SACP Augustino Senga: Wanaodai Nyeti zao zimepotea Tunduma Madaktari wamethibitisha zipo

SACP Augustino Senga: Wanaodai Nyeti zao zimepotea Tunduma Madaktari wamethibitisha zipo

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, alisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limefanya mikutano na wananchi kwa lengo la kutoa elimu na kutuliza taharuki iliyojitokeza, baada ya kuenea kwa uvumi wa kuwepo kwa watu wanaodaiwa kugusa wenzao na kusababisha kupotea kwa sehemu za siri hali iliyopelekea baadhi ya wananchi kujeruhiwa na watu wanne kupoteza maisha.

Hata hivyo Kamanda Senga amesema kuwa watu wote wanaodai Nyeti zao zimepotea Madaktari na Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa zipo, na hivyo kukemea vikali vitendo vya wananchi kuwashambulia watu kwa tuhuma zisizo na uthibitisho na kusisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Kamanda Senga amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati, pamoja na kuepuka kusambaza au kuamini taarifa zisizo na uthibitisho ambazo zinaweza kuhatarisha amani na usalama wa jamii.


 
1775302864650.png
 
Wachina wanahusika na biashara ya pini na rababendi

1775303155839.png
 
Back
Top Bottom