SACP David Misime awataka Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kuimarisha uhusiano na Waandishi wa Habari

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi nchini wametakiwa kuimarisha uhusiano na Waandishi wa habari ili kwa pamoja waweze kuelimisha jamii kuhusu miradi mbalimbali ya Polisi Jamii kwa lengo la kutokomeza uhalifu.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi yaliyokuwa yakifanyika mkoani Morogoro kuanzia Mei 3- 5, 2023.

Misime alisema Waandishi wa habari ni wadau muhimu katika kuhabarisha jamii hivyo ni uhusiano utakapoimarika itakuwa chachu ya kuifikia jamii.


Aidha, Misime aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa weledi na kujikita katika kutoa taarifa zenye tija kwa jamii inayowazunguka.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…