Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita , SACP. Safia Jongo amewaonya baadhi ya Waganga wa kienyeji ambao wamekuwa wakituhumiwa kuwatibu Wanawake kwa kuwarubuni na kufanya nao zinaa huku wakiwarekodi na kuwatishia kuziachia video hizo endapo wataachana, jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Hayo ameyaeleza katika Mkutano uliokuwa umeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita , katika kata ya Nyakagomba kwa lengo la kutembelea, kukagua miradi mbalimbali ya Serikali sambamba na kusikiliza kero za wananchi ambapo SACP. Jongo ameahidi kuwachukulia hatua wale wote watakao kiuka Maadili ya Kitanzania.