadi Mkapa, Kikwete na huyu fisadi dhalimu. Matokeo yake Tanesco ambalo lilikuwa moja ya mashirika bora nchini sasa hivi limegubikwa na madeni makubwa mno na mikataba hiyo kusababisha Tanesco iendeshwe kwa hasara kubwa miaka nenda miaka rudi.