SACP Maigwa: Hakuna aliyejuu ya Sheria za usalama barabarani

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Simon Maigwa, amewataka madereva wa vyombo vya Serikali kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, akisisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, bila kujali nafasi au cheo alichonacho.

Akizungumza Oktoba 23, 2026, katika kipindi cha redio cha Moshi FM wakati akiendelea kutoa elimu kwa umma kupitia kampeni ya Ongea na Kamanda, Maigwa amesisitiza kuwa kila dereva ana wajibu wa kufuata sheria za barabarani ili kulinda maisha yake na ya watumiaji wengine wa barabara.

Aidha, Kamanda Maigwa amewataka askari wa Jeshi la Polisi kuwa mfano katika uzingatiaji wa sheria hizo kwa kuhakikisha wanamiliki leseni za udereva na kuvaa kofia ngumu (helmet) wanapoendesha vyombo vya moto vinavyohitaji matumizi ya kinga hiyo.

Ameonya kuwa askari yeyote atakayebainika kukiuka sheria za usalama barabarani atachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu zilizopo, akisisitiza kuwa hakuna atakayeruhusiwa kujiona yuko juu ya sheria.

Maelekezo hayo ni sehemu ya juhudi za Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kupitia kampeni ya Ongea na Kamanda katika kuimarisha nidhamu, uwajibikaji na usalama barabarani kwa watumiaji wote wa barabara.
 

Attachments

  • IMG-20261024-WA0211.jpg
    191 KB · Views: 5
  • IMG-20261024-WA0213.jpg
    351.9 KB · Views: 5
  • IMG-20261024-WA0209.jpg
    235.6 KB · Views: 6
  • IMG-20261024-WA0210.jpg
    234.5 KB · Views: 6
  • VID-20261024-WA0204.mp4
    19.5 MB
TRAKIFIKI WAPO KWA BARABARA KUKUSANYA FEDHA ZA VIKOBA SAIZI KILA KITONGOJI TRAFIKI YUPO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…