Sabuni ya jamaa na Tanzania ya viwanda

Sabuni ya jamaa na Tanzania ya viwanda

Kabisa Mkuu tizama walivyoisambaratisha Tanesco kwa kuingiza siasa ili walazimishe mikataba yao mbali mbali ya kifisadi. Mikataba ya IPTL, Escrow, Richmond, Umeme wa gas etc yote hii ilijaa ufisadi wa kutisha na haikuwa na maslahi yoyote kwa Watanzania bali kwa hili genge la wahuni ndani ya Serikali kuanzia fisadi Mkapa, Kikwete na huyu fisadi dhalimu. Matokeo yake Tanesco ambalo lilikuwa moja ya mashirika bora nchini sasa hivi limegubikwa na madeni makubwa mno na mikataba hiyo kusababisha Tanesco iendeshwe kwa hasara kubwa miaka nenda miaka rudi.
Point yako ni nini hasa ndugu? Unataka kusema serikali ndio imefanya viwanda vya sabuni visitengeneze bidhaa bora itakayoshindana katika soko la kimataifa? Nafikiri na sekta binafsi ina nafasi yake katika uboreshaji wa teknolojia na ubunifu.
 
Unilever ni third part company.anakuwa kama master supplier wa bidhaa nyingi.sio kwamba ndio watengenezaji
 
Nilichokiona katika uzi huu ni kwamba watu wameathiriwa vibaya na siasa kiasi cha kwamba baya lolote lile nchini basi lazima siasa ihusike. Sasa huu si werevu bali ni ujinga.
 
Kitu kingine Tanzania ni big consumer hivyo serikali km ina nia ya viwanda ijaribu kufanya ushawishi kwa baadhi ya makampuni makubwa kama jamaa kuja kufunga viwanda vyao huku ikiwa itatoka malighafi kutoka nje zitatozwa kodi kubwa kuingiza. Mimi naamini vitu vinavyotoka kenya ni very quality kuliko vya tanzania.kuanzia brookside,maziwa mazuri yale huwezi kufananisha na azam.

Au toss sabuni ya unga ufananishe na puff sijui ya mo dewji yaani very low quality kbs.au mafuta ya kupikia ya fresh fri ufananishe na safi yaani tofauti kabisa.mtanzania hajali quality anajali quantity tu!mi nshaachaga kutumia vitu vya kibongo bongo hata wali nakula pishori tu!huu mchele unaambiwa wa mbeya kula wanamix na kitumbo
 
Sabuni ya jamaa inayotengenezwa nchini Kenya imekuwa ikifanya vizuri sana kwenye soko hapa Tanzania kwa miaka mingi sasa, kiasi ambacho imezifunika sabuni nyingi sana za kufulia hapa nchini.

Swali langu ambalo nataka kuwauliza wadau, je, ni kweli watanzania wameshindwa kabisa kuanzisha viwanda bora vya ku-compete na sabuni ya jamaa?...kwa nini tuendelee kuwanufaisha majirani zetu miaka yote hiyo?
Sio sabuni tu,hata madawa na bidhaa zingine wenzetu wako vizuri,sisi ubabaishaji mwingi
 
Wametoa nyinhine inaitwa whitewash nayo ni bora kuliko jamaa, na bado wanaile takasa kwa hyo 1 ya kwao,2 ya kwao 3 pia yakwao
 
Kuna sabuni inaitwa "White wash" ya kipande, ipo vizuri japo cjui ni ya tz au kenya
 
Hivi kwann mnadharaugi toothpicks? Ungejua technology ya kuzitengeneza ilivyo ngumu ni mara 100 kuliko kutengeneza sabuni.
Sabuni hata watoto wangu wa darasa la nne kuna siku wakiamuaga wanatengenezea jikoni na tunafulia vizuri tu
Hakuna mtu aliyedharau kitu hapo mkuu,just facts tuu ,tatizo letu ni kwamba hatufanyi kitu to perfection,thats all,so iwe sabuni,stics or anything,thats what i ment mkuu
 
Mo Dewj alitengeneza sabuni kama Jamaa but ubora wake ulikua hafifu sana, hakudum hata sokoni.
 
Sekta ya binafsi ipi unayozungumzia!? Hii inayobambikiwa tax assessments kubwa kupita kiasi? Hujasikia kuhusu mabiashara zaidi ya 7,000 kufungwa nchini!? Hukusikia kauli ya Muhongo na hakuna aliyekanusha Serikalini kwamba Watanzania wanaweza biashara ya kuuza juice tu!? Serikali ndiyo tatizo kubwa nchini kwa sekta ya viwanda kushindwa.
Huenda ukawa sahihi kwa mtazamo wako.
 
Hii sabuni ya mbuni enzi za Chama kushika hatamu hazikuwa nyingi madukani. Tuliuziwa kwa ratio pamoja na sukari batterries, khanga na vitenge
 
Back
Top Bottom