Sadaka itakayokuokoa siku ya Tabu

Hata kipindi cha manabii walioandikwa katika vitabu vyote vitakatifu....Kuna WAPUMBAVU waliwapinga.
 
Hata kipindi cha manabii walioandikwa katika vitabu vyote vitakatifu....Kuna WAPUMBAVU waliwapinga.
IPO Roho ya Ibilisi nyuma ya wanaopinga watu wasitoe sadaka na ZAKA.

Na wengi ni agents wa shetani, wao wanatoa sadaka Kwa Mizimu na Waganga na wanampa shetani vingi lakini wanawarubuni Wana wa Mungu wasitoe Ili waendelee kukaa kifungoni.

Mungu atusaidie.
 
Ubarikiwe na BWANA Mungu.
 
Umesomeka vyema.
Changamoto ni pale watumishi wanapozitaka kibabe,na kujipa uhalali as if wamezitafuta wao.
Hii,huathiri utoaji sadaka&zaka makanisani.
Binafsi huwa naziona baraka directly nikiwakumbuka wazazi,wajane,yatima,wahitaji&baadhi ya watumishi ambao huwa naguswa kuwapelekea..tena wakiwa hawajaniomba mimi,ila wamemwomba Mungu aliyewaita.
 
Umenena vyema.

Mtumishi wa Kweli halazimishi watu Kutoa sadaka,

Wa Kweli humwomba Mungu waumini wabarikiwe, kisha waguswe mioyo Kutoa Kwa ajili ya INJILI.

Kabla hata hujatoa Kanisani, mwangalie Jirani Yako, ikiwa ana shida msaidie.

Jirani analala njaa msaidie chakula, Jirani anaumwa msaidie, Si vyema ukawasha gari ukapeleka sadaka km 15 Kanisani, ilhali Jirani Yako amelala njaa na Hana uhakika wa kula.

Ubarikiwe .
 
Nimejifunza zaidi,barikiwa pia.
 
Umesema vyema mtumishi wa Mungu, lakini mbona Zaka ni 10% ya kile ulichopata
 
Mkuu Rabbon hongera sana kwa uzi wako, nimebarikiwa sana na hiyo sala ya toba, ingekua vyema kama hiyo sala ungeiweka kwenye kila thread yako humu, ata kama mtu mmoja atakiri kwa Mungu wetu ni ushindi mkubwa sana!!

Hakika tupo nyakati za hatari!!
 
Mkuu Rabbon hongera sana kwa uzi wako, nimebarikiwa sana na hiyo sala ya toba, ingekua vyema kama hiyo sala ungeiweka kwenye kila thread yako humu, ata kama mtu mmoja atakiri kwa Mungu wetu ni ushindi mkubwa sana!!

Hakika tupo nyakati za hatari!!
Ubarikiwe pia.

Thread nyingi nimekuwa nikiweka,

Na watu kadhaa wameokolewa na kumkiri Yesu kupitia maandiko Mungu anayonipa kuweka hapa.
 
Umesema vyema mtumishi wa Mungu, lakini mbona Zaka ni 10% ya kile ulichopata
AGANO la kale ZAKA ilikuwa 10%.

AGANO jipya ZAKA ni 100%, Mungu akamtoa mwanaye wa pekee,

Na Yesu Anamwambia yule tajiri, uza vyote ulivyonavyo Kisha wapewe maskini, ujiwekee hazina Mbinguni.

Sadaka na ZAKA AGANO jipya uongozwe na Roho mtakatifu. Si 10% pekee.

Ubarikiwe.
 
Lakini kafara kwa shetani mnatoa, unapoenda kwa mganga kupeleka kuku ndio sadaka
Wengine wanaua Hadi watoto wao Kwa kafara Ili wapate Mali za Giza.

Halafu hao ndio wa kwanza kudanganya watu wa Mungu wasitoe sadaka na ZAKA.

Mungu atusaidie Wana wa Mungu tuondokane na ukata Kwa Kutoa sadaka kufungua malango yetu ya kiuchumi,shukrani, na ulinzi katika siku za taabu.

Amen
 
Kuna kitabu nimeanza kukisoma kinaitwa RELIGIONS EXPOSED, aisee mpaka naanza kua na mashaka na Imani yangu na Kwa mbali naanza kumuelewa ndugu Kiranga
 
Hahaa. Kwa nini mkuu?

Tutaelewana tu polepole.
Jamaa ameongea vitu vingi sana vinavyofikirisha humo🤔 ndani. Mfano kama story ya Nuhu alivyoambiwa achukue pairs za wanyama awaweke kwenye safina. Inasemekana alikua middle east, sasa kuna wanyama wengine mfano polar bears , au kangaroo alikua anasafiri vipi hadi Australia kwenda kuwachukua nakuja kuwapakia? Na mfano mnyama kama tembo peke yake mmoja anakula tons of food per day same as rhino. Je, aliweza kustore chakula kiasi cha kutosha mfano kulisha species labda nne tu tofauti za rhino? And our God being all loving and merciful kwanini hakuna muua nyoka tusije wote kuja kua condemned? Na alivyomlaani nyoka kwamba atakua anatembelea tumbo, je before that alikua anatembea upright? Na nyoka kula dust is it true nyoka leo wanakula mavumbi? Bado naendelea kukisoma hiki kitabu aisee najifunza mengi sana. Mfano mamajusi waliiifata nyota iliyokua inatembea hadi ikawaonesha alipozaliwa masihi but in real sense nyota hazifanyi movement. Bado moyo unakua mgumu kusadiki what I have been told and my faith is based on fiction!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…