Wakaguongo
Member
- Sep 23, 2026
- 95
- 38
Kwa mtazamo wa kwanza, hii inaonekana kama ishara ya kuongezeka kwa imani ya Wakenya katika SACCOs kama njia ya kuweka akiba na kupata mikopo.
Hatahivyo takwimu nyingine kutoka Kwa Mamlaka ya kudhibiti Saccos, yaani Societies Regulatory Authority (SASRA) zinaibua swali tofauti. Akaunti zinazolala(dormant )nazo ziliongezeka kwa 15.75% hadi kufikia milioni 1.69.
Kwa lugha nyepesi, wakati karibu wanachama 480,000 wapya waliingia kwenye mfumo, mamilioni ya akaunti zilizopo hazikuwa zikifanya shughuli.
SASRA sasa imezitaka SACCOs kuchunguza sababu zinazowafanya wanachama kutotumia akaunti zao na kutafuta njia za kuwashirikisha tena.
Na hapa ndipo takwimu hizi zinakuwa 'interesting'. Wanachama wengi zaidi haimaanishi moja kwa moja kwamba watu hao wote wanatumia huduma za SACCO kikamilifu. Mtu anaweza kuwa mwanachama wa SACCO, lakini akaunti yake ikawa haifanyi miamala kwa muda mrefu.
Hivyo kuna picha mbili zinazojitokeza katika sekta hiyo:
+480,000 - wanachama wapya.
1.69 milioni - akaunti dormant.
Je, Wakenya wanaendelea kuamini SACCOs, au baadhi wanafungua akaunti na baadae wanapoteza sababu ya kuzitumia?
Na kwa SACCO zenye mamilioni ya wanachama, ni nini kinachowafanya watu waingie lakini wengine wakaacha kushiriki kikamilifu?